VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, February 12, 2007
WAZIRI MWANAUME ANAPOJIANDAA KUOLEWA
Mojawapo ya masahibu makubwa sana ya kuishi nchi za watu (ughaibuni) ni pamoja na kukulazimu kushuhudia mambo chungu mbovu ambayo kiutamaduni na uzoefu ni tofauti na kule utokako.

Pamoja na kwamba mambo ya usenge yana historia ndefu pengine kuliko hata baadhi ya dini,katika siku za karibuni mambo hayo yamekuwa ya wazi(pengine kupita kiasi) na pia kuwa hoja nzito za kisiasa na haki za binadamu. Upana wa masuala ya haki za binadamu hapa Canada ni mkubwa lakini wakati huo huo usioeleweka. Tangu mwaka 2002 mahusiano ya watu wa jinsi moja ni ruksa.Lakini wakati huo huo biashara ya kuuza mwili (prostitution) hairuhusiwi.Kutembea uchi wa mnyama sio kosa.Uvutaji wa bangi na hata madawa ya kulevya sio ishu kubwa sana hapa Canada na ndio maana kuna hata zile sehemu ambazo watumiaji madawa wanaweza kwenda na kupimiwa kiwango kinachowatosha kulingana na afya zao. Ninachotaka kusema ni kwamba mambo mengi sana yanaweza yakakuacha kinywa wazi katika hizi nchi za watu na pia ni vigumu sana wakati mwingine kuelewa ni lipi hawa jamaa wanaloliona ni la misingi yao kama nchi na lipi au yapi wanayaona vinginevyo.

Leo hii waziri wa afya wa jimbo la Ontario ambaye pia ni makamu waziri mkuu wa jimbo hili pia,George Smitherman, ambaye ni msenge,ametangaza kwamba atafunga ndoa na mwenzie wakati wa majira ya joto mwaka huu.Ili uone jinsi gani mambo haya yalivyo magumu wanandoa wa jinsi moja wanaruhusiwa pia kuadopt mtoto kama wakitaka!

Pamoja na kwamba nchi nyingi za kiafrika zina sheria zinazopinga mahusiano kama haya ya watu wa jinsia moja(sheria zipo ili kupingwa?), upepo huu wa kuruhusu mahusiano ya jinsi hiyo yalishapiga hodi nchini Afrika Kusini na kwa maana hiyo yapo mbioni kuibuka kwa nguvu zote na hivyo kulipa bara la Afrika wakati mpya katika mazingira mapya.Ndiko tunakoelekea?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 8:46 PM | Permalink |


Maoni: 2


  • Tarehe: 5:33:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Simon Kitururu

    Nafikiri ndiko tunaelekea.Nafikiri tokea tushindwe kuwakatalia kuhusu demokrasia si mda mrefu tutashindwa kuwakatalia vitu kibao.Mugabe kabla ya ishu za mashamba ya wazungu alikuwa anasikika sana katika kugombana na Wasenge. Lakini wasenge ni wengi Afrika , ni kwa sababu tu hawasikiki sana kwenye vyombo vyetu vya habari.Hivi yule Anti Modi aliyekuwa maarufu Dar kipindi fulani yuko wapi?Nakumbuka alikuwa anakataa kulinda usiku kwa kudai atabakwa.
    Duh!Nimemkumbuka na Shaba Ranks jinsi alivyopoteza umaarufu baada ya kuanza kupigwa vita na wasenge. Hivi hili neno wasenge ni politically correct?

     
  • Tarehe: 4:43:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Egidio Ndabagoye

    Usenge Upo kila sehemu Bongo bado kuhalalishwa.Kuna kipindi niliwahi kwenda pale kwa Macheni ile kufika tu nashangaa navutwa shati kila sehemu na mibaba sio mibaba wadada sio wadada walikuwa wasenge,tangia siku hiyo sijawahi kurudi tena pale na ndio nilipoanza kuwafahamu hawa wasenge
    Hili neno Usenge naona poa tu sababu hata watu wa BBC wanatumia hili neno naona ni kiswahili sahihi

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker