Ni wazi kwamba uteuzi wa baraza la mawaziri la Raisi Kikwete umepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa watanzania. Wapo ambao wameona amefanya uteuzi mzuri kwa maana ya kuteua baadhi ya sura mpya huku wengine wakiona kwamba amerudisha baadhi ya sura zile zile pasipo na rekodi yoyote ya kiutendaji.Wapo ambao wameshikwa na butwaa kuona kwamba "shikamoo" bado zimetamba.Wapo ambao wameona uteuzi wake wa kinamama kushika madaraka ya uwaziri katika wizara nyeti kabisa ni jambo la kujivunia na la msingi.Mimi pia naunga mkono uteuzi wa kinamama,lakini kwangu mimi sio suala la jinsia tu bali suala la uwezo wa kiutendaji.Yapo pia maoni juu ya mzigo ambao Kikwete tayari ameitwisha Tanzania.
Huku wanablogu wengi wakiwa bado vichwa chini wakitafakari,kupitia ule uwanja wangu wa Tanzania Daima kila jumapili,wiki hii (yaani jumapili ya kesho) nimeandika namna hii.Nimeona niweke kabisa waraka huu ili nisije nikasahau.
Nimeingia hapa nikakumbuka kuwa nilikuwa nitazame ukubwa wa sirikali ya Joji Kichaka nikasahau!
ReplyDeleteHivi ukubwa wa Serikali ndio uchapakazi? Hii serikali imekuwa kubwa mno. Wasi wasi wangu ni gharama za kulihudumia> Nchi imewekwa rehani, nadhani.
ReplyDeletenakubaliana na wewe kaka msangi kwa kuchokoza akili za wenzetu kule home katika hili. nia siku zote ni ujumbe ufike hivyo ni heko. sijui kama gazeti, mtanzania daima inauza kopi ngapi kwa siku/wiki? je kati ya hizop ngapi dar na ngapi nje ya dar?
ReplyDeletenakubaliana na uteuzi wa kina mama. ni waelewa na wasiopenda kukaa na mabomu. pia wana utu. kitonda cha hisia kuwa mgombea uraisi wa ajaye kuwa mama ni chema kwani hawa wenzetu hawana mgango wa kurig ili waongoze.
baraza la sasa japo lina gharama lakini ninaona kama muheshimiwa ametaka wabunge nao wamlipe fadhila kwani pia aliwapigia kampeni ya bidii katika ile slogan ya mafiga matatu. sasa anataka kila mtu amsaidie kwenye section husika ya ilani yake. nadhani kama uzalendo utashika nafasi yake inaweza ikawork out. vitu vingine mfano mapuri kupiga wananchi kupitia magereza polisi wangeamuaje? - labda ndo maana kawatenga. unajua kutokuwa na vitambulisho vya uraia vimewanyima watz nafasi na resources zao nyingi? labda tumpe nafasi kama nia yake ni nzuri, mazuri yaweza kupita gharama.
Jeff hicho kiunganishi cha Tanzania Daima kiko kwenye Construction hadi lini? Wengine tulishatanga za ukombozi wa kupata walau taarifa mpya tumechoka kusoma Uhuru na magezeti ya Mengi. Mtaarifu Mbowe mheshimiwa, mwambie asikie kilio chetu na kutuwekea kiunganishi hicho haraka kama alivyofanya kwa kuweka kiunganishi kwa bendera ya Uingereza kwenye ile tovuti ya chadema. (kauli hiyo ya mwisho ni ucheshi tu)
ReplyDelete