Saturday, May 06, 2006

UNAWEZA KUOTEA?


Unaweza kuotea hapa ni wapi?Picha hii ni nini,kwa nani,nk?

11 comments:

  1. Kwa haraka haraka ningeotea kuwa hapo ni ofisi ama ya ubalozi wa Bongo katika Canada ama kama si ya ubalozi basi inahusika (kiofisi) na Tanzania. Lakini kwa kuwa humu ughaibuni tofauti na Bongo kumiliki bendera na kuitumia ni suala huru. Mtu unaweza kuweka bendera ya marekani nyumbani kwako na hamna maneno. Unaweza ukamvisha mbwa wako bila tabu. Kafanye vivyo bongo kama haujaulizwa kwa mkong'oto. Ndio maana pale juu nimeweka kwenye mabano "kiofisi" Basi nabashiri hapo ni nyumbani kwako.

    ReplyDelete
  2. mawili - ofisi ya konsula au nyumbani kwako

    ReplyDelete
  3. naiona bendera ya Tanzania lakini sipajui!

    ReplyDelete
  4. naiona bendera ya Tanzania lakini sipajui!

    ReplyDelete
  5. Hapa ni nyumbani kwa ofisa mmoja wa ubalozi

    ReplyDelete
  6. nyumbani pako, ewe jeff msangi. kama unabisha sema!!!

    ReplyDelete
  7. Hapa mbona ni kama nyumbani kwa balozi wa Canada vile ingekuwa Marekani ningesema kwa Balozi Daraja pale Washington

    ReplyDelete
  8. Anonymous1:05:00 PM

    nyumbani kwako. Una usongo na nchi yako kweli...ninyi ndio mnaokunywa maji ya bendera, sio?

    ReplyDelete
  9. Shukrani kwa wote mlioshiriki katika kujaribu kutegua kitendawili hiki.Baadhi yenu mlikaribia kupata jibu sahihi.Wengine mlilitaja ila bila uhakika.
    Jibu ni kwamba huo ndio ubalozi wetu wa Tanzania nchini Canada!Ni full high commission.(high commission ni mbadala wa embassy.High commission ni kwa ajili ya nchi za commonwealth pekee).
    Kwa kutazama nje unaweza kuhisi kilichomo ndani.Swali langu ni je,nguvu ya kusukuma watalii waende Tanzania tunaimalizia wenyewe huku huku?Ubalozi ndio picha halisi ya nchi husika?

    ReplyDelete
  10. Anonymous5:35:00 PM

    50 Range Rd. Ottawa,

    Ontario Kin 8J4,

    CANADA



    Tel.: +1 613 232 1500 / 1509

    Fax: +1 613 232 5184

    Telex: (021) 533569

    E-Mail: tzottawa@synapse.net

    www.tanzaniahighcommission.ca
    Utanikataa hapo

    ReplyDelete