VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, October 04, 2007
UNA FURAHA?

Maisha bila furaha si maisha. Katika nchi zilizoendelea watu wengi sana hawana furaha wala raha ya maisha yao ukilinganisha na wale waliopo katika nchi zinazoendelea. Ndio maana inasemekana taifa lililo na furaha kupita yote duniani ni Nigeria ikifuatiwa na Mexico, Venezuela (hawa nasikia ndio wenye wanawake warembo kupita wote duniani) na El Salvador. Najua kama ulikuwa hujui hili unashangaa kwani ulidhani taifa hilo pengine lingekuwa ni Canada, Marekani au Uingereza. Maisha ya ughaibuni yamejaa presha. Ingia ndani ya gari lako au ndani ya basi kama sio treni saa za asubuhi kisha utizame sura ya jirani yako ndani ya basi au kwenye mataa uone kama anaonekana kuwa na furaha yoyote ya maisha. Utashangaa.

Watu wengi wanafanya kazi ambazo hawazipendi.Wamo kwenye mahusiano ambayo hayakidhi haja zao wala achilia mbali kukaribia japo robo ya ndoto zao. Msongo wa maisha umewajaa mpaka utosini. Idadi ya watu wanaojiua ni kubwa katika nchi zilizoendelea kuliko zinazoendelea au hata zile zilizogoma kuendelea!

Yawezekana wewe msomaji wangu huna furaha au tuseme raha ya maisha yako.Unaperuzi mtandaoni hivi leo ili tu kupunguza msongo wa maisha. Sasa ufanyeje ili kuwa na furaha au kufurahia maisha? Hebu jaribu kufanya yafuatayo;

 • Fanya mazoezi angalau kwa nusu saa tu mara tatu kwa wiki.
 • Hesabu Baraka zako. Siku inapofikia ukingoni jaribu kujiuliza ni mangapi ambayo wewe umebarikiwa kuwa nayo ambayo wengi hawana.

 • Tafuta muda wa maongezi- Jitahidi kupata muda wa kuketi chini na rafiki yako wa karibu au mpenzi wako mkaongea kwa uhuru na kinagaubaga.

 • Panda mti au ua na kisha lipalilie.

 • Tabasamu kwa mgeni utakayekutana naye leo.

 • Cheka-cheka kwa nguvu zako zote kila upatapo fursa.

 • Tenda jambo moja jema kwa siku.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:23 PM | Permalink |


Maoni: 8


 • Tarehe: 8:42:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Jeff hapa sina chakuongezea wala kupunguza!Posti timilifu kabisaa hii!Tuko pamoja!

   
 • Tarehe: 10:15:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Samahani, natoka nje ya somo!

  Njoo tumalizie kujadili kipengele, ili tuende kwenye hatua nyingine ya kuboresha wanajumuiya wa jumuiya ya Watanzania wanao tembelea au wanao blogi.

  Tembelea hapa : http://blogutanzania.blogspot.com/
  ilia tumalize kujazia dondoo ili tu anze na kipengele kingine.
  Idumu JUMUWATA!

   
 • Tarehe: 10:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Ukiacha Venezuela, sio kweli kwamba nchi hizo zina wanawake wazuri. Mexica na Nigeria zina mianamake mibaya hujawahi kuona. Msiwe mnaokota tu maneno mitaani kuja kuweka kwenye blogs jamani. Write something with substance!

   
 • Tarehe: 3:47:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff

  Anonymous,
  Wakati mwingine sio vibaya kama utaisoma habari na kuielewa kwanza.Kilichoongelewa hapo kwenye uzuri ni Venezuela tu. Hizo nchi zingine zimetajwa kama nchi zenye watu wenye furaha kupita wote duniani na sio wazuri kupita wote.Asante kwa kunitembelea.

   
 • Tarehe: 11:15:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Ni kazi ya mwandishi kuhakikisha kwamba anachooandika kinawafikia walengo bila utata. Umetaja nchi kisha ukaweka mabano na kesema kwamba (hawa inasemekana ......). Ilionekana kama hawa inawakilisha raia wa nchi ulizozitaja kabla ya mabano. Labda ungetumia umoja k.m nchi hii au ungetaja moja kwa moja kwamba Venezuela inasemekana..... isingeleta kutokueleweka.
  Hata hivyo sasa nimekuelewa zaidi.

   
 • Tarehe: 5:54:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Anonymous,naona peke yako ndio hukuelewa.Haishangazi basi na wewe umeandika "kesema". Jeff,endelea kutupa vitu bwana.Hiyo link ya statistics nimeipenda sana.Keep it up mwanangu.

   
 • Tarehe: 12:58:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Miriam

  Hayo mabano yangekuwa baada ya sentence kuisha; Mwandishi angemaanisha nchi zote. Lakini kwa sababu mabano yamewekwa baada ya nchi moja(Venezuela); Inamaanisha kuwa mwandishi anaongeza point kuhusu hiyo nchi, ambayo ni Venezuela peke yake. Mtu aliyejifunza kuandika ataelewa kuwa Venezuela ina wanawake wazuri na sio Nigeria, au Mexico.

  Kama mwanamke naamini kuwa kila nchi ina wanawake wazuri kufuatana na mila na desturi za nchi hiyo. Kama mtu anapendelea wanawake "blond" atasema Sweden kuna wanawake wazuri duniani. Kama mtu anapendelea wakina mama wanene kidogo na pia wanaafya, atasema Africa ndiyo inawanawake wazuri. Kama mtu anapendelea wanawake wenye ngozi inayojulikana kama "yellow" au pia waliochanganyika (Mix race, )basi watasema Venezuela au Hispanic ndiyo wazuri. Uzuri ni macho ya mtu. Enzi za watumwa, watu weupe tu ndiyo waliojulikana kama wazuri. Ukiniuliza mimi kama mwanamke wa Kitanzania, nitasema wanawake wazuri wako Tanzania.

  Lakini kusema ukweli, nina unga mkono mwandishi ukifatilia nchi kama Canada na USA, wanaamini kuwa Wanawake wa KiVenezuela in
  wazuri duniani.

   
 • Tarehe: 5:05:00 PM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Mwalimu wangu hapa Sweden aliniambia nchi inayoongoza duniani kuwa na watu wenye furaha ni Tanzania, lakini sikumuuliza source..alizungumzia darasani.
  Maelezo yako ni ya kweli, huku ni nadra sana kucheka jamani.
  Kazi njema kaka.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker