Sunday, April 15, 2007

USHINDANI NI MKUBWA,TUJIZATITI



Wiki kadhaa zilizopita rafiki yangu Metty wa Metty'z Reflections-Tanzania in Focus (Metty yeye hublog kwa kiingereza zaidi) aliandika waraka mfupi lakini mzito na akaupa kichwa cha habari Brand Tanzania:Please Do More. Alichokuwa akikiongelea Metty ni ulazima wa wizara na idara zetu zinazohusika na masuala ya utalii kufanya zaidi katika kuhakikisha kwamba utalii unazidi kustawi ili kuliongezea taifa pato la kigeni,ajira kwa wananchi wake nk.Niliupenda waraka wa Metty kwa sababu kimsingi ulijaa ukweli.

S
iku chache zilizopita nilipotembelea miji ya kusini mwa Marekani,hususani Tampa Bay,Florida nilikumbuka sana alichokiandika Metty.Miji mingi ya kusini mwa Marekani inalelewa na biashara ya utalii.Serikali za miji ile inajua thamani ya utalii na hivyo huhakikisha kwamba ukitembelea mara moja utatamani kurudi tena na tena. Nilipotembelea Busch
Gardens-Africa
(tafadhali tembelea hii tovuti yao ili uelewe zaidi ninachokiongelea), na kwa kuzingatia kwamba sijapata fursa ya kuziona mbuga halisi za wanyama kwa miaka kadhaa sasa,nilijihisi nimerudi nyumbani. Kuanzia vibanda vya wamasai, landrover za mbugani kama hiyo hapo pichani,(zilikuwepo landrover zenye plate number TZ NYANI,FISI,TEMBO nk) treni linalokatiza mbugani, mito,mabonde,majani kibichi nk ni vitu ambavyo vitakukumbusha mbali.Ukiingia humo ndani utaona karibuni kila aina ya mnyama unayemjua.Kwa ufupi zile mbuga zetu maarufu za Afrika Mashariki zote zimewekwa pale.Ukiona mto Congo waliotengeneza hawa jamaa utashikwa na butwaa.

I
ngawa kuna tofauti kubwa kati ya kuona kundi kubwa la twiga au wanyama wengine kule Manyara au Tsavo nk, kwa wenzetu wengi wa magharibi hii ni tosha kabisa.Pasipokuwa na kampeni imara za kutangaza utalii wetu ni wazi kabisa kwamba wengi wa watu hawa ambao tulitegemea ndio wawe watalii wa kesho na keshokutwa tutakuwa tumewakosa.Atakuwa na sababu gani ya kutembelea mbuga zetu endapo anaweza kuwaona wanyama hao nchini kwake au nchi jirani na kwake? Hapo hatujaangalia adha zingine kama malaria, ukosefu wa umeme, na sasa tishio la rift valley nk.Ni lazima wizara zetu zitambue kwamba zinakabiliwa na ushindani wa aina yake na wa hali ya juu sana.Ni muhimu tukajifunza kuzinadi nchi zetu,utalii wetu kuendana na karne hii mpya ya utandawazi. Kazi ipo mbele yetu.

4 comments:

  1. Anonymous12:47:00 PM

    Jeff,
    Picha zako ni nzuri sana bro.Kama hujali ningekushauri uiangalie sanaa hiyo pia.You are a great photographer.

    ReplyDelete
  2. Ni muhimu sana kwa Tanzania kujitangaza.Lakini pia huduma inabidi ziboreshwe. Naamini kitu cha asili mara zote kinamvuto na starehe ya pekee. Hivyo ni swala tu la kuvalia hili swala njuga.

    Pia naungana na anoni hapo juu, picha zako Jeff nzuri sana.

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha, sisi tuna serengeti asilia, mwingine anatengeneza serengeti feki halafu anapata mapato mengi kuliko sisi. Sijui hawa jamaa wana uchawi au ndiyo mtu kwao, kama huna hata kwa kaka yako ni kwenu!
    Waambie siku hizi hatuna yena Ma-TZ tuna T 234 ADG na nyingine.
    Vilevile wakaribishe tena huku wajifunze vizuri.

    ReplyDelete
  4. Anonymous1:08:00 PM

    @Anony,
    Asante kwa ushauri.Ninauzingatia
    @Simon,
    Umuhimu wa kujitangaza ndio suala muhimu ambalo nchi yetu nadhani inalipuuzia.Asante kwa kuzipenda picha,inanitia moyo kwa sababu naipenda sana sanaa ya picha.

    @Mloyi,
    Umenena kweli.Nikienda tena nitawakumbusha kwamba nambari zetu siku hizi ni digitali.

    ReplyDelete