VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, May 21, 2006
DUAL CITIZENSHIP


Kadiri siku zinavyokwenda suala la uraia wa nchi mbili linazidi kujitengenezea ulimbo na hivyo kuzidi kuzua mijadala motomoto kila kukicha. Suala hili lilijitokeza pia hata jana hapa Toronto katika kikao cha aina yake cha watanzania(Habari zaidi juu ya kikao hiki zitafuata siku muafaka ikifika).Ila kwa kifupi kilikuwa kikao chenye manufaa makubwa sana.

Kwa bahati nzuri serikali yetu ya Tanzania,kupitia
tume yake ya kurekebisha sheria imeshaanza kuandaa utaratibu wa kuliongelea kwa mapana zaidi suala hili. Hili linatia moyo kwa sababu wananchi watapata nafasi ya kuchangia na kuamua muafaka wake. Katika pitapita yangu kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali ya Tanzania nimeona hoja hii ikiwa imeletwa katika ukurasa wa mbele kabisa.

Je,tunakubaliana na hoja kwamba uraia wa nchi mbili utakuwa na faida kwa wachache tu hususani wahindi? Je,uraia wa nchi mbili utaondoa "uzalendo" kama anavyodai Profesa Shivji ambaye kwa asili yeye ni mhindi? Tuanze tena kulijadili hili kwa sababu ninavyoona hivi karibuni tutakuwa na kibarua cha kueleweshana na wabunge wetu kuhusu njia gani tuelekee kabla hawajaenda
bungeni Dodoma kufanya maamuzi ya mwisho.Kwa habari zaidi soma hapa. Pichani ni pasi za kusafiria za Tanzania na Canada ambazo kama uraia wa nchi mbili utaruhusiwa basi kuna watu watakuwa nazo zote mifukoni mwao.

Leo hii Ndesanjo kanikumbusha kwamba suala hili tuliwahi kuliongelea tena siku za nyuma.Pia akaniomba niweke kiungo cha mjadala ule.Binafsi nilikuwa nakumbuka vizuri sana mjadala mtamu tuliokuwa nao mara ya kwanza nilipoandika kuhusu hoja hii.Nilionelea kuirudisha tena kwa sababu ambazo nimezitaja hapo juu...lipo mbioni kuelekea Dodoma. Kwa kumbukumbu za mjadala ule na maoni ya washika dau wa blogs soma hapa.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:18 PM | Permalink |


Maoni: 9


 • Tarehe: 9:26:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger SIMON KITURURU

  Mimi sioni ni kwasababu gani tusiruhusiwe kuwa na pasipoti mbili.Siamini kuwa kwakuwa na pasipoti mbili Utaifa unapungua.Kwanza kwa Mtanzania Unaunganishwa na Taifa lako kinamna nyingi sana.Ndugu zako asilimia kubwa wako na watakuwa Bongo.Kuna ukweli sio watu wote watakaotaka kuwa na Pasioti mbili.Si lazima kila mtu atake pasipoti zaidi ya moja.Lakini kusema kwamba Wachache watanufaika ni sawa na kusema kuwa kama si wewe basi mwingine asipate.Hii kwangu ni kama ubinafsi usio faa.Kuhusu kuwa watu watakuwa wanaiba bongo kwenda kuwekeza nje, watu wanafanya hivyo leo hii.Na kama mazingira ya Bongo yatakuwa yanalipa kiuwekezaji kwanini isiwe kuwa watu watakuja kuwekeza Bongo?Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania haiguswi bado na jambo hili, kwasababau wanaishi ndani ya Tanzania na hawajawahi kutoka nje ya Taifa.Lakini kuna kundi la wasomi ambao ni wamanufaa kwa maendeleo ya Tanzania ambao wako nje, ingawa watu watasema ni wachache ila Mchango wao unahitajika sana na wangeweza kutoa mchango wao kirahisi zaidi ingawapo wangeweza kuishi, kufanyakazi na kusafiri katika nchi zaidi ya moja.Hii haina maana kuwa utanzania unawatoka.

   
 • Tarehe: 10:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger zemarcopolo

  suala la uraia wa nchi mbili lina manufaa kwetu watanzania.uzalendo ni kitu kiko moyoni mwa mtu na sio kitu cha mtu kulazimishwa kwa kukatazwa kuwa na uraia wa nchi nyingine.mimi kama mtanzania nikipata uraia wa nchi nyingine na sawa tu na kupewa endless visa!je kuna ubaya gani kupata kibali cha kuishi nchi fulani????halafu wanasheria wetu ni lazima wajue kitu kimoja.tunapotunga sheria siyo lazima sheria hiyo ifanane na sheria ya nchi fulani.mfano tunaweza kusema raia wa tanzania wa kuzaliwa wanaruhusiwa kuwa na uraia wa nchi mbili au zaidi ila raia wa nchi nyingine akitaka uraia wa tanzania ni lazima arudishe uraia wa nchi yake.tunaweza kutunga sheria kadri tunavyoweza kunufaika sisi watanzania.sio lazima iwe logical au undestandable kwa watu wengine.nitakupa mfano:daktari aliyesoma katika jumuiya ya ulaya akitaka kufanya kazi uingereza anaruhusiwa kufanya hivyo bila kupewa mtihani wowote,lakini iwapo datktari huyo siyo raia wa nchi mwanachama wa jumuiya ya ulaya ni lazima afanye mtihani wa kiingereza na mtihani wa udaktari kabla hajaruhusiwa kupractice hata kama amesoma kwenye jumuiya ya ulaya.there is no logic here,thats what benefits them and they decide it that way.katika ishu ya uraia pia twaweza kuweka sheria zinazowanufaisha wazawa hata kama hazitakuwa na manufaa kwa wageni!

   
 • Tarehe: 9:24:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Indya Nkya

  Uzalendo bwana haupimwi kwa karatasi. Mimi nadhani kuna watu wameishi na pengine kuwa na uraia wa nchi nyingi lakini bado nimioyoni mwao ni watanzania. Nimekutana nao wengi wanataka uraia wao wa Tanzania ubaki. Lakini kuna wasio na uzalendo hata kama hawana uraia wa nchi mbili. Kwa hivyo hili suala si la ajabu kwa Tanzania. Leo hii ukiangalia nchi kama India japo wahindi wana uraia wa nchi hata tatu bado wanarudisha mabilioni nyumbani. Yupo Tanzania lakini moyo upo India

   
 • Tarehe: 11:20:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Jeff, nadhani kuna wakati uliandika kuhusu hili kukawa na mjadala mzuri sana. Ukiweza kutuwekea kiungo cha ule mjadala na yale uliyoandika itakuwa safi sana. Nimetafuta sikufanikiwa kupata.

   
 • Tarehe: 12:17:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Ahsante Ndesanjo,
  Nimefanya uhariri kidogo hapo juu ili kutoa nafasi kwa wale ambao walikuwa hawajawahi kufuatilia mjadala huu huko nyuma.

   
 • Tarehe: 9:12:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

  Jeff,

  Tafadhali naomba utuletee habari za yule Dada wa Kisomali aliyejilipuwa Uholanzi. Akapanda ngazi mpaka kuwa mbunge wa chama cha mrengo wa kulia. Mwezi huu wakambaini na kumbana wakamwachisha ubunge na kutaka kumnyang'anya uraia. Wazee wa American Enterprise Institute wakamuona potential recruit sasa hivi yuko Washington anakula sahani moja na Hawks e.g Bush Jr, Dick Cheyne, Ronald Rumsfeldt Benjamin Kagan, Paul Wolfowitz, wa American Enterprise Institute.

  Miye yule dada simcondone wala kumcondem. Nasubiri toka kwako.

  F MtiMkubwa Tungaraza.

  PS/Bado nasubiri ule ujumbe wako kupitia barua pepe.

   
 • Tarehe: 11:04:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous ndesanjo

  Hisia zangu (yaani machale) zinaniambia kuwa uraia zaidi ya mmoja utakubaliwa Tanzania. Kama sio sasa basi ni hapo baadaye kidogo. Dunia inavyokwenda na inavyozidi kuwa ndogo na pia kuwa tambarare (kama anavyotuambia Thomas Friedman kwenye The World Is Flat) kukataa hoja ya uraia wa nchi zaidi ya moja kutakosa hoja za msingi.

  Asante kwa kutupa kiuongo cha mjadala ulioanzisha huko nyuma.

   
 • Tarehe: 11:08:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Jeff Msangi

  Mti Mkubwa,
  Ahsante kwa kunikumbusha suala la huyu mama wa Kiholanzi.Nitalitafutia viungo na kuliandikia.
  Sijakuandikia email kwa sababu sina email address yako.Nitumie japo kaujumbe kafupi kwenye jeffmsangi@sympatico.ca ili nipate address yako.

   
 • Tarehe: 1:05:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger P. Situmbeko Nalitolela

  Kwanza kabisa najua mjadalaa huu ni wa kimabo kidogo, karibia miezi miwili sasa. Lakini kama tulivyoongea karibuni kaka Jeff, miezi ya kati hapa bwana shule ilikuwa imebana mno nikapitwa hata na mambo mengi ya maana katika tovuti yakoo hii na nyinginezo nyingi.

  Bila kupoteza muda zaidi ngoja nirudi katika maada husika, yaani uraia wa nchi mbili.
  Kwanza kabisa ningependa kusema kuwa mie binafsi ninaunga mkono kuwepo kwa sheria itakayoruhusu raia wa Tanzania kuwa raia wa nchi mbili. Kabla sijatoa hoja zangu binafsi zinazokubaliana na maada hii, ninegependa kugusia masuala mawili matatu yaliyoongelewa na wenzangu mwanzo amabyo nayaunga mkono kwa asilimia 200.
  La kwanza ni la ndugu yangu Simon Kitururu aliyesema kuwa wanaopinga hoja hii kwa madai kuwa itawafaidisha watu fulani ni ubinafsi usio na maana. Nimeipenda sana hoja hii na ningependa kuonegezea kusema:
  Ni kweli kuwa kuna hatari ya baadhi ya watu hususani wale wasio raia wa Tanzania kutaka kutumia fursa hii kuchumia Bongo na kuwekeza nje.
  Lakini hatuwezi kuepuka kupitisha sheria ambayo pengine itawnufaisha watanzania wote kwa kuhofia kuwa fulani atanufaika zaidi ya mwingine.
  Isitoshe tunaweza kuzitunga sheria kwa namna ambavyo wanyemela kama hawa wenye nia ya kutunyonyoa tutaweza kuwakamata maana tutakuwa "janja ya nyani kula indi bichi kwishajua".
  Mojawapo ni pendekezo la ndugu zemarcopolo kuwa tunaweza kuwazuia raia wasio wazawa kupata uraia wa nchi nyingine kupitia mgongo wa Tanzania kwa kuchukua uraia wetu kwanz akisha kuomba uraia wa pili wa nchi wanayoipendelea wao. Na tunaweza kufanya hivi kwa kuweka sheria itakayoruhusu raia wale waliopata uraia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kurithi tu ndio wanaweza kupata uraia wa nchi nyingine. Hii itasaidia kudhibiti uwezekano wa watu kufanya uraia kama suruali sasa ambayo unabadili kila kukicha, au kila mtindo mpya unapotoka.

  Zaidi ya hapo hatuwezi kujibana kwa kuhofia kuwa watu wataihujumu Tanzania na kutorosha mali zetu. Kwani tunaweza kuwa na sheria ambazo zinadhibiti utoroshaji (laundering) wa fedha kwa kusema kuwa kilichochumwa Tanzania kitalipiwa kodi Tanzania na kitaiendeleza Tanzania angalau kwa silima fulani. Kwani hata katika nchi zenye uhusiano wa karibu kama Kanada na Marekani huwezi kuhamisha mali tu jinsi unavyojisikia eti kwa kuwa una uraia wa nchi zote mbili. Vinginevyo uzani (balance) wa matumizi katika nchi kadhaa ungekuwa mashakani kutokana na wananchi wake kuruhusiwa kuwa na uraia wa mchi mbili.

  La tatu ambalo ningependa kuligusia kwa kifupi tu maana limeshatajwa sana na liko wazi kabisa ni kuwa: UZALENDO WA MTU HAUPIMWI KWA KARATASI!!

  Na mwiso kabisa ningependa kuongezea sababu yangu binafsi ambayo najua imeshagusiwa kidogo kwa namna 1 au nyingine na waliotangulia, lakini inanigusa binafsi na napende kutilia msisitizo zaidi.
  Hili ni suala la wataalamu mbali mbalia mbao wamepata bahati kusoma au kufanya kazi nje. Nikiwa binafsi niko masomoni ughaibuni, nimeshamaliza shahada ya kwanza na natafuta ya pili sasa; nashuhudia vijana wengi wanaotoka nchi masikini kama zetu ambazo haziruhusu uraia wa nchi mbili wanavyojikuta wakibanwa katika kona pindi wamalizapo mafunzo yao.
  Mara kadhaa unakta mtu unapomaliza masomo unabahatika kupata nafasi fupi ya mafunzo ya kazi, na inakuwa nafasi amabayo una uwezo wa kupata mkataba wa muda mrefu zaidi (pengine mwaka, au miaka michache ya nyongeza) kwa maslahi amabayo unatamani kwa kweli uendelee kidogo kujibanza huku ili uzikusanye anagalau ukitua Bongo uweke kibanda chako na we uswahilini.
  Tatizo linakuja nchi za huku zitataka kukubana kuwa ili uongeze mkataba wako lazima uombe vibali 100 kidogo. Na makodi kibao juu yake ukiwa sio raia. Ama sivyo, ukitaka kujirahisishia mambo basi uchukue uraia. Sasa unapiga mahesabu ukiangalia kweli kazi ina manufaa kifedha na pia kielimu na kibinafsi. Unawez kukuta unafanya kazi ambayo Bongo huwezi kupewa majukumu yafananayo na haya ambayo yanakufaidisha kitaaluma.
  Hivyo kujiondolea adha ya kuomba maviza na vibali na kukatwa kodi lukuki, wenye roho nyepesi wanaona liwalo na liwe bwana. Wacha nichukue zangu tu uraia wa huku maana wanaithamini kazi yangu pengine zaidi ya Bongo.
  Hivyo basi tukiwa na uraia wa nchi mbili, tutazuia kumpoteza mtaalamu kama huyu 1 kwa 1 kwa kumpa nafasi kurudi Bongo kwa wakati wake kuwekeza pale anaporidhika na yale aliyoyapata katika nchi nyingine.

  Na hivyo Tanzania itafaidika kwa kiasi fulani na uwepo wake badala ya kumpoteza kabisa kwa nchi nyingine.


  Hayo ni machache niliyokuwa nayo; mtaniwia radhi kwa maelezo marefu mno. Lakini suala hili kwa kweli limekuwa likinikuna kwa siku nyingi na nimefurahi nimepata sehemu ya kupunguza "hasira" zangu kidogo heheh.

   
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker