VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Friday, August 24, 2007
WAANDAMANAJI MAMLUKI!
Kwa jinsi ambavyo bara la Afrika kila siku linakuwa mstari wa mbele katika purukushani za kisiasa na jinsi ambavyo mashirika mengi makubwa ya habari ya kimagharibi kila kukicha yamesheheni habari mbofumbofu kutoka barani Afrika, kuna wakati mtu unaweza ukadhani huku magharibi mambo ni shwari tu! Angalau kidogo,habari za Marekani kupoteza heshima na hadhi iliyowahi kujijengea (kwa wasiofuatilia historia ya dunia lakini) zenyewe zimetapakaa kila mahali. Kama bado unaiona Marekani kama pepo iliyopo duniani basi tovuti kama ya Information Clearing House inaweza kuwa yenye msaada.

Lakini kunako nchi zingine kwa mfano hii ninayoishi mimi ya Canada, habari zake ni kama hazipo.Zipo mitandaoni, kwenye magazeti na redio za mitandaoni lakini ni kama vile hazipo. Hazivumi.Subiri.Hivi karibuni ipo habari moja ambayo imevuma. Ilikuwa hivi; hivi karibuni Raisi wa Marekani, George Walker Bush, Waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper na raisi wa Mexico Felipe Calderon walikutana katika mji wa Montebello uliopo katika jimbo la Quebec (jimbo kubwa kupita yote Canada na ambalo wakazi wake wanaongea kifaransa zaidi). Mkutano ulikuwa unahusu masuala ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizi tatu ujulikanao kama NAFTA.

Kama ambavyo ungetegemea, waandamanaji kibao wakajitokeza kumzodoa zaidi raisi Bush kwa sera zake mbalimbali za kimataifa ambazo kadri siku zinavyokwenda zinazidi kuifanya dunia kuwa hatari zaidi. Siku hizi ukiiingia kwenye treni ya chini, kwenye basi la abiria au kuhudhuria mahali penye mkusanyiko wa watu wengi, kila mtu hamwamini mwenzake! Huu ndio usalama anaouongelea Bush. Dunia ya leo ukisikia watu zaidi ya 300 wameuawa katika mlipuko uliotokea baada ya mtu mmoja wa kujitoa mhanga kujilipua, hushtuki wala kusononeka sana.Imeshakuwa kawaida!


Sasa ili maandamo ya kumpinga Bush yaonekane kama yalikuwa yanafanywa na kundi fulani tu la wahuni, polisi wa Canada wakapandikiza waandamanaji (mamluki) ili wawafanyie fujo polisi,mabomu ya machozi yapigwe, watawanyike mkutano uendelee bila makelele.Baadaye polisi wamekiri taarifa hii bali wakajitetea kwamba walikuwepo ili kulinda usalama.Tatizo likaja kwamba polisi hao walikuwa wameshika mawe wakati maandamano yalikuwa ya amani na sio vita!

Kwa bahati nzuri au mbaya,waandamanaji wakawashtukia mamluki hao ambao walikuwa wamefunika nyuso zao ili wasitambulike.Kizazaa kikaanza,wakatakiwa watoe vitambaa walivyojifunga, waondoke kwenye maandamano. Kasheshe likaendelea kidogo na polisi (wenzao) wakajitokeza kujidai kuwashika na kisha kuwaondoa (bila kuwatoa vitambaa walivyojifunga kwenye nyuso). Kitendo hicho ndio ilikuwa hakikisho la kwanza kwamba waliojifunga nyuso ni polisi pia. Lakini pia wakati wa kuwakamata, walipojidai kuwadondosha chini soli za viatu vyao zikawaumbua.Zikaonekana kuwa sawa sawa. Swali moja kubwa ni hivi kwanini watawala hupenda kufanya watu watawaliwa wajinga? Kwanini watawala hupenda kuwafunga midomo watawaliwa? Tizama picha na video zilizopo kwenye habari hii.

Picha iliyowaumbua polisi.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:05 PM | Permalink |


Maoni: 2


 • Tarehe: 1:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mwandani

  Hawa jamaa wanaweza kufanya unyama kwa remote control huku wamevaa suti na tai, hata usiweze kufikiri kwamba nao wanatumia mbinu mbaya ku-discredit mawazo mbadala.

  Hapo hapo kwenye info-clearing house kulikuwa na filamu ya wakati wa maandamano ya wafanyakazi LA. Walipewa kipigo waandamanaji, wengine wakabururwa... lakini ndiyo hivyo - kwa kuwa wao ni "demokrasia nzuri" kuliko kwengine, yao huwa hayasemwi kwenye fox.

   
 • Tarehe: 1:47:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Patrick GK

  Hiyo ni kweli, ila najiuliza hivi kuandamana huwa kunasaidia chochote kweli? Kama viongozi wameamua walivyoamua sidhani kama kuandamana kutawafanya waamue tofauti.

  Mnakumbuka kule Amerika ya Kusini Bush alipokwenda kwenye mkutano na marais wenzake shughuli yake ilivyokuwa nzito kwa waandamanaji? Mimi naona dawa ya kuwaadibisha viongozi ni kisanduku cha kura tu, mtu anaondolewa kiulaini(kama kura hazitaibiwa!Duh kaazi kwelikweli!)

  Mwandani,
  Ndio uzuri wa blogu, vitu vinapaishwa "live", hakuna kufungana kamba wala nini.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker