VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, May 27, 2007
KOMBE LA DUNIA U-20

Kuanzia tarehe 1 Julai mwaka huu mashindano ya kombe la dunia la soka kwa vijana walio na umri chini ya miaka 20 yatakuwa yanafanyika. Mwaka huu mashindano hayo yanafanyikia hapa Canada na Toronto ukiwa ndio mji utakaokuwa na mchezo wa kufungua mashindano na pia kufungia(fainali). Afrika inawakilishwa na timu nne ambazo ni Zambia, Congo, Gambia na Nigeria.Jumla ya timu zinazoshiriki ni 24.

Kwa vyovyote vile mashindano haya hayana ushabiki kama yale ya kombe la dunia la wakubwa yaliyofanyika Ujerumani mwaka jana. Lakini kwa washabiki wa soka hapa Canada hii ni nafasi muhimu na ya kipekee katika kujaribu kuukuza mchezo wa soka ambao hauna umaarufu sana hapa ingawa jumuia ya mataifa ya Ulaya na Amerika ya kusini, walio wanazi wa kutupwa wa soka yamejaa hapa. Kuna jumuia kubwa sana wa wareno,wabrazili,wanigeria,waghana,wamexico,waargentina na watu wa kila aina. Inasemekana ni kwa sababu hakuna anayeweka pesa zake kwenye soka.Tusubiri tuone itakuwaje baada ya mashindano haya na pia David Beckham kuhamia huku ambapo atacheza katika ligi ya Marekani (MLS) ambayo Toronto FC wanashiriki pia. Mchezo wake wa kwanza hapa Marekani ya kaskazini unatarajiwa kuwa hapa Canada timu yake mpya ya Los Angeles Galaxy itakapopambana na Toronto FC.

Bwana mdogo Freddy Adu,mzaliwa wa huko Tema nchini Ghana ambaye sasa ni raia wa Marekani ndio anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa cha mashindano hayo.Yeye ndio kapteni wa timu ya USA.

Pichani juu ni uwanja wa BMO Field uliopo Exhibition Place.Uwanja huu ndio utakaokuwa na mechi ya ufunguzi na fainali.Unauwezo wa kuwaweka vitini mashabiki 20,000.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 8:37 PM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 4:45:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Huko nasikia mambo ni Aisi Hoki tu!Nasikia ndio mchezo unaolipa kuliko yote ukiwa huko kama mchezaji.Je , na wahamiaji wako sambamba na wenyeji katika mchezo huo?

   
 • Tarehe: 8:22:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Jeff Msangi

  Simon,
  Ukweli ni kwamba wahamiaji ni wachache sana katika michezo kama hockey.Sababu zinaeleweka,kwetu sisi soka ndio mchezo.Hii mingine mmmh

   
 • Tarehe: 6:11:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Innocent

  Halo Jeff,
  Sijakusoma siku nyingi,hili soka la vijana sisi wabongo hatuna hata timu za vijana.
  Vilabu vyetu ni sehemu ya majungu tu,na kutafuta kula ya viongozi.
  Naomba Beckam atakapocheza huko kwa mara ya kwanza utujuze huku.

   
 • Tarehe: 12:52:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Jeff Msangi

  Bila shaka Innocent.Nitajitahidi kuwepo uwanjani siku hiyo ili niibuke japo na picha mbili tatu,ikiwezekana nipate naye mahojiano kidogo.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker