
Si ajabu ushawahi kusikia juu ya maporomoko ya maji yanayojulikana kama Niagara Falls,yaliyopo hapa Canada. Pichani juu ni boti inayojulikana kama Maid of The Mist ambayo ni kiburudisho cha aina yake.Inachofanya boti hiyo ni kukupeleka chini ya maporomoko ya maji ili uweze kuyaona kwa karibu sana. Kama unavyoona kwenye picha hapo juu, abiria hulazimika kuvaa makoti ya plastiki kwa sababu kuloa ni jambo la kawaida kabisa ukishapanda boti hiyo. Historia kamili ya boti ina mvuto wa aina yake.
hapa naangalia hii boat halafu najiuliza,wakati unapiga hii picha ulikuwa umekaa wapi kwa sababu inaonekana ulikuwa katika chombo kirefu kuliko hii boat!
ReplyDeleteJeff,
ReplyDeleteShukrani kwa kutuletea mambo ya Niagara Falls.
Zemarcopolo,
Hapo bila shaka Jeff alikuwa nchi kavu, sehemu ambayo iko juu usawa wa maporomoko yenyewe.
ooh ok,cheers GK.
ReplyDeleteZermacopolo,
ReplyDeleteNi kweli kabisa alivyosema Patrick,nilikuwa nimesimama nchi kavu ambako hiyo boti ni kama inapita chini yake.