VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Wednesday, February 14, 2007
SIKU YA BIASHARA YA MAPENZI

Kwa walio wengi leo ni siku ya wapendanao.Ni siku ya kumuonyesha mwenzi wako kwamba wampenda,kwamba ungekuwa radhi kabisa kuweka kifua chako mbele ili kimiminiwe risasi endapo tu kwa kufanya hivyo ungeokoa maisha yake.Leo ni siku ya upofu (mapenzi ni upofu,hujawahi sikia wewe?). Leo ni siku ile ambayo Dr.Remmy Ongala anasema watu wapo radhi kula nyama mbichi,akiimaanisha penzi ni maajabu ya aina yake.

E
ndapo unashangaa kwamba kwanini katika mwaka mzima iwepo siku moja tu ambayo unatakiwa kuonyesha au kuadhimisha mapenzi yako kwa mwenzako,haupo peke yako. Upo nami katika kundi hilo huku pia nikiwa najiuliza kwanini mwezi huu wa pili wa mwaka,ambao ni mfupi kuliko miezi yote uwe ndio mwezi wa historia ya mtu mweusi. Kwa bahati nzuri hili la historia ya mtu mweusi sio la kidunia,bali la Marekani ya kaskazini zaidi. Ndio maana sitoshangaa kwamba huenda bado hujaisikia sana habari ya mwezi wa historia ya mtu mweusi.Inategemea sana uko wapi na ni kwa kiwango gani unafuatilia masuala ya dunia.

Siku ya wapendanao siku hizi sio tena kama ilivyokuwa hadithi yenyewe ya Valentino, hadithi ambayo wengi wetu hata hawajaisoma vizuri na hivyo kutuacha tukifuata mkumbo kama sio ushabiki. Siku hizi mimi naiita siku hii SIKU YA BIASHARA YA MAPENZI. Ninachokishuhudia mimi si mapenzi tena bali ni biashara.Badala ya maongezi,tafakuri,mahaba,kujitoa mhanga nk leo ni siku ya zawadi. Katika nchi za magharibi wiki hii nzima imekuwa ni wiki ya "mauzo" kama zilivyo siku za Christmas, Siku ya kinamama,kinababa nk. Kila utakapopita, kila utakachokisikia,kila utakachokiona hivi leo na wiki hii nzima kinalenga katika kukushawishi "utumie".Hivi huwezi kumuonyesha mwenzio mapenzi bila kutumia pesa au zawadi?Nashangaa!

K
inachoshangaza ni kwamba takwimu zinaonyesha kwamba mahusiano mengi sana ya mapenzi hufikia tamati hivi leo kwa sababu "hukuninunulia zawadi, hukunitoa out,sina gauni au shati jekundu".Yaani siku ya mapenzi kwa wengine ndio hugeuka kuwa siku ya vilio,chuki na hata kurushiana makonde.Pia wapo wale ambao hufumwa katika "njia panda" ya mapenzi wakitoa au kupokea zawadi kwenda au kutoka "nyumba ndogo". Leo ni siku ambayo simu za viganjani zinakuwa bize kupita kiasi.Ujumbe wa kheri ya siku ya wapendanao(siku ya biashara ya mapenzi) ndio unaotapakaa kuliko ilivyotapakaa tsunami.Michoro ya moyo ndio kama sala ya utakatifu wa siku.

W
akati nikifurahia kuona watu wakipendana na kuonyeshana mapenzi japo kwa mtindo huu wa ngonjera na maigizo(ni haki yao),ningefurahi zaidi kuona kwamba siku hii tunaitumia kwa kuonyesha upendo wa aina zingine pia.Upendo wa kujitolea kumsaidia jirani yako mwenye shida,upendo wa kumpa chakula na malazi yule asiye nayo. Ningependa unapompa mwenzio uaridi umkumbushe kwamba wapo mamilioni ya watoto wasio na baba wala mama na ambao wanahitaji msaada wake. Ningefurahi kuona wale watoto wanaoitwa "chokoraa" wakisaidiwa na sio kutukanwa na kukimbizwa huku anayefanya hivyo ameshikilia uaridi mkononi mwake.Mifano ipo kede kede na nikisema niiandike yote hapa tutakesha.Kwa hiyo kama unasheherekea siku hii au la sio vibaya ukaitumia siku hii kutafakari juu ya jinsi gani unaweza ukaipenda dunia au jamii yako pia.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:26 AM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 3:32:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MTANZANIA.

  Ni hatari Msangi!
  Siku hii imegeuka kuwa siku ya maambukizo.

   
 • Tarehe: 1:22:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Jeff, nimependa sana kichwa cha habari hii. Kichwa hicho kimeelezea kwa maneno machache hisia zangu binafsi juu ya siku hii. Kama kuna mtu hakupata salamu toka kwangu za siku hiyo, jibu unalipata hapa kwa Jeff.

   
 • Tarehe: 1:45:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Patrick GK

  Jeff,

  Wakati mwingine inabidi mtu ukubali yaishe maana ukibebea bango sana hizi sikukuu utajikuta unajenga hoja dhaifu kuzishutumu, halafu matokeo yake ukaonekana mlalamishi bure.

  Kwa mfano unapodai kuwa kwa nini kuwe na siku moja tu ya kuonyeshana mapenzi na mwenzako ukimaanisha Valentine's day hiyo kwa inakuwa siyo sahihi na wote tunafahamu hilo, mapenzi mnaonyeshana kila siku ila hiyo siku moja ni kama tu ya kuenzi jambo hilo.

  Hoja unayotoa ni sawa na kusema hata sikukuu zingine tusiziadhimishe mfano siku ya Kupambana na Ukimwi duniani ni Desemba mosi, lakini Ukimwi watu wanapambana nao kila leo sio siku hiyo tu(tena kadi za siku hiyo japo haijavuma sana si ajabu zikaanza kuuzwa) Hivyo Desemba mosi ni siku ya kuenzi hilo suala la kupambana na ukimwi.

  Mfano mwingine, pamoja na kuwa kuna "Siku ya Wanawake" haina maana kuwa siku nyingine zote wanawake hawatakiwi kuthaminiwa. Mifano ipo mingi tu ambayo ukiangalia unaweza kuona uwiano.

  Pili, katika ulimwengu wa leo karibu kila kitu ni biashara, pesa mbele. Wafanyabiashara hawajali ni siku gani we ukisema tu "siku fulani sikukuu" kosa... wao wanatafuta njia yoyote ile ya kutengeneza pesa.

  Sijui kama kuna siku ya ku-blog duniani? kama haipo basi siajabu inakuja lakini haitakuwa na maana kwamba siku zingine zote hutakiwi ku-blog. Nadhani umenipata.

  Cha msingi ni kuzitumia siku hizo kwa manufaa na siyo lazima uingie gharama yoyote ile.

   
 • Tarehe: 1:15:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Patrick,
  Kwa bahati nzuri au mbaya msimamo wangu ni huu huu hata katika hizo sikukuu zingine ulizozitaja.Kwa makusudi au kwa kuzidiwa na utandawazi,tumezifanya siku hizo kupoteza maana.

  Hoja ya msingi ni kwamba siku hizi zimeshapoteza maana tofauti na ilivyokuwa.Sio jambo baya kuwa na siku fulani ya maadhimisho au kilele.Tatizo linakuja kila kitu kinapogeuzwa kuwa "biashara" kama ilivyo hivi sasa.Tunajivika unafiki huku tukitambua.

  Pia lazima tukumbuke kwamba kuna watu ambao husahau kila kitu kuhusu jambo fulani (mfano mapenzi kwa mwenzio,kwa wazazi,ukimwi,uungawana,amani,uhuru nk) mpaka siku ya maadhimisho.Badala ya mambo haya kuwa ya kudumu yanageuka kuwa ya mara moja kwa mwaka kivitendo na hata tafakuri.Hapo ndipo utakapokuta kwamba watu wanasahau kwamba harakati au mapambambao dhidi ya ukimwi kwa mfano ni za mwaka mzima na sio Desemba mosi peke yake.Mifano ni mingi Patrick.Siwezi kukubali yaishe kwa sababu naamini tunahitaji kukumbushana kwamba kwa namna fulani wanadamu tunapoteza muelekeo.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker