VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Saturday, August 18, 2007
KUJITOLEA

Mojawapo ya tofauti kubwa za kijamii miongoni wa waafrika au watanzania tulio wengi ukilinganisha na wenzetu wa magharibi ni kwamba sisi hatupendi kujitolea. Kwetu sisi kujitolea ni lugha tusiyoielewa sana. Hatuamini katika kazi bila malipo.Tukiona kikundi cha wanafunzi wa kutoka magharibi nchini kwetu wakiwa wamekuja kujitolea kujenga shule iliyopo kijijini kwetu,tunaona kama wanadanganya,lazima wanalipwa hawa!

Hulka hii imetapakaa sana miongoni mwetu,imekuwa kama utamaduni.Bila malipo au faida fulani hakuna kinachofanyika. Viongozi wetu hawafanyi lolote bila malipo au faida. Usishangae basi kusikia kabla ya kuanza shughuli zozote masilahi binafsi ndio hujadiliwa kwanza. Ukiwaambia viongozi wetu wajitolee nusu tu ya mshahara wao wa mwezi ili kusaidia yatima,wasiojiweza na wagonjwa wa ukimwi usishangae ukageuka kuwa adui yao namba moja. Ndio maana mara nyingi nimeshaulizwa na ndugu,jamaa na marafiki kuhusu faida za kublog. Jibu langu huwa ni rahisi,naandika kwa kujitolea ili kusaidia kuelimisha,kupasha habari,kubadilishana mawazo na wanajamii wenzangu.

Kisingizio kikubwa ambacho wengi tumekuwa tukitoa ni kwamba tuko busy sana,hatuna muda. Visingizio kama hivi mimi huviona vya kinafiki kwa sababu mbona muda wa kukaa baa tunaupata? Mbona muda wa mnadani haukosekani? Mbona muda wa kumtembelea jirani na kupiga soga la umbeya upo? Ni kweli hatuna muda au hatujajijengea utamaduni wa kujitolea?

Lakini pia lipo kundi la watu ambao wanasema,wanapenda kujitolea lakini hawajui ni jinsi gani wanaweza kufanya hivyo. Habari nzuri ni kwamba kutokana na maendeleo ya kitekinolojia, sasa unaweza kujitolea bila hata kutoka ndani ya nyumba yako. Kwa kiingereza wanasema “you can be a virtual volunteer”. Tovuti kama www.onlinevolunteering.org ndio jibu kwa watu wa aina hii. Hapa Canada www.volunteer.ca ndio suluhisho. Tanzania pia tunaweza kuanzisha kitu kama hiki.Tunaweza kuanzisha utamaduni wa kujitolea. Kutoa au kujitolea sio utajiri, ni utashi tu. Tukisubiri mpaka mzungu aje kutoka magharibi ndio tuzibe mtaro uliopo mtaani unaozalisha mbu na hivyo malaria, tutakuwa tunajichimbia kaburi bila kujua. Umewahi kujitolea? Ilikuwa vipi? Bado unajitolea? Sote tungependa kusikia kuhusu uzoefu wako.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:34 PM | Permalink |


Maoni: 2


 • Tarehe: 2:33:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

  Kujitolea ni jambo jema sana, Zitto Kabwe alijitolea kusaidia wazalendo wasiendelee kuibiwawakaamua kumnyamazishalakini moyo wa mwanamapinduzi hauwezikunyamazishwa kirahisi hivyo.
  Tunatakiwa kujitolea kwa vitu vingi tuu,damu, kuhudumia wasiojiweza,kuhudumia jamii, lakini tatizo ni paleninapojitolea na mwingine anapokea malipokwa kudanganyakwamba kujitolea kwangu kulilipwa.
  Ndiyo, jamii ya vijijini haina watoa huduma wa kujitosheleza, wanahitaji walimu, wahudumu waafya, Usafiri, nawataalamu wa kilimo pia kwa uchache. Lakini tatizo ni lile lile tunakatishwa tamaa na mfumo uliopo tunaishia kuwatumikia wale waliojitosheleza na huduma hizo na wasio wenzetu, sijui kama hawa matapeli wa kishairi kama wanajua matendo yao yanaumiza wengi wasionauwezo na vilevile wanadumaza jamii yetuili mbele ishindwe kushindana na wengine.

   
 • Tarehe: 4:29:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Jeff Msangi

  Mloyi,
  Nakusikia ndugu yangu.Naelewa kabisa unachokisema,uchungu ulionao nauhisi.Kukatishwa tamaa ni kero ya aina yake.Kwa bahati mbaya jamii yetu ndio tumeijenga hivyo,kiakili na hata katika hali halisi.Hiyo ni minyororo ambayo lazima tuikate.Nakuomba usikate au kukubali kukatishwa tamaa.Tufanye,tutasikika tu,tutasaidia wengi.Viongozi ndio hao ambao hata kusema itabidi tulipie hivi karibuni.

  Cha msingi,lets volunteer,let us help each other.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker