Saturday, May 12, 2007

MAWE YA MWANZA!


Ukiambiwa uzitaje nchi ambazo zimejaliwa kuwa na mandhari nyingi tofauti na za aina yake usisite kuitaja nchi yetu ya Tanzania. Kama kuna mtu anabisha anyoshe kidole. Pichani ni mawe yaliyoko pembezoni mwa Ziwa Victoria jijini Mwanza. Hivi tukilisukuma lile jiwe pale juu litaanguka? Picha kwa hisani ya Ebby Mkandara, mkazi wa hapa Toronto aliyetembelea kanda hiyo ya ziwa hivi karibuni.

7 comments:

  1. Jeff!

    aisee hii ni bonge la picha. mpe hongera ebby. basi hapo ingenogab kungekuwa na ndama mweupe akila majani kwa pembeni, ama mbuzi akinywa maji kuleta uhai. lakini bado hiyo peke yake ni postikadi

    ReplyDelete
  2. Hujafika kwetu ukerewe bila kuona hayo mawe. Picha swafi.

    ReplyDelete
  3. Anonymous6:17:00 AM

    unanikumbusha siku moja darasani tuko watanzania,waganda na wazambia.basi mwalimu akatuuliza vivutio vya nchi zetu,ilikuwa rahisi sana kwa watanzania kujibu ila waganda na wazambia walianza kukun vichwa wajibu nini.kwa kifupi tumebalikiwa kupita kawaida.Swali:mbona hatuendelei pamoja na rasilimali zote hizi

    ReplyDelete
  4. nimeingalia tena hii picha naona kama kina cha maji kimepungua, hiyo mistari ya kwenye mawe inaonyesha maji yanarudi chini. tuombe mvua!

    ReplyDelete
  5. Watanzania tuna mengi mazuri ndani ya nchi yetu. hatuyajui, tunadhani utalii ni wa Wazungu kuja kwetu tu. Dhana ya utalii wa ndani haipo kwenye bongo zetu. Inasikitisha.

    ReplyDelete
  6. Naamini kabisa kuna kizazi kitakuja Tanzania nakushindwa kabisaa kutuelewa kwanini Tanzania inaitwa nchi masikini wakati baraka zake na utajiri wake uko nje nje namna hii!Huwa nacheka mara nyingine ni kikatiza katika baadhi ya nchi na kuona jinsi wanavyo lazimisha vivutio vyao vya asili kuwa vivutio.Lakini ipo siku

    ReplyDelete
  7. Anonymous11:05:00 PM

    Unaufahamu wimbo (au "mwimbo" kama jamaa fulani wanavyopenda kusema) wa dokta Remmy anaosema kuwa mji wa Mwanza una milima ya mawe. Maajabu fulani haya ya kijiografia.

    vipi, eneo hili halijabinafsishwa?

    ReplyDelete