Friday, April 21, 2006

BABU NA BIBI WAKO INDIA?

Mara nyingi tukiwatazama kaka zetu na dada zetu wamarekani weusi sisi tunaotokea Afrika ya Mashariki tunaona kama rangi ya ngozi zetu ndio kiungo kikubwa zaidi cha uhusiano wetu. Hii inatokana na historia ya biashara ya utumwa ambayo inatuonyesha kwamba ni kama hakuna mababu zetu waliopakizwa kwenye meli na kuvushwa bahari ya Atlantiki kuja huku Marekani ya Kaskazini ya leo. Historia inaonyesha kwamba wengi, kama sio wote miongoni mwa watumwa wale walichukuliwa kutoka Afrika ya magharibi na sio kusini wala mashariki mwa afrika. Nadhani ndio maana hata wale wamarekani weusi ambao katika vita ya kujitambua,kujua historia yao,kule watokako huenda zaidi kwenye nchi za afrika magharibi. Unaweza kuwa umeshawahi kusikia jitihada za wenzetu hawa kujitambua kwa kutumia majedwali ya "family tree".

Mwanahistoria, mtafiti Rashid Runoko(Ndesanjo anampata vizuri huyu bwana) yeye anazo hoja zake kabambe akielezea jinsi ambavyo watu weusi walikuwepo dunia nzima kabla na hata baada ya biashara haramu ya watumwa. Hoja za huyu bwana zina nguvu na ushawishi wa aina yake. Ni hoja muhimu sana kuzisoma wakati huu tunapojaribu kufumbua majedwali magumu ya historia zetu na zile za mababu zetu.

Lakini umeshawahi kujua kwamba huko India kuna mababu,mabibi,wajomba,mashangazi na ndugu zetu wa kila aina ambao wanateseka na kuishi katika ufukara wa aina yake kwa sababu tu wao ni weusi?Mateso ya ndugu zetu hawa ni suala ambalo halizungumzwi sana ulimwenguni.Kwanini?Dunia inapoongelea utetezi wa watu weusi huwa inawasahau kabisa watu hawa ambao historia inaonyesha kwamba wanatokea nyumbani kwetu kabisa...afrika mashariki. Soma zaidi hapa na kisha tujiulize kwa pamoja,sauti zile nani atazisikia bila ya sisi kuzisaidia?

5 comments:

  1. Hii inabidi niirejee baadaye. Umefika wakati sasa sisi wenye rangi mbaya tusaidiane wenyewe kwa wenyewe maana hatuna mjomba wa kutusaidia kokote kule.

    ReplyDelete
  2. Jeff safi sana kwa taarifa hii nitapita kuichota baadaye. Kazi nzuri sikuwahi kuwa na mawazo haya huko nyuma, Kweli haya Magazeti Tando yanasaidia sana kutupa habari zilizojificha na ambazo hatukuona umuhimu wake huko nyuma.

    ReplyDelete
  3. Anonymous8:19:00 AM

    Tena Jeff hapa umenikumbusha jambo muhimu sana katika historia ya mababu zetu, tukizingatia wakati ule wa vita ya kwanza ya dunia, hivi kweli mababu zetu walirejea wote kutoka kule Burma na maeneo kama hayo enewei nitapita tena kuchota taarifa hii ni muhimu sana katika historia ya weusi.

    Hii ndiyo inadhihirisha nguvu ya mawasiliano ya umma kama anavyosema Mwaipopo hii rangi nyeusi ni lazima sasa isaidiane si tunawaona hawa wenzetu weupe wanavyosaidiana.

    Jamaa yangu mmoja amenichekesha aliposema weusi noma ndiyo maana tukisugua ngozi zetu halafu tukanusa inanuka mavi ya kuku.(joke)

    ReplyDelete
  4. Anonymous4:29:00 AM

    Hapo Jeff umetugusa wengi sana!Nikiriria jinsi waafrika au watu weusi walivyotawanywa duniani kwa kweli inauma!Hii habari ya India ni nyeti sana kwani mara nyingi tumezoa kusikia wamarekani weusi au Afro-american lakini hatukuwahi kabisa kusikia weusi waliopelekwa India na Uarabuni!Kama navyosema Mwaipopo sisi wenye ngozi nyeusi inabidi tusaidiane sana!

    hii makala nzuri sana bado naendelea kuimeza!

    ReplyDelete
  5. Anonymous6:57:00 AM

    Utafiti umefanyika wa kina kuhusu Waafrika waliosambaa dunia nzim. Kuna vitabu kama African Presence in Early Europe, They Came Before Columbus (African Presence in Ancient America), African Presence in Early America, n.k. Ukiachilia ndugu Runoko, mwingine ambaye amechimba sana haya mambo ni Dk. Ivan Van Sertima (ambaye amewahi kufanya kazi kule Morogoro).

    Historia hizi huwa hatufundishwi mashuleni. Tunafundishwa historia kwa mujibu wa wazungu na sio kwa mujibu wetu.

    Sijui kama mnawafahamu ndugu zetu kule India wanaoitwa Sidis ambao walitoka Afrika Mashariki na hadi leo wana mambo mengi ya kitamaduni (vyakula, ngoma, majina, hadithi, n.k.) vinavyoendana na tamaduni za Afrika Mashariki.

    Labda niongeze pia kuwa mto Ganges unatokana na jina la jemedari wa Kihabeshi (Ethiopia). Kama ilivyo jila "Europe" linatokana na malikia wa Kiafrika.

    Jeff, masomo haya nadhani inabidi tuongeze bidii kuandika maana tusipoandika sisi na kufunza wadogo zetu nani ataandika?

    Shukrani zikujie.

    ReplyDelete