VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, July 10, 2007
MAHOJIANO YANGU NA GLOBAL VOICES!


Hivi karibuni jamaa wa Global Voices walinifanyia usaili.Usaili wenyewe haukuwa wa kuomba kazi ingawa natamani siku moja usaili wa namna hiyo uniangukie.Tamaa inatokana na ukweli kwamba jamaa wanafanya kazi waliyotumwa waifanye.Wanajaribu kwa nguvu zote kubadili jinsi dunia inavyopashana habari na kufanya mambo.Ubabaishaji unakuwa sio biashara yao kama ambavyo serikali fulani za kule kwetu zinavyofanya.

Kwani hujasikia bado kwamba kumeibuka waandishi, waliokabidhiwa madaraka kwenye gazeti la chama cha njano na kijani wanaodai eti gaveneta kapigwa "jungu" tu na manazi wanaotaka waingize mtu wao kwenye boti? Usishangae, waandishi wa namna hii bado wapo.Tena hao ndio kila kukicha wanaikwea ile ndege iliyokunyima na ambayo bado inakunyima huduma bora za afya na elimu ya wanao, wakipuyanga na aliye juu kidogo(aliye juu kabisa ni Mungu tu) huku na kule.Yaani anachotaka kusema mwandishi yule ni kwamba hao watu ni kabambe kushinda kawaida kwani sio tu wamefanikiwa kumpiga jungu gaveneta bali pia wana uwezo wa kumchagulia hata Mr.Handsome gaveneta wanayemtaka wao!Haya si ni matusi jamani? Lakini hebu cheki,andiko kama hilo likachapishwa na katibu muhtasi akaambiwa na bosi alinunue kisha aliweke kwenye briefcase ili mzee atakapokuwa anakoroma kwa usingizi jioni pale kwenye kochi lake liwe pembeni.Utafikiri atalisoma vile.Wangekuwa wanasoma yanayoandikwa si tungesha peleka mwezi kigamboni?


Lakini usikate tamaa! Tupo tunakuja,tunajiunda tu taratibu.Kwani miaka miwili iliyopita ulijua kwamba kutakuwa na viwanja viitwavyo blogs ambako watu wanasemasema angalau?Kwani wewe hujui kwamba siku hizi hata sisi tunaweza kufanya kama alivyofanya mwanamapinduzi Walter Rodney katika The Groundings with my brothers? Tunachotakiwa ni kujua tunakokwenda ili tukipotea tuseme tumepotea! Sasa unashangaa nini tena ndugu yangu? Kwani wewe hujui kwamba ukiwa hujui unakokwenda huwezi kusema umepotea? Au ndio maana maneno kama "samahani,tumekosea" hayajawahi kutoka miongoni mwa waheshimiwa wetu?

Ni hayo tu kwa sasa hivi.Pichani ni mimi.Nimeona niweke hiyo hiyo picha waliyoitumia Global Voices.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:07 PM | Permalink |


Maoni: 2


  • Tarehe: 11:49:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Majadiliano yako na Tungaraza nimeyapenda sana. Umegusia mambo ya msingi na kuonyesha kuwa chombo hiki, ingawa kutakuwa na watu watakaokitumia kuandika habari za jinsi walivyoamka, walivyokwenda madukani kununua nguo mpya, bado watakuwepo wengine watakaokitumia kama silaha ya kuleta maendeleo, kupanua wigo wa majadiliano, kuelimishana na kupeana habari. Asanteni maana mmetia mwanga blogu zetu za Kiswahili.

     
  • Tarehe: 7:38:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    majadiliano yalikuwa mafupi ila yamebeba ujumbe wote.bwana ndesanjo unaonekana kukerwa na waandishi wanaoandika maswala yao binafsi wakemee kwa kuwataja kama ilivyokuwa kwa pichazenu huyu sasa amechoka na michezo yake michafu.tuwe na utaratibu wa kukumbushana hata tunapokuwa wavivu na tunapoenda kinyume na maadili ya uandishi binafsi

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker