Matokeo ya raundi ya kwanza kuelekea mwisho wa tuzo za Blog bora nchini Canada yametoka. Kama mnavyojua blog yangu ya kimombo African Perspective kwa mara ya kwanza ilikuwa imeteuliwa kuwania tuzo hizo katika kundi la blog bora za kitamaduni.
Kwa bahati mbaya blog hiyo haikuweza kuchaguliwa kwenda raundi ya pili ya mchuano huo. Unaweza kutizama matokeo kwa kubonyeza hapa.Je,hilo linakushangaza? Mimi binafsi limenishangaza lakini sina budi kukubali kushindwa ili niwe mshindani (wakati mwingine labda). Asiyekubali kushindwa........
Ninachojua hivi sasa ni kwamba wengi wenu mlinipigia kura. Idadi ya barua pepe,simu,ujumbe mfupi wa simu za mkononi nk zilitosha kabisa kunionyesha jinsi gani mlinipa kura zenu.Kwa hilo sina budi kuwapeni shukrani zangu za dhati.Ahsanteni sana sana.Kilichotokea upande wa pili,baada ya kura zenu kuhesabiwa sikijui na wala huenda nisije kijua milele.Tekinolojia bwana,zina mambo yake!
Kwa wale ambao,kwa sababu moja au nyingine,hamkuweza kupiga kura wakati huu,tutajaribu tena wakati mwingine,inshallah.Nitaendelea kuandika kwa kutumia hizi lugha mbili,kiswahili na kule African Perspective,kwa kiingereza.
Sasa kwa sababu siku zote huwa inaudhi kushindwa, kumpigia kura mtu wako kisha asishinde, nimeona nikupe burudani kidogo na wimbo huu hapa chini wa hayati Bob Marley unaoitwa Three Little Birds(Ndege watatu wadogo).Ahsanteni sana.
Mimi kwa mtazamo wangu bado wewe ni mshindi.Mimi nilizipitia zile blogu zote zilizokuwa zinashindana chini ya utamaduni .Na ya kwako bado inaendelea kuwa iliyo mshindi kwangu.
ReplyDeleteJeff,
ReplyDeleteWaliwahi kumshindanisha Maradona na Pele nani mchezaji wa karne? Akashinda maradona! Kwa hiyo usishangae. Kura zetu ulizipata!Hongera kwa pale ulipofikia.
F MtiMkubwa Tungaraza.
Sina la kusema ila tu Nabii robert nesta marley kasema.long live jahrastafarian.
ReplyDeleteWimbo umeshanifanya ni "Feel-Good" Asante Kaka.
ReplyDeleteNilizipitia blogu ulizoshindanishwa nazo. Hayo matokeo hayana uhusiano wowote na hali halisi.
ReplyDeleteNakupongeza kwa kupeperusha bendera ya Uafrika kikamilifu. Mimi naamini umeshinda mpaka hapo.
Kazi ndio kwanza umeianza. Mwendo ni mbele kwa mbele.
Naandika kukupongeza kaka. Hongera!
Jeff!
ReplyDeletePamoja na matokeo hayo bado binafsi nakupa pongezi nyingi kwa ushindi unaotokana na kazi yako nzuri,
Iko siku.
/maggid