VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Thursday, April 26, 2007
TUFANYEJE?
Kama kuna faraja yoyote ambayo nimeipata tangu nilipoiweka hadharani picha ya watoto-wanafunzi waliokalia mawe hivi majuzi (kama hujui nazungumzia nini bonyeza hapa) ni jinsi gani sote tumekerwa na kudhamiria kufanya kitu ili kubadili hali hii.Maoni yaliyomiminika, simu mlizonipigia baadhi yenu, barua pepe mlizonitumia zilitosha kunihakikishia kwamba vita hii inawezekana kupiganwa.Tunachohitaji sasa ni kuazimia kuianza rasmi.

Serikali zetu, tawala na zote zilizopita haziwezi kukwepa lawama kwa kushindwa kwake vibaya katika kuleta mabadiliko ya kijamii yanayostahili,yaliyo ya haki na yanayotarajiwa.Tunapoongelea serikali tunaongelea suala zima la uongozi.Tunakuwa na viongozi ili sio tu kuheshimu dhana nzima ya demokrasia bali pia kupata watu wa kutusaidia katika kuijenga dira, kuleta mabadiliko ya kijamii, na kuzivusha jamii zetu kutoka upande mmoja mpaka mwingine.

Picha ya watoto-wanafunzi waliokalia juu ya mawe, ndani ya jengo chakavu kabisa huku wakionekana na kuwa na kila dalili ya njaa, ukosefu wa matumaini na ambao inaonekana jamii imewasahau imetukera, imetuhuzunisha na kutukumbusha wajibu mzito tulionao kama watanzania.

Ukiwauliza jamaa wa serikalini,viongozi,wabunge,mawaziri nk hawatokosa majibu. Hiyo ndiyo sheria ya kwanza ya taaluma ya siasa. Usishangae pia ukisikia lawama zikienda kwa wafadhili, IMF na Benki ya dunia na mara nyingine kwa kufoka kabisa,wakiwatupia wananchi lawama.Imeshatokea hata mwananchi kukabiliwa na kifungo kwa sababu alimuuliza mbunge wake swali gumu!

Japokuwa naafiki kuna mantiki fulani katika kuzitupia lawama jabali hizo za masuala ya fedha duniani kuhusiana na mustakabali mzima wa maendeleo, zaidi naamini kwamba wanasiasa na viongozi wetu siku hizi wanazitumia zaidi kama ngao ya kukwepa lawama na majukumu tu.Yapo mambo chungu mbovu ambayo yanawezekana bila kutegemea ufadhili wa mtu au nchi yeyote.Mbona hata hayo hayafanyiki? Tuna viongozi kweli? Kama serikali yetu inatoza kodi, inapiga tambo za kukua kwa uchumi na wakati huo huo inaweza kuwapatia viongozi wake vitendea kazi vyenye thamani kubwa mara dufu kushinda sio tu kipato chao bali pia kipato cha taifa, inashindwa vipi kuhudumia sekta muhimu kama ya elimu?Tunapata wapi fedha za kutupa kwenye kashfa nzito kama Richmond na ununuzi wa rada lakini tukashindwa hata kuwachongea wanetu madawati achilia mbali kuwapatia walimu na vitendea kazi vingine?

Tufanye nini? Hili ndilo swali ambalo hatuna budi kusaidiana kulijibu kwa pamoja. Jambo la kwanza ambalo naamini tunaweza kulifanya ni kutochoka kuhoji,kukemea na kusaidia kwa kutoa mchango wetu wa hali na mali. Tusiishie kuandika tu huku kwenye mitandao na wakati mwingine kutupiana lawama hata miongoni mwetu sisi wenyewe.Jambo moja ambalo ni muhimu sana ni kumuuliza mbunge kwa mfano wa jimbo hilo la Morogoro Kusini Hamza Abdallah Mwenegoha kwanini hali katika jimbo lake ni ya kukatisha tamaa na kutia aibu kwa kiwango kile? Binafsi nimeshafanya hivyo kwa kumuandikia barua pepe nikiambatanisha picha ile na kuhoji kwa kina,kulikoni? Ingawa bado sijapata majibu na pengine sitopata majibu kamwe nina uhakika kwamba ujumbe umemfikia na hivyo atatambua kwamba dunia inamtizama. Ukipenda kumtumia barua pepe pia unaweza kwa kutumia anuani ya hmwenegoha@parliament.go.tz
Usiishie kwa Mwenegoha peke yake bali pia mbunge wa jimbo
lako, kule utokako au kule ilipo familia yako,asili yako nk. Kwa bahati nzuri anuani za barua-pepe,simu za nyumbani, za ofisini, za kiganjani za wabunge wetu zimeorodheshwa katika tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Utaratibu mwingine wa kusaidia ni ule wa hali na mali. Ingawa ni vigumu kujua taasisi gani tunaweza kuiamini na kupeleka mchango wetu huko, naamini tukiulizana miongoni mwetu tutapata majibu tunayoyahitaji.Tupeane habari, tubadilishane uzoefu.

Mwishoni baadhi yenu mliomba kuona kama ninazo picha zingine za shule hiyo ya Kibogwa.Picha inayoambatana na ujumbe huu ni Shule ya Msingi Kibogwa kwa nje.Double click kwenye picha uione vizuri.Picha na Mathew Membe na nimeipata kupitia kwa Yahya Charahani, mwanablog, mwandishi wa habari aliyeko Tanzania.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 3:16 PM | Permalink |


Maoni: 8


  • Tarehe: 6:55:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger mloyi

    Nilisikia JK anataka kurudisha JKT, nategemea haitakuwa kama ile tuliyoenda sisi, safari hii itakuwa jambo bora kama wakiwa wanakaa kambini kama miezi miwili mitatu wakijifunza ufundi rahisi, kama wa kukabiliana na hali tuliyoiona kwenye picha ile, kwa kutumia pembejeo?("resources") zilizopo kwenye mazingira yetu. Baada ya hapo wanatawanywa vijijini kufundisha wanavijiji ufundi waliojifunza na kusaidia kuutumia huo ufundi. Hii itakuwa silaha kubwa kuipinga hali hii, inabidi kuwe na vipaumbele vya hali zisizotakiwa. Angalia Marekani na Uingereza, Juzijuzi tulisikia mfalme mtarajiwa wa Uingereza alikuwa chile kufanya kile kinachofanana na JKT kwetu. Vilevile kidogo Bush akose muhula wa pili wa urahisi kwa sababu watu walihofia hakwenda JKT! JKT bado inahitajika lakini ipewe mwelekeo unaoeleweka.

     
  • Tarehe: 11:41:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Mloyi,
    Nakubaliana kabisa na wewe kuhusu umuhimu wa JKT.Ninavyojua ni kwamba JKT lipo ila pengine linakosa tu dira na mwelekeo kama huu unaouzungumzia ambao unaweza kusaidia sana katika kurekebisha mambo kama haya.Kikubwa ambacho vijana wanajifunza JKT ni ufundi,jambo ambalo ni muhimu kwani wao wanaweza kuwa walimu wazuri sana wa wananchi wengine.Pia jeshi linasifa ya kuhamasisha kitu ambacho kwa mtizamo wangu ndicho kinachokosekana hivi sasa.

     
  • Tarehe: 1:54:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Mija Shija Sayi

    Jeff, hakuna haja ya kutafuta taasisi ya kupeleka michango yetu, tayari tuna JUMUWATA, tufungue akaunti ya benki tupeleke huko michango yetu halafu kama kuna taasisi zinataka kusaidia nazo ziingize pesa kwenye akaunti ya Jumuiya. Hili nadhani litakuwa rahisi hata katika ufuatiliaji pia.

    Au mnasemaje?

     
  • Tarehe: 9:27:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Damija,
    Nakubaliana na wewe,JUMUWATA inaweza kuanza kubeba majukumu muhimu ya kijamii kama haya.Nadhani hii itakuwa ni kazi ambayo viongozi wapya watakaochaguliwa hawana budi kuipa kipaumbele.Tukishapata wawakilishi kutoka kanda mbalimbali ni rahisi kujua au kuelekeza wapi mtu anayetaka kusaidia anaweza kuwakilisha msaada wake uwe ni wa nguvu au mali.

     
  • Tarehe: 3:40:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Christian Bwaya

    Nakubaliana kabisa na waoz la Damija.

    Jumuiya ya wanablogu inaweza kujitanua iwafikie watu katika mambo mengine ya kijamii kwa hali na mali.

    Tusiishie mitandaoni, umefika wakati tuingie na kule kusiko na mitandao, amabko ndiko kwenye uhitaji zaidi.

    Halafu Jeff, vipi siku hizi mbona huandiki tena Tanzania Daima?

     
  • Tarehe: 3:29:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    "...Mambo ya Bongo sasa hivi kiboko; kuna mashopingi moli kama ya mtoni, maubungo plaza, meifea plaza na maplaza mengine mengi tuuu! Maapatimenti, mariili esteti broka, mabangaloo, mafaivu staa hoteli, na maskai skrepa! halafu mabarabara ya kimtoni na madaraja kama lile la Kibiti, watasha wenyewe wanabloo! Na neshino stediumu mpya ikiisha litakuwa hamna tena Afrika nzima!

    Mademu siku hizi wanang'aaaa! Kuna maMiss kata, miss tarafa, miss wilaya, miss mkoa, miss Tanzania, mpaka miss yunivasi! Mafasheni shoo, madizaina, na mamodozi! Siku hizi mademu wanakutilia mavitu ya madizaina: jojo amani, guchi, siyo mitenge ya Sunguratex sijui Urafiki. Jamani Bongo tumetoka mbali, niliwahi kuchukua bonge la demu kufika homu chupi haivuki, mpira wa chupi umekatika akafunga fundo ilibidi alifungue kwa meno! Siku hizi maselebriti kibao: wa vipaji vya kitaaluma, kisanii, kimichezo, kisiasa, ua kwa majina ya ukoo. Kuna Matamasha, mabonanza, na makonseti hatari tupu!

    Redio stesheni za kumwaga siyo kama wakati ule idhaa tatu tu; taifa, biashara na eksteno sevisi iliyokuwa inafunguliwa kwa masaa maalumu na kipindi kimoja tu cha salamu siku za Jumapili mchana! Na tivii chaneli kibao siyo kama enzi zile tivii Zanzibar minara michache mitaa ya Upanga na Ostabei tena usalama wa taifa wasiione, ukionekana mnara utakuwa umeenda kinyume na Azimio la Arusha kwa kuwa bepari au kabaila kwa sababu ya kumiliki tivii! Siku nyungo kila nyumba. Mpaka vijijini wana nyungo. Nilikuwa Ng'apa, Lindi huko nikafikiri nitaikosa mechi ya Aseno na Livapuli, mshikaji baa zote zilikuwa zinaonyesha gemu, mashabiki wa ligi ya premia kapu na yuefa wapo mpaka Umachingani huko! Eee bwana na magari mengine yaliyopo Bongo hata ughaibuni hamna: sijui mabaluni, maviieksi, mashangingi, mamuso, mahama, mafoo whili draivu, maleksuzi, yaani wee acha tu!

    Elimu nayo sasa imepanda kuna mainteneshino skuli kuanzia nasari mpaka hai skuli. Siku hizi mtoto mdogo anaongea kingreza kama mzungu! Yunivesti siyo UDSM na SUA tu kuna mayunivesti kibao sijui Nyegezi, Sijui Mikocheni, Makumira, Tumaini, na jingine la nguvu linaangushwa Dodoma unaambiwa hilo yunivesti sijui litakuwa linachukuwa wanafunzi ngapi sijui kwa wakati mmoja! Yaani hilo yunivesti litakuwa kama Kembriji, Oksfodi, au Havadi! Eee bwana eee!

    Siku hizi simu siyo big dili! Unaambiwa nilikuwa Nanjumbu, Mtwara vijijini ndani ndani huko nikakikuta kibibi kizeeee utafikiri hakikuwahi kuwa kitoto kichanga! Unajua nini? Kilikuwa na kimobiteli cha Nokia hizi ndogo ndogo kinaongea sijui na nani? Mwenyewe nilizimia! Enzi za POSTA NA SIMU ilikuwa lazima uende kibanda cha simu tena ukikikuta simu nzima una bahati vinginevyo sumni yako inaliwa na simu haifanyi kazi. Ua ukitumia simu za nyumbani siyo laini kuingiliana! Au unaweza kujikuta unasikiliza simu tano kwa wakati mmoja! Siku hizi hela yako tu: kuna bazi, seliteli, voda, mobiteli lakini mimi naiona seliteli ndiyo kiboko lakini voda nao moto! Jamaa wa posta kweli walikuwa wanatuzingua barua unaituma Kibaha toka Dar inachukuwa mwezi! Siku hizi unatuma teksi meseji au ukiona namna gani vipi unaenda intaneti unatuma imeli!

    Mabenki ya kumwaga hakuna mpango wa kupangapanga foleni tangu asubuhi mpaka jioni. Mahospitali hela yako tu. Kuna mahospitali yana vifaa kupita Muhimbili. Unapigwa eksrei huku unajicheki kwenye skrini, unafanyiwa opresheni bila kupasuliwa, maamblensi mengine mabenzi yana huduma mpaka za kuzalishia!

    Usafiri siku hizi siyo sijui ATC, UDA, sijui KAMATA, nyooo! Siku hizi mtu unataka kwenda Mwanza unapaki begi lako unaenda eyapoti unachagua pipa gani udandie Prisisheni, Igo, eyaTanzania au bomba lolote tu! Mabasi siku hizi kuna malakshari yana maeyahostesi kama wa kwenye ndege! Mabasi yana vyoo, tivii, slipingi kochi yaani kama mtoni tu! Prezidenti naye ana pipa lake mwenyewe nasikia lina bafu na jim humo humo!

    Bia na fegi za kumwaga. Siku hizi hakuna ulanguzi wa bia wala fegi. Bia unakunywa unayoipenda mwenyewe. Miye bia ninayoipenda kesto (Castle). Bia na Fegi zinakosa maketi mpaka zinafanyiwa advataizment kila mahali. Mzee mzima alitaka kuleta mpango wa kufunga mabaa mapema, kipato cha taifa kikashuka wakamwambia asitishe zoezi lake. Taratibu wakamng'oa asilitie taifa hasara bure!

    Unafiki wa kuitana NDUGU imepigwa ribiti! Mzee mzima alipoingia madarakani akaona huu unafikitu. Wewe tangu lini Mchaga na Mpogolo wakawa ndugu? Au mbunge na mesenja au waziri na nesi udugu uko wapi? Lazima tukubali watu wengine ni WAHESHIMIWA na wengine watu tu!

    Mimi ughaibuni wala sikuzimii. Jamaa wanaenda ughaibuni nasikia wakifika huko wanabeba maboksi na kukosha vizee. Nanihii alikuwa na bonge la posti akajifanya kwenda ughaibuni kufanya mastazi. Kabla hajaondondoka alikuwa kavimba: mimba hiyoo, mashavu utafikiri anapuliza moto! Hiyo mastazi imemtokea puani: karudi mimba imekatika, kakondaa utafikiri Msudani ya Kusini, miguu kama mikono ya mawani, yaani utamuonea huruma! Unajua Bongo michoro yako tu! Misheni kibao inategemeana na wewe mwenyewe jinsi unavyopanga kete zako. Hapa hapa bongo kuna watu wanakwenda huko ughaibuni kila siku utafikiri andazi na kikombe cha chai! Hapa hapa Bongo kuna majamaa wanaishi kama mtoni: asubuhi wanapata brekifasti ya masoseji, hambagi, juisi na chai ya maziwa matupu au uji uliopikwa na unga wa keki ukatiwa na mapande ya siagi na krimu! Lanchi chikeni chipsi na kuku, dina steki hevi na grili pateto au raisi! Yaani wee acha tu, Bongo New York.

    Na manjagu wanakula mavitu hevi siyo kama enzi za Mahita tangu kaja Said Mwema manjagu wanatia vitu vya kimtoni 'maksi' sijui mabelti, mapikipiki, yaani we acha tu! Bongo niu yoki. Cheki mwenyewe hapo chini!



    Ofisa na askari wa Jeshi la Polisi wakisimamia bomoabomoa ya vibanda vya wafanyabiashara iliyofanyika jana katika eneo linalozunguka jengo la DDC Kariakoo katika barabara ya Kongo, Dar es Salaam. (Picha na Richard Mwaikenda).

    Makala
    • Harakati za SHIRECU kuondokana na ukata
    • Je, kigezo cha shahada ya Chuo Kikuu ni muhimu kwa mwandishi?
    • Lifahamu zao la paprika, matumizi yake, linavyooteshwa
    • Lifahamu zao la paprika, matumizi yake, linavyooteshwa
    • Wakulima Kaskazini wanavyonufaika na mafunzo wanayopata
    • Dakika 30 zilizommaliza Mtikila
    • Mbu, baada ya malaria sasa aeneza homa ya bonde la ufa

     
  • Tarehe: 2:05:00 AM, Mtoa Maoni:- Blogger Mjengwa

    Mh! Tufanyeje?!
    Tuna lazima ya kufikiri kwa bidii.

     
  • Tarehe: 11:37:00 AM, Mtoa Maoni:- Anonymous Anonymous

    Nami nimemwandikia huyu mbunge mwenye jimbo lenye "shule" kama hii. Tunahitaji sana picha kama hizi maana zinatuonyesha kuwa tuna kila sababu za kudai utendaji bora zaidi toka kwa serikali yetu na pia ni njia nzuri ya kuwa wasemaji kwa wale wasio na sauti kama watoto wanaokwenda kwenye "shule"hii ambao watakuja kuwa walinzi wa mlangoni wa wale wanaokwenda zile shule za "ninihii" medium.

     
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker