VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Friday, May 18, 2007
UKIWAZA KUHUSU UGHAIBUNI UNAPATA TASWIRA GANI?

Nilipokuwa mtoto na hata mwanzoni mwa ujana wangu, nilipokuwa nikisikia kuhusu majiji maarufu duniani kama vile Toronto,New York,Paris,London nk taswira iliyokuwa inanijia kichwani ilikuwa ni majumba marefu yenye gorofa nyingi,bustani za maua zinazovutia sana, wasichana warembo,wavulana watanashati wenye tabasamu zisizoisha kwenye nyuso zao nk. Kwa ujumla nilikuwa nikipata picha ya paradiso ya duniani. Ni kivipi nisipate taswira za namna hiyo wakati maisha ya ughaibuni yalikuwa yakiletwa kwenye mboni za macho yangu na kisha kutuama kwenye ubongo wangu kupitia sinema za Hollywood na vyombo vya habari vya magharibi ambavyo vilikuwa vimeapa (sijui siku hizi) kwamba havitoonyesha kitu kibaya hata kimoja kutoka magharibi?

Kwa bahati nzuri au mbaya, mpaka leo hii, wapo watu wanaoiwazia dunia ya magharibi kwa taswira ile ile niliyokuwa nayo mimi enzi hizo. Siwezi kuwalaumu hata kidogo.Wa magharibi bado wanataka tuamini kwamba kwao mambo ni mswano tu. Kwa makusudi au bahati mbaya wanaficha kila lao lenye doa hata chembe tu.Wanasema Image Is Everything. Lakini kweli???Picha unazoziona ni kutoka mojawapo ya mitaa maarufu hapa jiji Toronto. Ni karibu kabisa na soko maarufu la Kesington. Najua ningesema tuotee hapo ni wapi majibu ambayo ningeyapata yangeweza nikatisha tamaa. Je hii ndio picha ya unayoipata ukijaribu kupiga picha za jiji la Toronto kichwani kwako? Enzi hizo je?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:25 PM | Permalink |


Maoni: 6


  • Tarehe: 4:12:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Pole kwa majukumu ya kimaisha Bw Jeff. Kwa kweli picha tunayokuwa nayo wengi wetu kabla ya kukanyaga huku katika nchi "Zilizoendelea" ni ya kila kitu chema, Kwamba Ulaya, Australia ama Marekani hakuna kibaya. Mawazo haya si ya kweli. Naungana na wewe kuwa hawa jamaa ni hodari sana wa kuficha maovu yao na kuonyesha yaliyo mema tu. Hizi ni propaganda za vyombo vyao vya habari, na nadhani kwa hili wamefanikiwa kutuficha mengi sana. Kadri ninavyozidi kuzungukia nchi hizi, nagundua mambo mengi ambayo ndio hayo hayo wanayaponda katika nchi zinazoendelea. 'Slums' kama za Manzese hata huku Ulaya zipo. Mateja wa dawa za klevya ndio sina hata la kusema, omba omba ndio kabisa! Inatakiwa tubadili mtazamo huu kwa kadri tunavyoweza. Nitatuma picha za huku Ulaya, kuhusu haya ninayoandikaa hivi karibuni.

     
  • Tarehe: 5:51:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Anonymous,
    Asante kwa maoni.Usemayo ni kweli kabisa.Omba omba hapa Toronto wapo wengi sana na wanasumbua kuliko hata wale kina Matonya.

    Tafadhali nitumie hizo picha katika jeffmsangi@sympatico.ca na mimi nitaziweka hewani ili kila mtu aone upande huu mwingine wa nchi "zilizoendelea".

     
  • Tarehe: 4:37:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mzee wa mshitu

    Yess kaka hapa umesema kweli kabisa nami katika kuzunguka haya mataifa ya wenzetu nimegundua kumbe wakati mwingine hata kwetu ni kuzuri kiasi fulani kuliko kwao sema wanatuzidi extent.

    Katika haya majiji yao makubwa kuna masikini kupita kiasi wasio hata na cha kujivunia afadhali Matonya wetu, kuna mambo ya kunuka kama ukahaba, na ushoga wa ngazi ya juu. Big Up nayaona mambo yako.

     
  • Tarehe: 1:51:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Patrick G. Kamera

    Jeff,

    Huu sasa ndio upande wa pili wa ughaibuni ambao kamwe hautauona kwenye CNN. Unajua hata nchi tajiri vipi bado kuna maeneo kama hayo kwenye picha zako.

    Nakumbuka niliwahi kukatiza vichochoro fulani Geneva, Switzerland(kunakohifadhiwa pesa za vigogo wengi duniani) kipindi fulani du kulikuwa kumechoka kinoma, utadhani hauko ile Uswisi tunayoiona kwenye runinga.

    Picha kama hizi zinasaidia kuondoa ile dhana ya kuogopa au kuabudu wazungu. Hapo kusini tu ya Chicago kuna sehemu maji ya kuchota na ndoo na umeme hakuna, ila ukisogea downtown ama wenyewe wanaita Chi-Town kunatisha kwa mi-skyscraper ya nguvu na mabarabara ya kumwaga.

    Ndio hivyo tena, wahenga walisema tembea ujionee usingoje kuambiwa...

     
  • Tarehe: 8:56:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Patrick,
    Usemayo ni kweli kabisa.Ninazo picha za South Chicago na zile za downtown Chicago.Siku moja nitaziweka hapa ili watu waelewe kwa undani unachokiongelea.

     
  • Tarehe: 11:02:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Kuna picha na habari uliwahi kuandika kuhusu Indiana alikotokea Maiko. Nayo ilikuwa ikibeba ujumbe kama huu.
    Mimi naona tatizo kubwa ni tafsiri tuliyoikubali ya maendeleo. Majumba marefu, masoko makubwa yanayoitwa supermarket, majumba ya starehe, vituo na vipindi vya luninga, na mambo kama haya tumeona kuwa ndio vielelezo vikuu vya maendeleo. Tusichokubali ni kuwa vitu hivi huficha msuguano wa kijamii, kifamilia, na kibinafsi ulioko kwenye nchi zenye maendeleo ya vitu. "Maendeleo" ya vitu huficha umasikini wa watu. Masikini wataonekana vipi wakati vyombo vya habari vimejaa habari za watu maarufu (wanamuziki, wanasiasa, wacheza sinema, wafanya biashara, wana michezo, n.k.)?

    Endelea kutuonyesha sura ambayo mfumo wa ubepari huificha.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker