Tuesday, January 30, 2007

MSOME MAKENE NA WARAKA WAKE KWA JK!

Uandishi wa habari wa Tanzania mara nyingi umekuwa ukibezwa kwa kuwa wa "kioga".Uandishi wa habari kama mhimili muhimu katika maendeleo ya taifa imekuwa ni kama njozi isiyoisha kiasi kwamba tofauti kati ya ndoto na ukweli imekuwa ngumu kutambulika.Dhihaka hizo ndizo zilizomfanya mchora katuni,mtanzania anayeishi Kenya kuibua mjadala wa aina yake alipoakisi kwamba waandishi wa habari wa Tanzania "wanalamba" viatu vya mheshimiwa raisi. Mjadala mkali sana ulizuka lakini mwisho wa siku mwenye masikio alisikia na mwenye macho aliona.

Boniface Makene,mwanablogu wa siku nyingi,rafiki yangu,siku zote amekuwa akipiga vita suala la kuandika "porojo" huku zikisindikizwa na woga.Ukimsoma Makene kwa makini utagundua kwamba anapenda kutumia kalamu yake ya uandishi kama silaha halisia katika kuelimisha,kukosoa na kuelekeza na pia hata kuburudisha inapobidi. Leo Makene amemuandikia raisi waraka mzito,wenye tungo makini.Tafadhali usome waraka huo kisha fungua mabano.

2 comments:

  1. Nimepita kwenye kasri, habari aliyoandika ni murua sana. Ahsante kwa kutubonyeza.

    ReplyDelete
  2. Anonymous5:24:00 PM

    Nimepita pale na kuacha maneno yangu maana makala ile nimesema imeonyesha moja ya silaha tulizonazo dhidi ya uozo katika viambaza vya utawala: ujasiri na umakini.

    ReplyDelete