Baada ya zoezi la kupiga kura ili kuchagua muda muafaka wa mkutano wetu, imeonekana kwamba waliopendekeza saa nane mchana kwa saa za Tanzania wameshinda.Kwa maana hiyo mkutano wetu wa kwanza wa wanablog, wasomaji,wachangiaji,watanzania,mimi na wewe utafanyika Jumamosi ya Tarehe 18 Novemba,2006 kuanzia saa nane mchana kwa saa za Tanzania.
Ukurasa wa wiki wa mapendekezo ya ajenda za mkutano huu bado upo wazi. Unaweza kuupata ukura huo kwa kubonyeza hapa.Unazo haki zote za kimsingi za kuchangia na kutoa mapendekezo yako pale pale.
Shukrani nyingi kwa wote ambao wameshiriki zoezi la kupiga kura ya kuchagua muda.Tunaweza.
Kaka Jeff hamna kukata tamaa,tumekaza buti moto bati,acha tu.
ReplyDeleteJeff!
ReplyDeletesamahani, lakini imebidi nibandike kwa hayo ya hapo chini ambayo nadhani yanafaa kuwa ajenda, kwani yaonesha kiswahili kinabaguliwa na watu wa google ingawa kinaungumzwa karibu dunia nzima.
kwa maana ingine ni kwamba iko haja ya kutafuta njia za kufuta jasho watu wenye kuhangaika kama wewe kwa njia ya matangazo, lakini hili linakatisha tamaa.
nimeleta mada hii kwako kwa uchambuzi na ushauri pia. kaka ndesanjo na makene na wengine naomba tulivalie njuga swala hili ili kiswahili kipitishwe kupokea matangazo kama ilivyo kwa hao wenzetu watajwa kwenye link zao hapo chini
nawasilisha hoja huku nikifyumu
Hello Muhidin,
Thank you for your interest in Google AdSense. Unfortunately, after
reviewing your application, we're unable to accept you into Google
AdSense at this time.
We did not approve your application for the reasons listed below.
Issues:
- Unsupported language
---------------------
Further detail:
Unsupported language: We have found that the content of your site is
primarily in a language that we do not support at this time. A full
list of supported languages is available at
https://www.google.com/support/adsense/bin/answer.py?answer=9727&hl=en_GB .
If you manage or own another site in one of our supported
Michuzi,
ReplyDeleteAhsante kwa kulileta hili kibarazani.Ni kitu muhimu sana kufanyika ili lugha yetu itambuliwe zaidi.Ngoja niangalie nini tunaweza kufanya.
Hili kweli la kulivalia njuga. Jeff, tupe maendeleo utakapofikia.
ReplyDelete