Friday, February 23, 2007

Ukitaka kufurahi kila jumamosii
Njoo uburudike na wana sikinde oyee.


Hicho ni kionjo cha muziki wa wanasikinde enzi hizo wakitukumbusha kwamba wikiendi ni mwendo wa kuburudika kwa dansi na nyama choma na fanta(au bia?). Lakini ukiwa ughaibuni nyama choma ni kwa msimu au la ujichomee mwenyewe ndani ya nyumba yako huku ukijiandaa kuifukiza nyumba yako yote kwa moshi.Nje hapakaliki kwa baridi nyakati kama hizi na ndio maana nyama choma zinakuwa kwa msimu. Sasa ufanye nini? Kwanini usimsikilize Bob Marley akiongelea masuala kuhusu urasta,ganja,vyombo vya habari,siasa ndani ya muziki nk kama alivyohojiwa huko New Zealand mwaka 1979?

4 comments:

  1. Anonymous12:52:00 PM

    Jeff,
    huwa sichoki kumtazama na kumsikiliza Bob. Ananifurahisha pale anaposhangaa msimamo wa serikali juu ya bangi ambayo anaiita "herb" (mtishamba). Anasema, "herb is a plant" kisha anauliza kwanini watu wanaodai kutenda mema ("who calls themselves government and this and that...") wanataka kukataza watu kutumia hii dawa.

    ReplyDelete
  2. Ndesanjo,
    Wewe ni kama mimi.Huwa napenda sana kusikiliza mahojiano yoyote aliyowahi kuyafanya Bob popote pale kwa sababu kila mara nimsikilizapo huwa najifunza kitu fulani.

    ReplyDelete
  3. Hapa umenikumbusha mbali Jeff! Asante sana.
    /Maggid

    ReplyDelete
  4. amenifurahisha alipojibu kuwa rasta ni wewe moyoni na sio nywele ama nini.

    jeff umetupeleka mbali kweli. natfuta mahojiano aliyofanya bruce lee akiongelea sanaa ya kujilinda kwa mkono mtupu (karate) na mambo mengine.

    kama ujuavyo bruce lee alikuwa masiha wa karate na bob wa reggae na urasta. hivyo kama alivyosema ndesanjo kila neno lao linahesabika kama somo

    ReplyDelete