VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, March 15, 2007
HIVI KWANINI?
Ukiniuliza kuhusu jambo moja ambalo linanikera sana kuhusu "ughaibuni" naweza nikawa na majibu kibao. Kutegemea na wakati naweza kukuambia kinachonikera hapa ughaibuni ni hadithi ya mtu kukuambia kwamba mambo yake safi sana kwa sababu amefanikiwa "kununua" nyumba bila kukupa ufafanuzi ambao utakupa jibu amefanikiwa "kukopeshwa" nyumba na wala sio kununua kama anavyojinadi.Deni hilo la nyumba atalilipa taratibu kwa zaidi ya miaka hata 20 au zaidi!Uwezekano ni mkubwa kwamba atastaafu (inategemea amekopeshwa nyumba hiyo akiwa na umri gani) na pengine hata kufariki akiwa bado anajikakamua kumaliza deni la nyumba. Deni la hapa halifutiki kirahisi, usipokuwa makini utarithisha watoto madeni.Hii ni tofauti kabisa na mahali kama Tanzania ambapo ukisikia mtu amejenga nyumba uwezekano ni mkubwa sana kwamba amejenga na hana tena deni na mtu. Nasikia siku hizi mikopo ya maisha kama hii huku inaanza kukua kwa kasi nchini Tanzania kutokana na utandawazi ambao umeleta mfumuko wa huduma za kibenki na mashirika mengine ya fedha.Kaa chonjo mwanakwetu.

Lakini kama kuna jambo linanikera kupita yote ni jinsi ambavyo vyombo vya habari ya hapa visivyojua au kutaka kujua kuhusu lolote zuri kutoka nchi kama Tanzania,Zimbabwe,Zambia au kwa kifupi bara zima la Afrika.Nimewahi kuandika kuhusu jambo hili mara kadhaa,linanikera na litaendelea kunikera.Wazungu wengi bado wanadhani Afrika ni nchi moja.Nchi moja ndogo yenye kila aina ya matatizo kama njaa,vita,ukimwi nk.Mara nyingi wanaiongelea Afrika utadhani wanaongelea kijiji cha Ungekuwawewe. Ukisikia jambo lolote kuhusu nchi yoyote ya kiafrika basi ni kitu kibaya. Majuzi kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe alipokamatwa na kupigwa na polisi wa Mugabe sio tu ilikuwa ni habari kubwa hapa magharibi lakini ilikuwa ikirushwa kana kwamba bara zima la Afrika limewaka moto na ndivyo tulivyo. Najua ushaanza kujiuliza;Je naunga mkono mambo kama hayo yatokee na yasilaaniwe na wapenda haki,uhuru na amani duniani kote?Hapana, na tena binafsi nalaani ubabe wa namna ya serikali ya Mugabe ambao bado unaendelea kuwa adui wetu barani Afrika na hata magharibi chini ya utawala wa viongozi kama G.Bush wa Marekani. Pamoja na hayo ninachotamani mimi ni balanced news. Mwaka jana nilimuuliza news anchor mmoja maarufu sana hapa Canada kwamba kwanini wao wanapenda kuonyesha mambo mabaya tu kuhusu Afrika na wala wasionyeshe lolote jema?Jibu alilonipa ni kwamba "ndicho watu wanachopenda kuangalia/kuona".Nakumbuka kumwambia kitu kimoja,kama nyie weupe mnapenda sisi hatupendi na wala haitufurahishi na lazima waheshimu hilo. Bado ningali kwenye vita hiyo na bado sina uhakika kwamba kama ni kweli ndicho tunachopenda kuona.Mimi sipendi!

Yapo mabaya chungu mbovu barani Afrika lakini pia yapo mema na mazuri. Tunaweza tusiyaone kwa sababu za kisaikolojia.Barani Afrika kuna upendo,watu bado wanasalimiana wakitaka kwa dhati kukujulia hali,wanatakiana kheri,wanatabasamu sio kwa sababu ndio masharti ya kazi zao.Watu bado wanasaidiana sio kwa minajili ya kupata unafuu wa kodi bali kwa sababu za kiubinadamu. Ukifiwa mahali kama Tanzania utaona ninachokiongelea,ukiwa na harusi au shughuli yoyote unachotakiwa ni kusema tu.Utasaidiwa.Hapa Canada nimeshahudhuria msiba uliokuwa na watu kumi na mbili tu. Nikimjua jirani yangu ni kwa sababu anataka kitu fulani kutoka kwangu au kinyume chake. Hali duni bado ni tatizo katika nchi nyingi za Afrika lakini hilo halijawazuia watu kuwa wakarimu. Ule usemi It Takes Village to Raise a Child bado una maana fulani katika nchi za Afrika(ingawa kuna ujuha umeingia wa kudhani kufanya hivyo siku hizi ni ushamba na kutokwenda na wakati). Hili huninyima raha kabisa kwa sababu wakati wenzetu wameshagundua kwamba waliwa wanakosea na washaanza kubadili muelekeo kwa kasi,sisi ndio kwanza tunaiga utamaduni ambao wenyewe wameshauona hauna mantiki.!Ndio sisi watanzania,ndio sisi waafrika.Jamaa mmoja ameandika kitabu na kuuliza ndio tulivyo?

Ingawa miradi mingi inaliwa na wanaojidai wajanja(dawa yao ishachemka,bado kuwanywesha) ipo miradi ambayo inaendelea.Nadhani kilio cha wananchi wengi ni kwamba viongozi wapunguze uroho na ukibaka ili maendeleo yawe ya kasi zaidi ili serikali isiwe "tatizo letu" kama ilivyo hivi sasa.Wako vijana wenye muamko,walio na bongo zinazochemka,wavumbuzi.Wapo watu wenye utu,wanaojali jamii zao. Wapo watu ambao naamini uongozi ungewapa mazingira yanayoeleweka wangefanya miujiza.Zipo rasilimali ambazo ni vigumu kuzipata sehemu yoyote ile duniani zaidi ya ndani ya nchi za kiafrika. Tunayo mengi ya kujivunia na kwa maana hiyo vyombo vya habari vya magharibi vinayo mengi mazuri ya kuripoti. Vinapochagua mabaya tu tusikae kimya na wala tusijikombe.Hatujisaidii kwa kujidai hamnazo.

Nani tumlaumu? Je, ni sisi wenyewe ambao tumekubali kuendelea kushikiliwa na minyororo ya utumwa wa kiakili? Je sisi ndio chanzo cha habari zote mbovu kuhusu nchi zetu?Ukiulizwa kuhusu nchi yako unasemaje? Unaanza kwa kuelezea mazuri (hata kama unadhani ni machache) au unaanza kwa kulia njaa? Wakati mwingine huwa najiuliza hivi raisi wetu akikutana na viongozi wenzake wa nchi zingine anaanza vipi mazungumzo yake? Nini inakuwa salamu yake? Akiulizwa "How is Tanzania doing Mr.President?" anajibu nini?

Najua wakati mwingine inakuwa ngumu kukubali au hata kuona lolote jema linalofanyika ndani ya nchi zetu.Nyingi zimejaa rushwa,mipango mibovu ya kimaendeleo,viongozi wanaotamani wasingezaliwa Afrika maana hata kukaa nchini hawataki,kutwa wapo safarini.Kila mtu serikalini anatafuta fursa ya kwenda nje eti kubadilishana uzoefu na kujifunza wenzetu walivyofanya.Uzushi mtupu. Lakini je ni kweli kwamba hakuna lolote jema kabisa? Je ni kweli kwamba nchi zetu zote za kiafrika ni uwanja wa fujo, mshikemshike,mbinde kila kukicha, kila kukicha heri ya jana? Vyombo vyetu vya habari, sisi wanablog,wewe msomaji,wewe mwananchi unasemaje?Mtazamo wangu umeshausoma hapo juu.

Ndesanjo aliwahi kuuliza siku moja,now that we have got blogs,what are we gonna do with them? Ndesanjo alikuwa akiongelea muungano na muelekeo mpya wa blogs kama nyenzo mpya ya mabadiliko ya jamii. Mabadiliko hayo yalijumuishwa vizuri na BBC wiki chache zilizopita walipouliza can we rebrand Afrika? (samahani sijapata kiungo cha habari hii) Napenda kuamini kwamba inawezekana hata kama wengine mnadhani tumeshachelewa sana.Lazima sisi watanzania/waafrika tuanze kuonyesha picha tofauti ya kuhusu nchi zetu/bara letu.Kama tunakubaliana kwamba blogs ni nguvu mpya ya umma basi hatuna budi kuitumia.Kumbuka kwamba sisemi kwamba tusionyeshe mabaya yetu ila ninachosema ni kwamba tuonyeshe mazuri pia(ikiwezekana mengi zaidi) na pia wakati huo huo tuonyeshe mabaya ya wenzetu na ikiwezekana mazuri pia ambayo yanafaa kuigwa. Huo ndio uundwaji mpya wa jamii katika dunia ambayo inazidi kuwa kama kijiji.

Ombi: Kama unayo picha au unazo picha zinazoonyesha shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania, shughuli chanya za utalii,sanaa,michezo, maisha au lolote lile jema,lolote lile unalodhani vyombo vya magharibi visingependa kulionyesha tafadhali nitumie kwenye e-mail jeffmsangi@sympatico.ca na mimi sitosita kuziweka kwenye blog zangu hususani ile ya kiingereza ya proudafrican.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:39 PM | Permalink |


Maoni: 7


  • Tarehe: 9:26:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff, ni kweli. Unakumbuka Mwalimu Nyerere alikopa pesa benki kujenga nyumba yake ya Msasani? Deni lilikuwa gumu hadi 'akaona watoto watakufa njaa,' akaomba serikali iijenge na kuimiliki nyumba hiyo iwe ya rais, si Nyerere. Lakini serikali ya Mwinyi baaday eiliona aibu, ikampa kama zawadi nyumba hiyo. Nyerere alikuwa na uwezo wa kujenga bila mkopo, kwani raslimali za taifa zilikuwa nje nje, miongoni mwa wajinga. Hakufanya hivyo. Aliweka mfano ambao waliomfuata hawakuufuata. Siku hizi watu (maofisa wa serikali) wanaolipwa shilingi laki 2 kwa mwezi, wanajenga nyumba kubwa za kifahari bila mkopo benki na bila deni na mtu yeyote. Wanazipata wapi? Ni zao? hapo ndipo tulipo!

     
  • Tarehe: 6:47:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    ukiwa europe maeneo ya UK deni linafutwa baada ya miaka 6 na unakuwa safi bila na ata deni moja baada ya hapo.

    Njia nyingine ambayo kama hautaki kusubiri miaka 6 ni kujitangaza bankruptcy na kufutiwa madeni yote na kuanza upya ingawa itakuwa vigumu kupata mikopo tena.

    Njia ya kwanza ukifuata utapata tena mikopo.

     
  • Tarehe: 5:12:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger MACHWEO

    Ngurumo anashangaa kuhusu wafanyakazi wenye mshahara mdogo lakini wanamiliki zaidi ya kile kinachomaanisha mshahara wao! Nyote si wageni na wala si lengo langu kuonesha kuwa rushwa afrika inatula na kuwaneemesha wachache huku wengi tukiwa tunaumia kwa kukosa muhimu yaliyokombwa kwa rushwa. Mshahara kwa baadhi ya wafanyakazi si kitu, kinachothaminiwa sasa ni nafasi uliyopo inakuwezesha 'kuwasiliana'. Mikopo ipo lakini si wote wanaoweza kuipata hasa wale walio mbali na jiji na miji mikubwa

     
  • Tarehe: 2:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Patrick G. Kamera

    Mzee Jeff,

    Sijaona sababu ya msingi ya "kukerwa" na mtu kukuambia mambo yake safi kwa kuwa kanunua au "kakopeshwa" nyumba.

    Kama unavyofahamu piga ua ukiishi huku "ughaibuni" lazima utakuwa unalipa pango au mortgage, sasa kama utaishi miaka kadhaa, kipi bora, kupanga nyumba au "kukopa" nyumba? Vile vile kumbuka kuwa hiyo nyumba ukiamua kuiuza kabla ya kumaliza deni bado utaondoka na kianzio kizuri tu kwa hiyo bado utakuwa unapeta si unajua masuala ya equity(I guess ndio "mambo ya mtu kuwa safi" hayo) tofauti na ukipanga ambapo utaondoka mkavu!

    Nakumbuka Tanzania tulikuwa na benki ya nyumba (THB) ambayo ilikuwa inatoa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, leo hii ni historia...

    Ujenzi wa nyumba Tanzania uzuri wake ni kuwa ukimaliza huna deni ila ukijenga kwa mshahara wa serikali kihalali si ajabu ukamaliza baada ya miaka kibao vilevile au ukahamia na wala usiimalizie nyumba ukakubali tu yaishe. Ila ukiwa na mshahara wa NGO au mashirika ya nje au ukiuza nyumba yako huku ukadondoka na kianzio chako basi ujenzi utamaliza mapema mradi kusiwepo na migogoro ya viwanja.

    Kwa habari za runinga za magharibi kuhusu Afrika ni ukweli usiopingika kuwa hawataki kuonyesha mambo mazuri, wao wanataka watazamaji, wasikilizaji na wasomaji wao huku waendelee kuwa na picha potofu ya Afrika ili wao waendelee kupeta.

    Hushangai wanaweza kuonyesha watu wako hoi bin taabani yaani hali mbaya kweli, mazingira machovu mno ila hawaonyeshi wao waandishi wa habari na wapiga picha wao wamefikia wapi na wanaishije kwenye hizo hizo nchi za Kiafrika wanajua wakifanya hivyo tu hata zile "hardship allowances" zitapungua kama siyo kufutika kabisa, hivyo wao pia wametanguliza maslahi yao binafsi mbele.

    Nakumbuka Will Smith aliwahi kusema kwenye interview moja baada ya kutoka Afrika Kusini kuwa hakutegemea kuona maendeleo aliyoyaona maana alivyofundishwa toka mdogo shuleni ni kwamba Afrika kuchovu sana alisema "I was misinformed to the point of being lied to" na tangia hapo akaamua kuwa atakuwa anapeleka familia yake kutembea Afrika mara kwa mara ili watoto wake waujue ukweli na nadhani amenunua nyumba huko Afrika Kusini, sasa huyo ni mmoja tu, wako wengi bila shaka.

     
  • Tarehe: 2:51:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Imekuwa zaidi ya habari kubwa kupigwa kwa kibaraka wao zimbabwe! sijui kama wakitokea watu waanze kuandamana Newyork, Montreal, London na kwingine kwa aina hiyo kwa lengo la kuiangusha serikali kama watatoka salama!
    Kumbuka historia ya London, Liverpool miaka ya mwisho ya sabini na mwanzoni mwa themanini, weusi walipoandamana kudai kutendewa haki kama wengine polisi walifanya nini? Marekani ndiyo usiseme, Juzijuzi kijana wa kibrazil katwangwa risasi kwa kukataa kusimama aliposimamishwa na polisi, mwaka jana/juzi ufaransa waliwafanyia nini wageni waliokuwa wanaandamana kupinga hali wanazowekwa, bado hatujasahau mambo ya Denmark wiki iliyopita wananchi walioandamana kupinga kuvunjiwa nyumba zao, Iraq na Afghanistan mambo yanyofanyika huko hawayasemi kwa undani. Haya yote hayakuwa habari kubwa ila ya kupigwa kwa Morgan ndiyo ipewwe nafasi kubwa kiasi hicho au ilitumika kufunika mambo ya Denmark?
    Wanatakiwa wajue historia ya Zimbabwe na kwa nini Mugabe wanayemchukia anashinda uchaguzi ndiyo wafikie maamuzi yao.

     
  • Tarehe: 10:45:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Mloyi, UMENENA.

    TUSIWE BENDERA KUFUATA UPEPO, MUGABE KWELI NI MZEE, LAKINI MSIMAMO WAKE, MIMI SINA WASIWASI NAO. HAPENDI VIBARAKA.

    ETI THAMANI YA FEDHA IMESHUKA KWA ASILIMIA 1700.

    SHVANGIRAI ATAIPANDISHA KWA VIPI!
    YAANI KWA MISAADA! AU!

    HAKUNA MWANAUME YEYOTE CHINI YA HII MBINGU ATAWEZA KUKUSAIDIA HIVI HIVI, LABDA NDUGU YAKO KWA BABA NA MAMA MJOMBA AU SHANGAZI. ETI bush AMSAIDIE sadamu sorry osama HIVIHIVI!!

    NI SASA TU WANAMPENDA AKISHIKA MADARAKA WATAMPELEKESHA HADI AHISI JOTO.

     
  • Tarehe: 11:52:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Mtukweli...
    'Mr. President how is Tanzania'
    Jaribu kufikiria kile alichokuwa akikisema mh. JK ktk mfululizo wa ziara zake nje. Nakumbuka ya nchi za scandnavia. 'Tanzania imepiga hatua, tumepunguza vifo vya kina mama kwa asilimia ..., tumepunguza vifo vya watoto wanapozaliwa kwa asilimia..., tumepunguza maambukizi ya maleria kwa asilimia..., ukimwi bado ni janga la kutisha, nchi ilikumbwa na ukame uliyosababisha upungufu wa chakula, ukosefu wa umeme n.k' Maana ya kutamka haya ni kuwa mwisho wa siku unaambiwa chukua hizi 10bill. za ukimwi, hizi 5bill za maleria, si hapo amefanikisha ziara yake?
    Nani unafikiri ataongelea mazuri ya kwetu wakati tunatangaza shida zetu kila kukicha. Hivi bonde la usangu kuzalisha chakula mpaka tukamtafute mtu Canada?
    Ebu wale wataalam wa kuimbisha waniambie ukimtokea binti kwa sifa nyingi na pesa maana yake ni kuwa akuchukuliye hivyo au? kama tumetanguliza shida zetu nje nani akuelezee juu ya mazuri yako ya ndani? Ndugu yangu kweli mazuri yapo juu ya nchi yetu, may be kwenye utalii, ukimaliza utalii unaongelea lipi? Elimu, UD watu wanafurika class mpaka nje, Usafiri, tumekodi Air Malawi, Ferry shida, Barabara Foleni Hiyo kwa Dar, mikoani Rami unaisikia tu, Reli choka mbaya, Chakula hatuna uwakika wa miaka 2, Maji shida, vitu feki kibao, low quality za waindi kibao, Uwezo wa uvumilivu kwa wanasiasa ni 0 kila mmoja anataka kuwa CCM, Uwezo wa wannanchi kutetea haki zao na kuhoji bungeni 0,uchumi upo Dar tu? Huko upcountry hakuna Rais, wanaongozwa na media. Hivi unajua Bongo yetu Familia ya watu 50, akifaulu dogo kwenda sekondary uko bushi kwenye watu 49, kama wewe wa Dar ujatoa mkwanja hakuna shule? tena hela yenyewe elfu 20.
    Hawa wa Magharibi huwenda hawakosei, maana hayo mabovu ndo yanacoverage kubwa, kwani ndugu yangu yakitoweka watabaki kimya si itakuwa heri kwetu?

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker