Saturday, March 31, 2007

MTAANI


Ukitembelea jiji la Toronto utakuwa hujakamilisha matembezi yako kama hutotembelea mtaa maarufu wa Yonge ambao unasemekana ndio mtaa mrefu kupita yote duniani.Halikadhalika ukitembelea jiji la Chicago (kule Michael Jordan alipojipatia umaarufu mkubwa wakati akichezea timu ya mpira wa kikapu ya Chicago Bulls) utakuwa hujakamilisha ratiba usipotembelea Michigan Avenue kama unavyoonekana pichani.Na ukiwa jijini Dar-es-salaam halafu usikatize Samora Avenue (zamani Independence) utakuwa umekamilisha ratiba?

Wakati huo huo hebu soma habari ya askari aliyekutwa uchi baada ya kumbaka mahabusu binti wa miaka 15 ambaye alikuwa mahabusu kwa madai ya kumuibia mwajiri wake.Tafakari,binti wa miaka 15 tayari alishakuwa na "mwajiri".Hivi huyo aliyekuwa mwajiri wake naye hana kosa la kuajiri mtoto?

NB:Picha haina mchanganuo (resolution) wa kutosha kwa sababu ilipigwa tokea ndani ya gari kupitia kioo cha upepo.

2 comments:

  1. Anonymous2:11:00 PM

    Nadhani huyo askari na mwajiri wa mtoto wote wana makosa.Washitakiwe

    ReplyDelete
  2. Anonymous6:51:00 AM

    Na ukifika Moshi lazima upite pale "Dabo Rodi."

    ReplyDelete