VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, March 01, 2007
NINI TAFAKURI YA KAULI HII?
RAIS Jakaya Kikwete, amesema matatizo yanayojitokeza katika mikataba mbalimbali ambayo serikali imeingia na wawekezaji, pamoja na mambo mengine, yanasababishwa na uwezo mdogo walionao baadhi ya wataalamu wa Kitanzania wanaoshiriki katika majadiliano ya mikataba hiyo
Huo hapo juu ni utangulizi wa habari iliyoandikwa leo katika gazeti la Tanzania Daima chini ya kichwa cha habari "JK aiangukia Norway".Kama mwandishi wa habari hiyo (mwandishi wa raisi?) amemnukuu vizuri raisi wa jamhuri,basi ni wazi kwamba amekiri na kuanisha mambo mengi sana.

Je ina maana Tanzania imekuwa kila siku inatuma "vihiyo" wakajadili mikataba yenye maslahi mazito ya kitaifa?Je ni kweli kwamba Tanzania haina wataalamu wa kuweza kuuangalia mkataba fulani na kuona mapungufu yake kabla haujasainiwa? Kwanini basi tumvike mtu majukumu mazito kama ya kuamua kuupitisha au kuukataa mkataba fulani kama hatuna imani na uwezo wake?Mtu kama huyu aliajiriwa vipi,alipata vipi cheo alichonacho.Unaweza kuisoma habari nzima kwa kubonyeza hapa.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:30 PM | Permalink |


Maoni: 6


  • Tarehe: 11:53:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Patrick G. Kamera

    Jeff!

    Duh! Hii kali yaani kwa maneno mengine Raisi anadai kuwa wataalam wetu ni "vihiyo"! Hapo katoa matusi ya rejareja.

    Swali, ikiwa huo ndio ukweli basi nani wa kulaumiwa? Unajua mtu ukizoea kuwa ombaomba kila uendako utajikuta unaongea chochote tu upate sababu ya kusaidiwa hata kama ni kujidhalilisha kama alivyofanya hapo.

    Huyu Raisi "mtalii", a.k.a Christopher Columbus a.k.a Vasco da Gama hapo kachemsha, sijui hao wataalam walioitwa "vihiyo" watasemaje? Mfano mdogo tu, wataalam pale Tanesco waliigomea Richmond lakini baada ya amri kutoka juu wakapuuzwa, leo eti wanaambiwa ni mabongolala!

    Sasa kesi kama hizo bila shaka ziko katika sekta zote bongo, wakubwa wana-mind 10% zao, mambo yakiharibika wengine webebeshwe lawama na kuitwa "vihiyo".

    Yaani kaazi kwelikweli!

     
  • Tarehe: 9:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    Patrick,
    Nakubaliana na wewe kabisa kwamba raisi amekosea na kimaadili na uungwana anapaswa kuwaomba radhi wataalamu ambao wamekuwa wakipuuzwa kwa ushauri wao kwa kumezwa na siasa na longolongo zingine.Bado naendelea kuitafakuri kauli ile na sipati majibu bali maswali zaidi na zaidi.

     
  • Tarehe: 6:21:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

    Mwanadiplomasia hatukani bila kukusudia. Jakaya alikuwa waziri wa mambo ya nje - lazima anaijua diplomasia. Lakini kawadharau wataalamu wake kinamna. Kakosea.

    Halafu Tanzania inayo wataalamu makini tu ila pengine hawana uzoefu wa ku-negotiate dili za dizaini hizo. Hata wangeona hitilafu kwenye dili - mwisho wa siku ni wanasiasa ndio wanaozipitisha dili kama hizo.

    Naona Jakaya angeomba msaada wa wanasiasa na mawaziri wa ki-Norwei kuja kuwasaidia watanzania.

     
  • Tarehe: 5:36:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MTANZANIA.

    Jeff,
    Hili suala ni nyeti! Kwa upande moja yawezekana kabisa Raisi ametoa kauli hiyo on the basis "samaki moja akioza basi wote wameoza".

    Ukiangala upande wa pili wa shilingi utagundua tatizo kubwa au chanzo cha haya yote ni RUSHWA. Kama kweli ni vihiyo, Je walivipataje hivyo vyeti vyao vya utaalamu? Je walipitaji kwa milolongo ya interview? Je ni mikataba mingapi wamei-iingiza nchi ktk hasara kubwa? n.k

    Namalizia kwa kutoa mfano wa huyu Mh. wa chama tawala aliyepatikana na hatia ya kugushi vyeti. Baadhi ya magazeti yamemripoti akisema kughushi vyeti sio tatizo maadamu yeye ni mchapakazi makini. Kwa mtaji huu tutafika?

     
  • Tarehe: 12:59:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Patrick G. Kamera

    Ninapenda kuamini ya kwamba wataalam wetu wako makini siyo wababaishaji wala siyo vihiyo ila wanasiasa ndio wanaoharibu mambo, wao wanatanguliza ubinafsi wao na kuwapuuza hawa wataalam wetu. Mfano mwingine, yule katibu mkuu wizara ya nishati si aliikataa ile dili ya IPTL kwani aliona hapa tunauvaa mkenge lakini wote tunajua kilichotokea...

    Kauli kama hizo za Mheshimiwa raisi zitawavunja moyo hawa wataalam.

     
  • Tarehe: 10:34:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger NDABULI

    Sasa hivi swala la Mkataba likija ni deal (Squared) maana jamaa watachukua chao kwa sababu hamana atakaye muuliza si wote mnajua bwana kwamba hawezikunegotiate sasa mtalaumu nini. Yaani jamaa wamefunguliwa njia nyeupee peee fanya utakavyo.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker