Sunday, November 12, 2006

SIKU YA MWISHO YA KURA

Kama ilivyotangazwa ijumaa iliyopita, leo ndio siku ya mwisho ya kupiga kura ili kuchagua muda muafaka wa mkutano wetu wa Jumamosi ijayo Tarehe 18 Novemba,2006. Kura zilikuwa zikipigwa hapa. Hivyo kama bado hujapiga kura yako na ungependa kufanya hivyo kabla ya siku hii kumalizika unaweza fanya hivyo kwa kubonyeza hapa na kufuata maelekezo katika ukurasa utakaofunguka.

Halikadhalika, ukurasa wa kuandaa ajenda (zoezi pekee lililobaki) za mkutano wetu upo wazi kwa kila mtu na mapendekezo yanaendelea kutolewa. Fungua hapa uone mapendekezo yaliyokwisha tolewa na pia utoe ya kwako nk.

2 comments:

  1. Kaka Jeff,Gazeti Tando la Rastafarian limeungana na gazeti tando la kijiweni rundugai,kwa hiyo nitakuwa napatikana katika
    www.rundugai.blogspot.com
    karibuni wote.jah live.

    ReplyDelete
  2. Ahsanteni sana kwa taarifa na hongereni sana kwa muungano.Umoja ni nguvu.Ni wazi kwamba mambo mengi yataendelea kutujia kutoka kwenu.Kila la kheri na ahsanteni kwa kuwa mfano wa ujamaa.

    ReplyDelete