
Kama kuna mwanamapinduzi hadithi ya maisha yake ina mvuto wa aina yake na pengine wa kipekee kabisa,mwanamapinduzi huyo lazima awe ni Ernesto Guevara de la Serna ambaye wengi tumekuja kumsoma au kumtambua kama Che Guevara. Mzaliwa wa Argentina ambaye ukombozi wa dunia na upinzani wa dhati dhidi ya ubepari, ulikuja kuwa ilani yake ya msingi alikuwa na ujasiri (lakini pia katili) wa aina ya pekee kabisa.Nini kilikuwa kinamsukuma Che-Guevara mpaka akaingia hata misitu ya Congo na kisha Bolivia ambako mauti hatimaye ilimfika? Kama ni uanamapinduzi(leo hii angeitwa gaidi namba moja,au?) yeye aliionaje dunia?
Pengine na wewe hujui ni kwanini mpaka hivi leo watu wengi wapinga udhalimu,hususani wa kibepari, bado wanaranda mitaani wakiwa wamevalia t-shirts zenye picha ya sura yake(hiyo hapo juu), skafu,vijarida,vipeperushi nk? Ukitazama documentary hii hapa chini pengine unaweza ukaelewa kwanini. Documentary ni ya kama lisaa limoja na nusu hivi lakini nakuhahakikishia,inafaa kutizamwa.Fuata link hii hapo chini.
THE TRUE STORY OF CHE-GUEVARA(2007)
Huyu jamaa kweli amngekua anafanya hivi kipindi hiki , angeitwa terrorist. Pia angeweza kushtakiwa kama muuaji katika nchi fulani au hata katika Mahakama za kimataifa.