Ingawa hatujaonana hapa kijiweni kwa muda kiasi,natumaini kwamba hujambo na Mungu amekujalia kuuona mwaka huu wa 2009 ukiwa mwenye siha njema kabisa.Nikutake radhi kwa kunikosa kwa muda mrefu.Mipangilio ya kiutendaji,majukumu,afya,familia na mambo kama hayo ndio chanzo cha kimya changu.
- Weka malengo yanayotimizika au yenye uhalisia-Jiangalie ulipo,angalia vitendea kazi ulivyonavyo,tizama kwa makini ujuzi ulionao kisha yapime vizuri malengo yako.
- Jiulize swali au maswali;Nitayatimizaje malengo yangu?Ukishafanya hivyo jiwekee utaratibu wa jinsi ya kutimiza malengo yako.Wazungu wanasema weka vyema Action Plan yako.
- Nenda taratibu-Mwaka ndio kwanza umeanza,yakaribie malengo yako kwa mwendo wa taratibu.Usiwe na haraka wala pupa.Si unakumbuka kwamba mambo mazuri hayataki haraka?
- Usiogope kurekebisha malengo-Kadri mwaka unavyoanza kusonga mbele,unaweza kugundua kwamba huenda usiweze kutimiza malengo fulani.Hiyo inawezekana kutokea kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi,kiafya au kibinafsi.Usihofu kurekebisha malengo yako.
- Usiogope kushindwa-Yawezekana kabisa ukashindwa kutimiza malengo fulani fulani.Sababu zaweza kuwa kama hizo nilizozitaja hapo juu.Usiogope.Cha muhimu ni kujaribu na kujaribu na kujaribu.Jitahidi kadri unavyoweza.Nina uhakika ukijaribu utafanikiwa kwa hiyo mwisho wa siku hadithi ya kushindwa wala haitokuwepo.
- Omba msaada inapobidi-Yapo mambo mengine ambayo hutoweza kuyatekeleza peke yako.Hilo linapotokea,usiwe mgumu kuomba msaada.
Ni kweli kabisa kuwa tunatakiwa kuwa watu wa malengo ila tatizo linalotusumbua ni pale unapoweka malengo yako halafu baada ya muda unabadilisha malengo tena kutokana na kukoswa labda mtaji wa kufikia ulipopanga.