VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, May 21, 2007
UTALII UGHAIBUNI!

Pichani ni landrover niliyoikuta huko Busch Gardens-Africa,Tampa Bay,Florida mwezi wa nne mwaka huu. Ni mwendelezo wa nilichoandika kuhusu utalii na kwanini serikali zetu hazina budi kuvuja soksi.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:20 AM | Permalink |


Maoni: 4


 • Tarehe: 8:29:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger tanzanianboy

  Urewedi Jeff,

  Hongera kwa kazi nzuri.Hili gari lipo ktk kuitangaza TZ kitalii au limeegeshwa tu hapo?

  Naomba rasmi "uanachama" ktk "kijiji" chako.

  Bravo Msangi.

   
 • Tarehe: 6:19:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous


  Waziri Membe atoboa: Kuna warasimu serikalini

  Habari Zinazoshabihiana
  • Membe ziarani Mashariki ya Mbali 12.05.2007 [Soma]
  • Kikwete ateua mawaziri 12.01.2007 [Soma]
  • Samsung kujenga daraja Kigamboni 25.05.2007 [Soma]

  *Asema wanakwamisha sera ya diplomasia ya uchumi
  *Alonga kuwa wanatanguliza maslahi binafsi si Taifa
  *Abainisha vituko vyao alivyovikuta ziarani ughaibuni


  Na Hassan Abbas

  WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe amerejea nchini kutoka ziara ya nje na kuwapasha watendaji warasimu serikalini, aliosema wanakwamisha mafanikio ya sera ya Diplomasia ya Uchumi.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Bw. Membe ambaye alikuwa ziarani Japani, Korea Kusini na Indonesia, alisema kuna fursa nyingi za Tanzania kuendelea, lakini urasimu ambao alikiri upo katika baadhi ya wizara, unaweza kupeperusha azma hiyo.

  "Hili nimeona niliseme kwa manufaa ya Taifa letu. Mimi ni sehemu ya Serikali, lakini nimeona tukumbushane. Ziara niliyoifanya imenipa fursa ya kubaini mambo mengi," alisema.

  Bw. Membe aliyeonekana dhahiri kukerwa na hali hiyo, alisema nchi za Korea, Japani na Indonesia, ziko tayari kusaidia maeneo mbalimbali ya maendeleo nchini hasa katika sekta ya kilimo, lakini zinakerwa na uamuzi wa baadhi ya watendaji wa Serikali.

  "Hili lazima tuambiane ukweli. Kuna haja ya kubadilika ili uwekezaji wenye tija usaidie kuwaletea wananchi maendeleo," alisisitiza.

  Akitolea mfano wa sekta ya kilimo, Bw. Membe alisema alipokuwa Korea na Indonesia, alishuhudia jinsi wakulima walivyojipatia maendeleo makubwa kwa kutumia matrekta madogo, yenye bei nafuu na uwezo mkubwa wa kufanya kazi.

  Alisema mradi wa matrekta kama hayo umekuwa ukishindikana kuletwa nchini, kwa sababu baadhi ya watendaji serikalini, waliwahi kusema Tanzania kuna tope na udongo mgumu, kiasi kwamba matrekta hayo madogo yasingeweza kuwa na ufanisi.

  Aliongeza kuwa wakati matrekta hayo ya bei nafuu na anayoyaamini yana nguvu yakikataliwa, viongozi hao ambao hakuwataja, walikuwa wakiunga mkono kununuliwa matrekta makubwa kutoka nchi za Magharibi ambayo ni ya gharama kubwa.

  "Maelezo hayo (kuwa matrekta madogo hayana nguvu) si ya kweli. Nilipokuwa Indonesia walionekana kushangazwa na kauli hiyo.

  "Tanzania kuna tope gani zaidi ya lile la Bonde la Kuala Lumpa ambako inalimwa michikichi kwa matrekta hayo hayo!," alishangaa Bw. Membe.

  Alisisitiza: "Uongozi bora hasa katika nchi kama zetu ni sawa na mapambano. Kuna haja ya kupambana na urasimu huu ambao upo katika wizara nyingi.

  "Tubadilike kwa kukubali kuwa sasa umefika wakati wa kuangalia zaidi kwa wenzetu wa Mashariki ya Mbali na kukubali teknolojia zao ambazo ni rahisi ili kuwaletea wananchi maendeleo kuliko zile za Magharibi zenye gharama kubwa."

  Waziri Membe pia alitoa mifano kadhaa kuainisha kuwa ipo haja kwa watendaji wa Serikali kuchangamka hasa wakati huu ambapo nchi inatekeleza sera ya Diplomasia ya Uchumi.

  Alitoa mfano wa Serikali ya Korea kuwa katika msimu uliopita ilitumia dola bilioni 300 za Marekani kununua bidhaa mbalimbali kutoka nje kama vile kahawa, pamba, ufuta, chai na korosho, lakini Tanzania iliambulia kuiuzia nchi hiyo bidhaa zenye thamani ya dola 200,000 tu.

  "Hiki tulichopata sisi ni kiasi kidogo ikilinganisha na fedha ambazo Wakorea walizitenga kwa ajili ya ununuzi ya aina mbalimbali. Tunahaja ya kuamka na kuchangamkia biashara kama hizi kabla wengine hawajatuwahi," aliasa.

  Pia Waziri alizungumzia suala la utalii na kusema zipo fursa ambazo Tanzania bado inasuasua kuzitumia.

  Akatoa mfano wa nchi za Japani na Korea pekee, kuwa mwaka jana kulikuwa na takribani watalii milioni 10 ambao walitoka nchi hizo na kwenda sehemu mbalimbali duniani kwa shughuli za kitalii, lakini katika idadi hiyo Tanzania iliambulia watalii 16,000 tu.

  Akatoa changamoto kwa idara za utalii na wizara mbalimbali kuajiri wataalamu wa lugha mbalimbali na kuboresha sekta ya hoteli ili kuvutia watalii zaidi.

  Alipotakiwa kufafanua jinsi uwajibikaji unavyopaswa kuimarika hasa kutokana na changamoto alizoziona, Membe alisema kuna maeneo maalumu yenye kero hizo wataziarifu wizara husika kwa maandishi.

  "Bahati nzuri tuna utamaduni wa kuambiana kwanza na kisha tukaangalia mabadiliko. Hivyo maeneo na kero zinazoelekea kutukwaza tutawaambia wahusika na kuwataka wabadilike. Sisi (Mambo ya Nje) ni wachagizaji tu.

  "Wakishindwa kubadilika zipo hatua ikiwamo kuwafikisha katika hatua za juu zaidi ili kuhakikisha ufanisi unaongezeka," alisisitiza.

  Katika hatua nyingine, Waziri Membe alitoa msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu meli mbili za Korea zilizoandikishwa kufanya kazi Zanzibar ambazo zilitekwa na maharamia nchini Somalia.

  Bw. Membe aliitaka Serikali ya Mpito ya Somalia kusaidia kulimaliza tatizo hilo kwa amani.

  "Niliamua kulitolea ufafanuzi suala hili kwa sababu hata nilipokuwa Korea wenzetu walituomba tulishughulikie suala hili.

  "Lakini pia sisi kama nchi ambayo hivi karibuni tu tuliahidi kusaidia kutoa mafunzo kwa askari 1,000 wa Somalia, hatuoni kama kitendo hicho ni cha kiungwana," alisema Bw. Membe.

  Alisema watekaji nyara hao bado haijabainika wanatoka kundi gani, lakini alisema kwa kuwa Serikali ya Mpito ya Somalia ina uwakilishi wa makundi mbalimbali, basi ina wajibu wa kuhakikisha wafanyakazi wa meli hizo mbili wako salama.

  "Taarifa zetu zinaonesha kuwa bado wako salama na wamewekwa Kusini mwa Somalia wakati watekaji wakidai fedha kutoka Serikali husika.

  "Tusingependa kwa wakati huu kuanza kutoa shinikizo, lakini tunadhani kitendo hicho kinatuogopesha hata sisi ambao tuliahidi kuwapatia mafunzo watu ambao sasa wanaonekana hawana ulinzi na usalama," alisisitiza na kuongeza:

  "Naamini wenzetu watalishughulikia suala hili na tusingependa kwa sasa kutabiri nini kitatokea," alisema.

  Meli hizo mbili ziitwazo Mavuno I na II zilizotengenezwa na kampuni ya Korika ya Korea Kusini zilitekwa nyara Aprili 16 mwaka huu, wakati zikisafiri kutoka Mombasa kwenda Yemeni.

  Katika meli hizo kuna jumla ya raia 24 kutoka China, Korea, Indonesia, India na Vietinamu.

  Imenukuliwa na F M Tungaraza

   
 • Tarehe: 8:53:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Jeff Msangi

  Tanzanian Boy,
  Karibu sana kijijini.Hilo gari limepakiwa katika 'mbuga" ya kutengeneza iliyopo hapo Tampa Bay.Nia sio kuutangaza utalii wa Tanzania bali kuzileta mbuga za wanyama za Tanzania pale Tampa ili pasiwe na haja ya kwenda Tanzania,Kenya au kwingineko.Hapo ndani kuna mto Congo wa kutengeneza,ngorongoro nk.Kwa maneno mafupi wanaua kabisa utalii wa Tanzania.

   
 • Tarehe: 4:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Inasikitisha kuwa ndio sisi wenyewe tunawapa hawa jamaa wanyama. Ndio hawahawa kila siku wanafanya reseach zao kwenye mbuga zetu wakati sisi hizo mbuga hata kuzitembelea tunaona ni kitu cha ajabu hivyo tunawaachia watalii kutoka nchi za nje.Mpaka sasa hivi mara nyingi huwa nakutana na watu kutoka nchi za magharibi ambao wanajua tabia na aina za wanyama Tanzania mpaka mimi mwenyewe napigwa butwaa.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker