Huo msemo kwenye kichwa cha habari nimeusikia toka enzi zile nikiwa pale kijijini kwetu Ndaga.Enzi zile nikiteleza na kuchubuka magoti kwenye changarawe nikiwa njiani kuelekea shuleni.Enzi zile za kujifunza kuandika na kuhesabu.Enzi zile za kuandika chini,nje ya darasa,kwenye mavumbi.Enzi zile za mikufu ya vijiti vya kuhesabia au vifuniko vya soda vyenye tobo katikati vikiunganishwa vyema kwenye uzi.Enzi zile za kuvaa bugaloo siku ya jumapili na kwenda kanisani tuking'aa nyuso kwa mafuta ya mgando!
Enewei hizo ni enzi zile,zimepita lakini hupenda sana kuzikumbuka.Nilichotaka kusema hapa ni kwamba nina uhakika wengi wetu ni wapenzi wa muziki.Na kwa wale wenzangu na mie waliopo "ughaibuni" kuna zile nyakati ambazo unakosa kabisa kupata ladha za muziki kutoka nyumbani Tanzania au barani Afrika.Mimi kwa bahati nzuri kila siku iendayo kwa mungu huwa naburudika na muziki kutoka nyumbani,barani Afrika na dunia nzima.Hili ni jambo zuri au ndio hicho kizuri ninachokisema hapo juu.Sasa kama na wewe unataka kuburudika basi bonyeza hapa. Ukishafanya hivyo kwenye hizo "genre" tafuta African,hapo utakumbana na redio kibao,zinatwanga muziki kutwa nzima.Na kama unapenda "bongo fleva" basi jamaa wa motovibes wapo kwa ajili yako.
jeff, aksante sana. sasa hivi nakula rhumba "juju" music toka kule yoruba land. muziki wao ni tajiri sana.
ReplyDeletecheers
Pata burudani Mark,maisha haya lazima yaendane na burudani la sivyo wote tutaishia Mirembe!
ReplyDeleteUliponimaliza ni hapo ulipotaja mafuta ya mgando. Unakumbuka ashanti? Au ulikuwa hujazaliwa enzi zake?
ReplyDeleteHAya ngoja niende huko kwenye muziki. Asante.
Ndesanjo,enzi za ashanti nilikuwa tayari ninadunda mitaani nikipigana ngumi za "kuputa".
ReplyDeleteNikufagilie kidogo bwana kwa makala ya Jumapili kwenye Tanzania Daima. Sikuwa mnunuzi wa magazeti hayo ila sasa naona utanifanya nikufuatilie kwa huko. Kazi nzuri sana Jeff, lakini kumbuka bado utamaduni wa kusoma hapa nyumbani uko chini sana. Hilo halikatishi tamaa, ni changamoto kwa waandishi na wanataaluma kama wewe, ambao wana moyo wa uzalendo kwa watu wao.
ReplyDeleteNiko kunako muziki haswaa, napata ile kitu roho "inapenda". Siku njema "mzee".
Jeff umenikumbusha mbali sana ulipozungumzia mafuta ya mgando na challenge ya ashati imenifuraisha sana anyway maisha yanaenda yakibadilika ndio maana kizazi cha sasa wanatumia lotion sio mafuta mgando tena. Well done site ya music ni nzuri inasaidia walio mbali na nyumbani kupata muziki wa nyumbani
ReplyDelete