Mara nyingi nimekuwa nikipokea barua pepe kutoka kwa vijana wakiniuliza wafanye nini ili kusaidia au kuikoa dunia yetu. Huwa napata moyo sana ninapopokea barua pepe za namna hii.
Sasa naomba niseme kabisa kwamba ni wazi hakuna formula moja ya kusaidia dunia. Zipo njia mbalimbali, nyingi kuliko tunavyotizamia. Yapo mashirika yasiyo ya kiserikali chungu mbovu. Mengi kati ya hayo ni ya ukweli. Ni muhimu tukakumbushana kwamba yapo pia mengi tu ya uongo, yale yaliyo kwenye mikoba na matumbo ya wachache. Nchi za Afrika zinaongoza kwa kuwa na mashirikia ya namna hii. Serikali fadhili za magharibi ziliposema serikali za nchi nyingi za Afrika zimejaa ufisadi na hivyo wanaona ni bora wakawa wanatoa misaada yao kwa mashirika yasiyo ya kiserikali hawakujua kwamba viongozi wale wale wa serikali ndio pia wamiliki wa mashirika hayo. Ikawa ni pata potea.Halafu wazungu eti wanasema waafrika hatuna akili! Inakuingia akilini kweli. Sema tu ujanja wetu unakuwa hauna dira.Yaani unaiba hela, unanenepesha tumbo wakati ndugu na jamii yako inaangamia kwa sababu wewe ule mshiko wa kujengea dispensary umeenda kufaidi na hawara yako kwenye ile baa ya kona, pale mkwajuni , karibu na matuta mapya. Ama kweli.
Katika kujaribu kuangalia ni mashirika gani ambayo nadhani vijana wanaweza kujiunga nayo na kusaidia kuokoa dunia ni haya yafuatayo;
The Freechild Project
Free The Children
i-EARN
Peace Child International
TakingITGlobal
Youth Link
Zitembelee tovuti hizo na uangalie ni shirika lipi unadhani unaweza kushirikiana nalo katika harakati zako, iwe ni hapo mtaani kwako, mji unaoishi, wilaya, mkoa nk. Ukihitaji msaada wa tafsiri ya lugha ya kiingereza usisite kuwasiliana nami.
Poa kwa kunyooshea vidole harakati hizi zinazofaa vijana. Kuna ambazo nilikuwa nazijua ila nyingine ndio nimezijulia hapa.
Halafu pale juu kuhusu mrembo yule kuwa kama rais wake. Ni jambo la kuchekesha ila kuna ukweli. Wewe kama una rais wa nchi inayoongea kiingereza lakini akawa hajui hicho kiingereza sawasawa...malizia.