Saturday, August 04, 2007

MBIO DHIDI YA UBAGUZI

Ubaguzi wa aina mbalimbali ni changamoto ya kila siku miongoni mwetu kama wanadamu.Kimsingi kila mtu ni mbaguzi.Unabisha? Unajidanganya.Tofauti inakuja kwenye ni jinsi gani unavumilia wengine.Ubaguzi sio tu wa rangi bali mambo mengine chungu mbovu. Ubaguzi wa rangi ndio ambao dunia inauzungumzia zaidi kutokana pengine na historia ya dunia yetu yakiwemo mambo kama ukoloni,biashara ya utumwa nk. Kuna wakati nimewahi kuuliza kundi la vijana kuhusu wao wanambagua nani na kwanini.Majibu ya vijana hao yalinifanya nianze rasmi kuwa mshiriki kila mwaka katika mbio dhidi ya ubaguzi wa rangi (Race Against Racism) hapa Canada.Picha unayoiona niliipiga mwezi wa saba mwaka huu wakati wa mbio hizo zilipofanyikia katika jiji la Brampton,Ontario.Je wewe unambagua nani na kwanini?




No comments:

Post a Comment