

Ukisema ulikwenda kutembea,kuhudhuria mkutano/kongamano,kusoma au kuishi Canada hususani kwenye jimbo la Ontario basi si ajabu ukaulizwa kama uliwahi kupanda/kutembelea CN Tower au kama ulikwenda kuyaona maporomoko ya maji ya Niagara(Niagara Falls). Kwa wale ambao hamjawahi kuyaona au kufika hapo Niagara leo nimeona niwaletee picha ya maporomoko haya nikitumaini kwamba wikiendi yako ilikuwa njema.
Maporomoko ya niagara ni makubwa kuliko ya victoroa falls?( samahani kwa ku-genisha mali asili ya waafrika.)
ReplyDeleteMloyi,
ReplyDeleteKwa urefu Victoria Falls ni marefu kushinda haya ya Niagara ila kwa ukubwa/upana Niagara Falls ni makubwa kushinda Victoria.
Mloyi, maporomoko wazungu waliyoyaita Maporomoko ya Vikitoria yanaitwa Mosi O Tunya! Yaani moshi utoao mlio kama radi.
ReplyDeleteJeff, naona unaelekea kuwa Michuzi mdogo siku hizi. Kakupa kizizi nini? Unarembesha kazi zako vizuri sana kwa mapicha. Tunafaidi. Endelea mwanakwetu.