"...Mambo ya Bongo sasa hivi kiboko; kuna mashopingi moli kama ya mtoni, maubungo plaza, meifea plaza na maplaza mengine mengi tuuu! Maapatimenti, mariili esteti broka, mabangaloo, mafaivu staa hoteli, na maskai skrepa! halafu mabarabara ya kimtoni na madaraja kama lile la Kibiti, watasha wenyewe wanabloo! Na neshino stediumu mpya ikiisha litakuwa hamna tena Afrika nzima!
Mademu siku hizi wanang'aaaa! Kuna maMiss kata, miss tarafa, miss wilaya, miss mkoa, miss Tanzania, mpaka miss yunivasi! Mafasheni shoo, madizaina, na mamodozi! Siku hizi mademu wanakutilia mavitu ya madizaina: jojo amani, guchi, siyo mitenge ya Sunguratex sijui Urafiki. Jamani Bongo tumetoka mbali, niliwahi kuchukua bonge la demu kufika homu chupi haivuki, mpira wa chupi umekatika akafunga fundo ilibidi alifungue kwa meno! Siku hizi maselebriti kibao: wa vipaji vya kitaaluma, kisanii, kimichezo, kisiasa, ua kwa majina ya ukoo. Kuna Matamasha, mabonanza, na makonseti hatari tupu!
Redio stesheni za kumwaga siyo kama wakati ule idhaa tatu tu; taifa, biashara na eksteno sevisi iliyokuwa inafunguliwa kwa masaa maalumu na kipindi kimoja tu cha salamu siku za Jumapili mchana! Na tivii chaneli kibao siyo kama enzi zile tivii Zanzibar minara michache mitaa ya Upanga na Ostabei tena usalama wa taifa wasiione, ukionekana mnara utakuwa umeenda kinyume na Azimio la Arusha kwa kuwa bepari au kabaila kwa sababu ya kumiliki tivii! Siku nyungo kila nyumba. Mpaka vijijini wana nyungo. Nilikuwa Ng'apa, Lindi huko nikafikiri nitaikosa mechi ya Aseno na Livapuli, mshikaji baa zote zilikuwa zinaonyesha gemu, mashabiki wa ligi ya premia kapu na yuefa wapo mpaka Umachingani huko! Eee bwana na magari mengine yaliyopo Bongo hata ughaibuni hamna: sijui mabaluni, maviieksi, mashangingi, mamuso, mahama, mafoo whili draivu, maleksuzi, yaani wee acha tu!
Elimu nayo sasa imepanda kuna mainteneshino skuli kuanzia nasari mpaka hai skuli. Siku hizi mtoto mdogo anaongea kingreza kama mzungu! Yunivesti siyo UDSM na SUA tu kuna mayunivesti kibao sijui Nyegezi, Sijui Mikocheni, Makumira, Tumaini, na jingine la nguvu linaangushwa Dodoma unaambiwa hilo yunivesti sijui litakuwa linachukuwa wanafunzi ngapi sijui kwa wakati mmoja! Yaani hilo yunivesti litakuwa kama Kembriji, Oksfodi, au Havadi! Eee bwana eee!
Siku hizi simu siyo big dili! Unaambiwa nilikuwa Nanjumbu, Mtwara vijijini ndani ndani huko nikakikuta kibibi kizeeee utafikiri hakikuwahi kuwa kitoto kichanga! Unajua nini? Kilikuwa na kimobiteli cha Nokia hizi ndogo ndogo kinaongea sijui na nani? Mwenyewe nilizimia! Enzi za POSTA NA SIMU ilikuwa lazima uende kibanda cha simu tena ukikikuta simu nzima una bahati vinginevyo sumni yako inaliwa na simu haifanyi kazi. Ua ukitumia simu za nyumbani siyo laini kuingiliana! Au unaweza kujikuta unasikiliza simu tano kwa wakati mmoja! Siku hizi hela yako tu: kuna bazi, seliteli, voda, mobiteli lakini mimi naiona seliteli ndiyo kiboko lakini voda nao moto! Jamaa wa posta kweli walikuwa wanatuzingua barua unaituma Kibaha toka Dar inachukuwa mwezi! Siku hizi unatuma teksi meseji au ukiona namna gani vipi unaenda intaneti unatuma imeli!
Mabenki ya kumwaga hakuna mpango wa kupangapanga foleni tangu asubuhi mpaka jioni. Mahospitali hela yako tu. Kuna mahospitali yana vifaa kupita Muhimbili. Unapigwa eksrei huku unajicheki kwenye skrini, unafanyiwa opresheni bila kupasuliwa, maamblensi mengine mabenzi yana huduma mpaka za kuzalishia!
Usafiri siku hizi siyo sijui ATC, UDA, sijui KAMATA, nyooo! Siku hizi mtu unataka kwenda Mwanza unapaki begi lako unaenda eyapoti unachagua pipa gani udandie Prisisheni, Igo, eyaTanzania au bomba lolote tu! Mabasi siku hizi kuna malakshari yana maeyahostesi kama wa kwenye ndege! Mabasi yana vyoo, tivii, slipingi kochi yaani kama mtoni tu! Prezidenti naye ana pipa lake mwenyewe nasikia lina bafu na jim humo humo!
Bia na fegi za kumwaga. Siku hizi hakuna ulanguzi wa bia wala fegi. Bia unakunywa unayoipenda mwenyewe. Miye bia ninayoipenda kesto (Castle). Bia na Fegi zinakosa maketi mpaka zinafanyiwa advataizment kila mahali. Mzee mzima alitaka kuleta mpango wa kufunga mabaa mapema, kipato cha taifa kikashuka wakamwambia asitishe zoezi lake. Taratibu wakamng'oa asilitie taifa hasara bure!
Unafiki wa kuitana NDUGU imepigwa ribiti! Mzee mzima alipoingia madarakani akaona huu unafikitu. Wewe tangu lini Mchaga na Mpogolo wakawa ndugu? Au mbunge na mesenja au waziri na nesi udugu uko wapi? Lazima tukubali watu wengine ni WAHESHIMIWA na wengine watu tu!
Mimi ughaibuni wala sikuzimii. Jamaa wanaenda ughaibuni nasikia wakifika huko wanabeba maboksi na kukosha vizee. Nanihii alikuwa na bonge la posti akajifanya kwenda ughaibuni kufanya mastazi. Kabla hajaondondoka alikuwa kavimba: mimba hiyoo, mashavu utafikiri anapuliza moto! Hiyo mastazi imemtokea puani: karudi mimba imekatika, kakondaa utafikiri Msudani ya Kusini, miguu kama mikono ya mawani, yaani utamuonea huruma! Unajua Bongo michoro yako tu! Misheni kibao inategemeana na wewe mwenyewe jinsi unavyopanga kete zako. Hapa hapa bongo kuna watu wanakwenda huko ughaibuni kila siku utafikiri andazi na kikombe cha chai! Hapa hapa Bongo kuna majamaa wanaishi kama mtoni: asubuhi wanapata brekifasti ya masoseji, hambagi, juisi na chai ya maziwa matupu au uji uliopikwa na unga wa keki ukatiwa na mapande ya siagi na krimu! Lanchi chikeni chipsi na kuku, dina steki hevi na grili pateto au raisi! Yaani wee acha tu, Bongo New York.
Na manjagu wanakula mavitu hevi siyo kama enzi za Mahita tangu kaja Said Mwema manjagu wanatia vitu vya kimtoni 'maksi' sijui mabelti, mapikipiki, yaani we acha tu! Bongo niu yoki. Cheki mwenyewe hapo chini!
Ofisa na askari wa Jeshi la Polisi wakisimamia bomoabomoa ya vibanda vya wafanyabiashara iliyofanyika jana katika eneo linalozunguka jengo la DDC Kariakoo katika barabara ya Kongo, Dar es Salaam. (Picha na Richard Mwaikenda).
Picha kama hizi tunazihitaji sana maana ni kielelezo cha ukweli unaofichwa na majengo marefu ya kisasa Dasalama na magari ya kifahari. Hawa ndio watanzania wenzetu waliosahaulika. Watanzania tunaopenda kuwasahau.