VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, July 03, 2007
KWAHERI AMINA!


Sikuwa kimya kwa sababu mbaya.Nilikuwa natafakari niseme nini. Msiba wa mbunge kijana Amina Chifupa uliniacha nisijue la kufanya wala kusema. Nilishtushwa kama mlivyoshtushwa watanzania wenzangu. Najua kuna ambao hawakushtuka.Hawa waliuona msiba ukikaribia kwa kuangalia jinsi gani ambavyo historia ya nchi yetu imekuwa tangu enzi na enzi. Kwanini unafunga macho sasa?Kwani wewe hujui kwamba Tanzania hutakiwi kuwasemea walio juu? Kwani hujawahi kuona uozo mbalimbali ukifumbiwa macho kwa sababu waliouona wanaogopa kupoteza maisha yao? Au unataka kujifanya hujui yaliyowahi kutokea siku za nyuma? Acha bwana wewe!

Yawezekana kabisa kifo cha Amina kikawa ni mipango ya mungu. Kinachotia hofu na hivyo kuhalalisha gumzo ni mazingira ya kifo chake. Akasema atawataja hadharani wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya. Magazeti uchwara yakaandika vichwa vya habari na wala yasimuunge mkono wala kuchimba kwa undani.Wakapewa lead lakini wakagwaya.Halafu unataka kunifunga mdomo,Thubutu! Kilichofuata mumewe (ambaye kila afunguaye mdomo anasema yeye pia ni “zungu la unga”) akamtaliki! Sababu aliyoitoa; ugoni! Amina akashindwa kutokea mbele ya waandishi wa habari kama alivyokuwa afanye.Baba mtu akatokea badala yake bila majina ya wazungu wa unga.Akawapa story waheshimiwa waandishi na wao wakakubali. Historia ya Amina ikawa ndio imefikia kikomo.Mauti yakamfika siku ya kuadhimisha vita dhidi ya matumizi ya kulevya!

Kuna vitu vinavyoitwa na wenzetu conspiracy theories.Sijawahi katika siku za hivi karibuni kukutana na nzito zaidi ya hii.Eti nini? Kafariki kwa ugonjwa wa kisukari? Eti alipata ukichaa? Eti malaria? Ipi kati ya hizi sababu inakuingia akilini? Unajua serikali imesema nini? Itafanya uchunguzi wa kifo chake kama itaombwa! Mazingira gani inahitaji? Anewei, ngoja niachie hapa au unataka niseme nini tena?

Kama wewe una anuani ya barua pepe inawezekana kabisa uliupata waraka ulioweka hadharani mambo ya BoT..hujakosea ni ile Benki Kuu ya Nchi! Bila shaka pia ulipata nafasi ya kusoma skandali nzima ya jinsi mihela inavyoliwa na wanaojiita wajanja,wengi wao sio hata raia wa Tanzania. Wabunge wa upinzani ambao ni wachache sana wakaiweka ishu hadharani.Wale wa chama tawala walikuwa wameipata barua pepe lakini wasithubutu kusema. Ngoma ikaenda mheshimiwa mwenye mvi akasema serikali inachunguza. Hapo ndipo niliporuka toka kwenye kiti,almanusura nivunje mguu.Utachunguza vipi wakati watuhumiwa wakuu tukianza na gavana Balali bado wapo ndani ya nyumba? Hivi inaingia akilini kweli? Kwanini katiba ya nchi au aliyemchagua gavana asimwambie mzee kaa kushoto kwanza mpaka uchunguzi uishe? Nani anasoma maandiko haya? Kama hujaisoma dossier ninayoiongelea hapa niandikie e-mail nami nitakutumia.Nchi hii ikoje lakini?

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 11:59 AM | Permalink |


Maoni: 6


  • Tarehe: 12:59:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff,

    Mambo yenyewe ndiyo kama haya hapa chini:

    Government shuns debate on Mkapa

    2007-07-04 09:22:47
    By Lusekelo Philemon, Dodoma

    The government has insisted that it will never work on media reports over allegations leveled against former President Benjamin Mkapa on his involvement in private business while working at the State House.

    The government position was stated yesterday by the Minister of State in the President`s Office (Good Governance), Philip Marmo, when debating budget estimates of the Public Service Management.

    Responding to requests of the opposition that the government comments on the scandal, Marmo said the government would never work on newspapers reports.

    `We will not work on newspapers reports. If there is any one who wants to find the truth of the matter, the procedures are there. The stand of the government is that we will not at any time get involved in such kind of debate. The existing rules and regulations are adequate,` he said.

    `The law provides proper channels for any one who is not satisfied with the trend of any leader in this country. Anyone can use those channels by paying only 1,000/- to the ethics tribunal.` Marmo said.

    He further explained that the government had circulated about 6, 415 forms to be filled by top government officials to show the property they owned and where and how they got it.

    Marmo said there were about 3, 317 government officials who had returned their filled in forms.

    * SOURCE: Guardian

     
  • Tarehe: 1:48:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

    MtiMkubwa,
    Asante kwa taarifa hii.Hii inaonyesha jinsi gani tunayo serikali..

     
  • Tarehe: 2:13:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Innocent Kasyate

    Kaka Jeff,
    naomba unitumie hiyo dosier tafadhali sijaiona.
    Hili la Chifupa nimeandika kwangu kama una muda pitia kwangu alafu utoe maoni kidogo.
    Hivi kuna haja gani ya mtu makini kuwa mbunge?Yaani tusiseme vitu viovu, hivi tutafika kweli?
    Kaka nakutakia sikukuu njema ya Africa huko Kanada, tuwakilishe mzee.

     
  • Tarehe: 10:58:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Pius Ntwale

    Kaka Jeff,
    Nami ninaiomba hiyo habari kuhusu kashfa ya BOT,hivi kuna nchi kama yetu duniani?kinacho niuzi zaidi, mambo haya yakiendelea wenye nchi tunaangalia tu.Tunasema mchana, usiku tunalala, tukiamka tumesahau.Yatupasa tubadilike ili tulete mabadiliko.

     
  • Tarehe: 2:21:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Innocent na Pius,
    Nitawatumia hiyo dossier muione.

     
  • Tarehe: 11:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Jeff,
    Hii ndiyo Tanzania yenye rasilimali lukuki.

    Sijui, lakini labda tungetakiwa tufanye mapinduzi haraka sana kabla hizi rasilimali hazijaishia nje au kwa MANYANG'AU wachache. Ndiyo ni manyang'au, watu gani wasiyo na huruma na binadamu wenzao?

    Sisemi wagawe fedha kwa kila mtu, la hasha, wajitahidi kuwahamasisha na kuwaelekeza jinsi ya kutumia fursa zilizopo karibu nao jinsi ya kuzalisha kipato.

    Huwa napenda sana kuzungumzia huyu mwananchi wa chini kabisa mwanakijiji.

    Tuna mabwana mifugo na mabibi mifugo, wapo mabwan ashamba na mabibi shamba.

    Hawa walipwe vizuri waweze kwenda vijijini kuwaelimisha wananchi jisi ya kujenga mabanda bora ya kuku wa asili pamoja na ukulima wa faida kama mboga mboga nk.

    Jeff, hapa tanzania ni nadra sana kama una hekari moja uweze kupata gunia 15 za mahindi. hata hivyo ukijikakamua kutumia mbolea ukapata hizo gunia 15, bei yake haizidi shs 14,000.00 kwa gunia(14,000 x 15 = 210,000.00 kama una ekari 4 ni shs 840,000.00 hizi ni fedha gani kwa mwaka, ukikata matumizi kitabaki kitu gani!!!!!!!!

    Lakini mkulima wa vitunguu au nyanya pale ilula, ekari moja anaweza kupata zaidi ya shs 5,000,000.00 kwa msimu.

    Ni hawa viongozi wanapaswa kuweka miundombinu kwa raiya wake ili waweze kutekeleza majukumu na kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao.

    Ufugaji wa kuku wa asili nadhani wakielimishwa hawa wanaweza kujikwamua kwa kiwango kikubwa sana.

    Jeff, mikakati ninayo na ninaanda miundo mbinu kwa ajili ya kuelimisha wanakijiji wangi kwa ujumla wao. Mimi siyo tajiri lakini najisikia furaha na faraja nikiweza kutoa mawazo yangu na kuwafaidisha watanzania wenzangu.

    Kuna jambo moja nilifanya mwaka 2005 mwamnzoni, ile ni alama. Na bado, elimu yangu ni ndogo lakini nitahakikisha nawabadili wanakijiji wenzangu wote hasa wale wenye vipande vidogo vya ardhi ili wazalishe kipato kikubwa kuliko ilivyo hivi sasa katika kipande hicho hicho. Mfano wataona kwangu, sasa ninapoandika huu ujumbe, katika familia yangu tayari nuru imekwisha onekana.

    Mmmoja kaniandikia ujumbe na kusema, nanukuu

    "....nasikia arufu ya fedha nyingi sana, sasa mimi ni tajiri"
    mwisho wa kunukuu

    Huyu yeye anataka kutumia ekari moja na nusu. Utafiti amekwisha fanya na baadhi ya miundo mbinu imekwisha kamilika, anatarajia kupata zaidi ya shs 3,500,000.00 kwa mtaji usiyozidi shs 300,000.00 kwa mwaka.

    Tukumbushane, Feb 2008 panapo uzima, nitatoa maendeleo ya mradi.

    nadhani viongozi wetu wanapaswa kufanya haya, wasiwe wachoyo na tamaa ya kujipendelea wao tu.

    Billion moja ingeweza kuwa chuo kizuri sana kwa zaidi ya vijiji vitano kila mkoa.nimesema CHUO, NADHANI HAPA NIMEELEWEKA.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker