VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, November 07, 2006
KURA YAKO BADO INAHITAJIKA!
Natambua wazi kwamba wengi wetu vichwa bado vichwa vinauma kufuatia tukio la kifo cha mtanzania mwenzetu Hassan Mbonde. Mbonde ameiaga dunia kufuatia mkono wa mtanzania mwenzetu mwingine, mtu tuliyeamini kwamba ni kiongozi na wala sio mtoa roho! Pole nyingi kwa wote walioguswa na msiba huu na ambao wanaamini kwamba kila mtu ana haki ya kuishi hata kama hana kitu,hajulikani kwa yeyote,hana jina linalovuma kama upepo wa nyika.

Matukio kama haya ya kinyama na uonevu ni mengi,yanatokea kila mara. Hili limevuma labda kwa sababu limetokea jijini Dar ambapo angalau kuna vyombo vya habari, kuna wapiga vipyenga (whistle blowers) ambao wasingeweza kukaa kimya.Hawastahili kukaa kimya. Je, ni mangapi yanatokea huko mikoani na wala yasisikike? Ni wananchi wangapi wanaonewa,wanavuliwa utu wao,wanadhalilishwa,wanauawa na wale ambao wanajificha kwenye kivuli cha "ukubwa"?

Ni sababu na tafakuri kama hizi ambazo zinafanya iwe muhimu sana kwa taasisi za umma kuundwa na kuwa imara ili kuhakikisha thamani ya maisha ya kila mtu inaheshimiwa. Haki za kila raia zinaandikwa katika kila paji la uso.Ndio maana mkutano wetu wa Jumamosi Tarehe 18, Novemba,2006 unazidi kuwa muhimu. Bado ukumbi wa kupiga kura ya kuchagua muda upo wazi.Ukumbi utakuwa wazi mpaka Jumapili Tarehe 12, Novemba,2006(wiki hii mwishoni) Baada ya hapo ukumbi wa kupiga kura utafungwa kisha kura zitahesabiwa ili tuafikiane rasmi muda muafaka wa kukutana. Mpaka hivi sasa wanaosema tukutane kuanzia saa nane mchana kwa saa za Tanzania wanaongoza.Kama bado hujapiga kura yako tafadhali bonyeza hapa ufanye hivyo.

Kama hukusoma tangazo la kwanza juu ya mkutano huu bonyeza hapa. Ukitaka kujua jinsi gani mkutano huu utafanyika bonyeza hapa. Kumbuka tu kwamba hata kama huna blog bado unakaribishwa kushiriki mkutano huu.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:34 PM | Permalink |


Maoni: 7


  • Tarehe: 11:19:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

    Kaka Jeff,asante sana.Ningependa Blogu itumike kama ketetea wale ambao wananyanyaswa na mtu yeyote.Ingekuwa vizuri kama tungetumia blogu zetu kuchapisha yale yanayo tokea katikata sehemu tofauti tofauti hapa Tanzania na Duniani kwa jumla.Blogu ni kioo cha jamii na huu ni wajibu wetu.

    Naomba kuwakilisha.
    N.B.Siku za karibuni umeme umekuwa hapatikani kwahiyo naomba tuwe makini kuchaguwa siku na saa.

     
  • Tarehe: 8:03:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Luihamu,
    Taarifa za umeme tunategemea basi ninyi ndio mtuambie. Kumekuwa na taarifa zinazotofautiana kuhusu saa umeme unapatikana. Kwahiyo unaposema tuwe makini ingekuwa vyema ukatoa taarifa zaidi ili tujue jinsi ya kuwa makini. Bila kuwa na taarifa zaidi kuhusu upatikanaji wa umeme (saa, siku, n.k.) itakuwa vigumu kujua tuwe makini kivipi.

    Lakini sehemu nyingi zenye migahawa ya intaneti si zinatumia majenereta? Au?

     
  • Tarehe: 10:08:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger luihamu

    @Ndesanjo

    Sehehu nyingi zinazotoa huduma ya mtandao zinatumia jenereta,lakini wanalipisha kiasi kikubwa cha hela kwa mfano lisaa 1500/2500.Najaribu kudadisi,kama wakikata umeme Ijumaa,inamaana tutapata umeme Jumamosi,lakini wakiwasha umeme Ijumaa hatutapata huduma ya umeme Jumamosi.

     
  • Tarehe: 5:44:00 PM, Mtoa Maoni:- Blogger MICHUZI BLOG

    Jeff/Ndesanjo!

    je kuna uwezedkano wa kula tizi kwanza kabla ya huo mkutano? yaani, naomba ikiwezekana tufanye zoezi/mazoezi kabla ya siku ya siku, na ndesanjo/jeff utoe maelekezo kabla na tujaribu, sema kwnye jumapili hii, ili tuone tuko wapi. nasema hivi kwa sababu sio wote wenye utaalamu wa kufika mkutanoni. nina maana jeff/ndesanjo mtoe maelekezo mafupi kabla ya siku hiyo na tujaribu kukutan mara mbili ama tatu tuione ama tusahihishe namna ama jinsi ya kufanya.

    naomba kutoa hoja

     
  • Tarehe: 1:23:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Mija Shija Sayi

    Michuzi hilo ulilolisema nalo lina umuhimu sana, maana itasaidia siku yenyewe watu kutokuchelewa kuingia mkutanoni. Naunga mkono.

     
  • Tarehe: 7:48:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Rama Msangi

    kwa wale wenye kuhitaji vile vihesabu muda, kuelekea siku ya mkutano wetu, mnaombwa kuwasiliana na MK

     
  • Tarehe: 4:00:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Ni sawa tunaweza kufanya majaribio ili kujua kabisa tunafanya nini tusije poteza muda siku hiyo. Ni akina nani na nani wanataka kufanya majaribio, lini, saa ngapi?

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker