VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Monday, June 25, 2007
NITACHELEWA, KUNA FOLENI ILE MBAYA!
Sina budi kuwaomba samahani wasomaji wangu ambao kwa takribani majuma mawili sasa mmekuwa mkitembelea blog hii na kukuta hakuna jipya. Nimewahi kujiuliza hivi siku ukiingia mtaani na ukatafuta gazeti lako la kila siku ulipendalo kisha muuza magazeti akakuambia “samahani sana leo gazeti halikuchapwa” utajisikiaje? Kwa kutambua karaha yake ndio maana sina budi kukuomba msamaha.

Nimekuwa busy na mambo mengine,ningekuwa na uwezo wa kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja wallahi ningefanya hivyo. Basi tu haiwezekani.

Foleni jijini Dar-es-salaam inazidi kuwa kero.Kufika kazini inachukua zaidi ya masaa mawili mpaka matatu. Mwenye gari binafsi na mpanda daladala siku hizi hawana tofauti sana. Sana sana tofauti ni kwamba huyu mwenye gari binafsi anakuwa na nafasi ya kusikiliza redio au muziki anaoupenda tofauti na yule mwenzangu ndani ya daladala ambaye hana budi kusikiliza muziki anaoupenda dereva na konda wake. Kama humpendi Lucky Dube na dereva na konda ndio wanamuona idol wao basi ujue kazi ipo,weka pamba masikioni!

Tatizo la foleni nzito nzito jijini Dar-es-salaam zina sababu mbili kuu.Kwanza ni wingi wa magari. Siku hizi uwiano unakaribia kuwa kila familia mbili zinamiliki gari. Huku ughaibuni kila familia inamiliki gari,huo ndio uwiano. Sababu ya pili ni mipango butu ya njia za usafirishaji kama barabara. Ndio maana majuzi yule jamaa mwenye mvi nyingi akaona aingilie kazi ya mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam na kubuni habari ya njia tatu. Mimi nadhani hii ni kuwakosea binadamu wengine adabu na kukiuka haki zao.Kama naenda opposite direction na traffic hiyo ni bahati na mipangilio yangu.Usinitibue.

Kuna watu wameniandikia barua pepe na kuniuliza, hivi brother Jeff huko uliko hakuna tatizo la foleni? Jibu ni kwamba tatizo hili lipo hata huku. Tena foleni za huku hazina hata ujanja wa kuzikimbia. Ukikamatwa na foleni katikati ya highway ujue zako zimefika.Utapiga mruzi mpaka uchoke. Kama ndio ulikuwa unawahi kuchukua watoto day care ujue kila dakika unayozidisha wenzako wanachaji dola moja!

Lakini wenzetu wanafanya jambo moja kupunguza foleni mabarabarani, kutunza mazingira, kusave hela, kuifanya safari kwenda kazi inoge nk. Wanachokifanya kinaitwa carpooling. Kama mimi na wewe tu majirani, wote tunafanya kazi mitaa ya posta, wote tuna magari, kwanini kila mtu aendeshe gari lake kuelekea kazini? Kwanini tusifanye utaratibu wa kwenda kazini kwa kutumia gari moja? Yaani kwanini kwa mfano mwezi huu tusitumie langu kisha mwezi ujao tukatumia la kwako? Huoni kwamba njiani tutakuwa na muda mzuri tu wa kubadilishana mawazo huku tukisave hela, tukitunza mazingira na kupunguza foleni mabarabarani? Wenzetu wanafanya sana mchezo huo na ndio wanaouita CARPOOLING. Unawasaidia kupunguza foleni na unawapa pia faida zingine nilizozitaja hapo juu.

Ukitaka kuona wenzetu wanafanyaje basi tembelea hizi tovuti carpool.ca autoshare.ca na pia hata zipcar.com. Eti tatizo sisi liko wapi? Hatupendani? Tunaogopana? Au tunahisi kutokwenda kazini ukidrive utaonekana huna mafanikio au kupunguza status? Siamini na ndio maana naamini mzee wa mvi angeweza pia kuanzisha hii harambee.Watanzania ni watu waelewa,mbona timu ya taifa imechangiwa hela kibao hata kama hawajaleta kombe nyumbani? Si wamemfunga mmagharibi tu?

Kama unataka kujua kiasi cha fedha utakachoweza kusave wewe na jirani zako mkianza mchezo huu bonyeza hapa.

Picha kwa niaba ya Michuzi.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:52 PM | Permalink |


Maoni: 3


  • Tarehe: 10:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Na wewe ni walewale?
    Zamani waliitwa "wabenzi" siku hizi naona ni "washangingi" maana unasema unachelewa huku sioni kipanya chochote kwenye hiyo foleni?
    Wao hawajui bei ya petroli ila sisi wanatupandishia kwa makusudi na kutuambia tujifunge mikanda.
    Angalia. Motowaka bado yupo.

     
  • Tarehe: 8:42:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    car pooling ni nzuri. Lakini lazima tupunguze idadi ya magari barabarani mjini. Kwa mfano, ulijua kuwa watumishi wa serikali hawalipi kodi wakiomba gari kutoka nje, Soma tovuti wa tra tra.go.tz

    Pia, inabidi tuboreshe public transport

     
  • Tarehe: 12:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger kifimbocheza

    Samahani, nimerudi tena. Kwa kweli, foleni mjini ni changamoto kubwa kwa madereva kama mimi.

    Lakini kwa abiria wa daladala, ni ngumu mno. Ukitegemea daladala hapa Dar es Salaam, usishangae kusubiri muda wa saa moja au zaidi kupata usafiri. Sisi madereva tumebarikiwa kwa kweli. Tukichelewa husikiliza redio tu. Lakini wenzetu huvumulia kujaa ndani ya daladala kama dagaa ndani ya gunia.

    Tukifikiria suala la foleni mjini, tusisahau ndugu zetu.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker