VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Tuesday, January 30, 2007
MSOME MAKENE NA WARAKA WAKE KWA JK!
Uandishi wa habari wa Tanzania mara nyingi umekuwa ukibezwa kwa kuwa wa "kioga".Uandishi wa habari kama mhimili muhimu katika maendeleo ya taifa imekuwa ni kama njozi isiyoisha kiasi kwamba tofauti kati ya ndoto na ukweli imekuwa ngumu kutambulika.Dhihaka hizo ndizo zilizomfanya mchora katuni,mtanzania anayeishi Kenya kuibua mjadala wa aina yake alipoakisi kwamba waandishi wa habari wa Tanzania "wanalamba" viatu vya mheshimiwa raisi. Mjadala mkali sana ulizuka lakini mwisho wa siku mwenye masikio alisikia na mwenye macho aliona.

Boniface Makene,mwanablogu wa siku nyingi,rafiki yangu,siku zote amekuwa akipiga vita suala la kuandika "porojo" huku zikisindikizwa na woga.Ukimsoma Makene kwa makini utagundua kwamba anapenda kutumia kalamu yake ya uandishi kama silaha halisia katika kuelimisha,kukosoa na kuelekeza na pia hata kuburudisha inapobidi. Leo Makene amemuandikia raisi waraka mzito,wenye tungo makini.Tafadhali usome waraka huo kisha fungua mabano.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 1:22 PM | Permalink | Maoni 2
Wednesday, January 24, 2007
UNAWEZA CHEZA JUU YA BARAFU?

Sifa moja kubwa nchi ya Canada iliyonayo ni kwamba ni nchi yenye baridi sana.Watu wengi wanaoishi jirani na Canada (Marekani) huwa hawataki kuitembelea Canada kwa sababu wameshasikia kwamba kuna baridi kupita mfano. Lakini ukweli ni kwamba Canada sio nchi yenye baridi kushinda zote ulimwenguni.Maeneo mengi ya Canada hususani kusini mwa Canada yana viwango vya baridi karibuni sawa tu na miji mingi ya Marekani.Mahali ambapo pana baridi kushinda sehemu zote duniani ni mahali panapojulikana kama Vostok (kituo cha utafiti cha warusi) na pia Plateau Station huko Antarctica. Olymyakon,Russia pia pana baridi kuliko Snag,Yukon kaskazini mwa Canada ambapo ndipo panapoifanya Canada ikimbiwe na wasiopenda baridi. Kiwango cha baridi cha chini kabisa ambacho kimewahi kurekodiwa huko Snag,Yukon ni Fahrenheit -81.4.

Kama ambavyo picha ya juu inaonyesha,sio kila mtu anayachukia majira ya baridi kali.Wapo wanaofurahia. Tatizo kubwa linakuja kwetu sisi wakuja ambao michezo ya kwenye barafu sio yetu na tunaiogopa kama ukoma (kuvunjika kiuno ukiwa mtu mzima sio mchezo). Hapo ni katikati ya jiji la Toronto ambapo kila mmoja anakaribishwa kufurahi na familia yake kwa michezo ya barafu. Tujifunze?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:42 PM | Permalink | Maoni 3
Wednesday, January 17, 2007
TOVUTI YA "UHURU"....MMMH!


Waingereza wanao msemo usemao "Beauty is in the eyes of the beholder".Maana halisi ya msemo huo ni ukweli usiopingika.Lakini pia kuna wakati umma mzima unaweza kukubaliana kwamba kitu au jambo fulani sio kizuri. Upo hata wakati binadamu fulani fulani hukubali kwamba wao ni "wabaya" aidha wa sura au roho. Nadhani unakumbuka kwamba Tanzania iliwahi kuandika historia kwa kuwa na mashindano ya "watu wabaya".Kama ilivyotegemewa wanaume ndio waliojitokeza. Mpaka leo hii sijawahi kukutana na mwanamke aliyekiri kwamba yeye ni "mbaya".Natumaini ushawahi pia kusikia mtu akijitapa kwamba yeye ana roho "mbaya".Watu wengi walishikwa na mshangao pindi shindano lile la aina yake la Tanzania lilipotangazwa.

Mshangao haukuishia kwenye kujitokeza kwa wingi kwa washiriki wa shindano la kumtafuta mtu mbaya kupita wote bali lilinoga pale baadhi ya washiriki walipopinga matokeo. Walisema ah yule aliyeshinda bwana kapendelewa,mimi ndio mtu mbaya kushinda wote!Yule mzuri kabisa. Bado sijasahau jinsi ambavyo mshindi wa shindano lile la "mtu mbaya" kushinda wote (nakumbuka aliitwa Masoud kama sikosei) alipoanza kufuatwa fuatwa na vimwana wa kila aina wakitaka penzi lake(au hela zake?) Kama wote tulikubaliana na uamuzi wa majaji kwamba Masoud alikuwa ni mbaya kuliko washiriki wengine kama Mzee Jangala,Remmy Ongala na wengineo inatokana na msemo wa hapo juu kwamba beauty is in the eyes of the beholder.

Tukiachana na uzuri au ubaya wa wanadamu(wengine wanasema ni dhambi kukosoa kazi ya mungu), siku hizi si ajabu ushasikia zawadi zikitolewa kwa tovuti bora za mwaka katika nyanja mbalimbali. Best designed websites huwa ni mojawapo ya kipengele ninachokipenda sana. Hivi karibuni nimesikia kwamba kuna tuzo zinaandaliwa kwa ajili ya tovuti (sio blogs ingawa kiufundi blogs ni tovuti) mbalimbali za kitanzania.Keti chini usubiri.

Wakati maandalizi yanaendelea naomba leo niseme wazi kwamba,kwa mtizamo wangu, tovuti ya gazeti la uhuru la Tanzania,mojawapo ya magazeti makongwe kabisa nchini Tanzania inanipa kizunguzungu na kwa kiasi kikubwa inanipa simanzi nikizingatia kwamba Uhuru ni gazeti linalomilikiwa na Chama Tawala.(mbona hii kidogo inavutia?) Kwa rasilimali walizonazo, jamaa wa uhuru wanaweza kabisa kuwa na kitu bora.Hivi ni nani mkarabati wa tovuti hii? Tafadhali, itengenezeni jamani.Tunataka tusome sera na ajenda zenu(hata kama zimejaa longolongo za kisiasa) bila kupata maumivu kama ilivyo hivi sasa.Unasemaje msomaji?

Pichani juu ni mimi kutokana na e-mail moja niliyowahi kutumiwa,nikaambiwa nitizame moja kwa moja kwenye monitor yangu kisha nitabasamu ili nipigwe picha.Nilifuata maelekezo na matokeo yake ndio kama hayo hapo juu,nikageuka kuwa mzungu!
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 12:02 PM | Permalink | Maoni 3
Monday, January 15, 2007
MGOGORO WA DARFUR-TUMLAUMU NANI?

Bara letu la Afrika limeshuhudia majanga makubwa kila mara. Imefikia mahali kila janga,hangaiko la binadamu na mengineyo yamepewa sura ya "Afrika". Bara letu limekuwa ndio kisima na kiini cha kila aina ya uharamia. Haikunishangaza wakati Katrina ilipogonga kuta za New Orleans kule Marekani na serikali ya Marekani kushindwa kuwahudumia wananchi wake, walalamikaji walisikika wakisema "ah, itakuwaje jamani,hapa sio Afrika bwana,ni Marekani"!Maneno yale yalimaanisha pengine ni sawa kwa majanga kama haya kutokea huko Afrika na sio kwingineko.Ingawa janga la Tsunami lilifika pia Afrika, kuua watu na pia kuharibu mali nk hakuna aliyetaka kusikiliza wala kuwasaidia walioathirika. Lakini unakumbuka nguvu iliyopelekwa huko Banda Acheh?Unadhani ni kwanini?

Mifano ya migogoro ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo imewahi kulikumba bara letu la Afrika na bado inalikumba ipo mingi na ina sababu nyingi.Wanazuoni,wanahistoria,wachumi,walimu,wanafunzi na wengi wanaohusika wanayo maswali na majibu kedekede kuhusu kwanini Afrika,kwanini sisi?Majibu mengi huzua maswali zaidi.

Mgogoro wa Darfur ni mfano hai wa migogoro mingi iliyopo barani mwetu. Mgogoro huu wa Darfur ambao eti kiini chake ni ubaguzi, ungali unaendelea,ungali unakatisha maisha ya maelfu na ni mfano mzuri wa jinsi gani sisi waafrika tunavyojiweka katika ramani ya ulimwengu. Ni nani alaumiwe kuhusiana na mgogoro wa Darfur? Jibu rahisi ni kwamba viongozi wetu na wengineo wenye uchu wa madaraka. Hawa ndio wanavipa faida viwanda vya silaha vya magharibi na kutoka nchi za Asia kama China,Japan nk.Viongozi wetu ndio wanaotia sahihi mikataba ya silaha za maangamizi badala ya kutia sahihi masuala ya kiuchumi na maendeleo.

Ni kwanini viongozi wetu hawajiulizi maswali kama nini mchango wa nchi kama Uchina katika migogoro yetu barani Afrika? Viongozi wetu wanapoikumbatia China kama mwambata mkuu wa biashara wanajua wanafanya nini? Hivi ni kwanini hakuna anayesema wazi kwamba China ilikuwa na mchango mkubwa sana katika mauaji ya halaiki ya Rwanda kwasababu mapanga yaliyotumika yalikuwa yametengenezwa Uchina? Endapo China ingeuliza mapanga yote haya ya nini na kusitisha "order" ile nini kingetokea? Ni nani anayeuzia silaha wanamgambo wa janjaweed? Kwanini huyo asiwe ni adui yetu mkubwa? Nini viongozi wetu wa bara la Afrika wanafanya ili kutokomeza vita visivyokwisha barani Afrika?

Kimsingi, siamini kama kuna kitu kinachoitwa jamii ya kimataifa.Kilichopo ni mataifa yanayoshindana ulimwenguni. Marekani, China,Japan, Canada,Uingereza, Urusi,Italy nk si washirika wa chochote bali washindani. Sasa kama wao kwa wao wanashindana,inakuwaje viongozi wetu wanadhani au kuhadaika kwamba baadhi ya nchi nilizozitaja hapo juu na nyinginezo nyingi ni marafiki zetu? Kwanini wasitazame kwa makini historia? Nani washauri wao?

Viongozi wetu wa Afrika lazima watambue hilo na kuunda jamii yao wenyewe ambayo itaongozwa na kulindwa na wao wenyewe wakishirikiana na wananchi(sisi). Lazima pawe na nia ya pamoja ya kukomesha mauaji holela na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu tunaoushuhudia hivi leo. Lazima tujilaumu sisi wenyewe kwanza.Lazima tukasirike na kuamua kutokuwa wanyonge na masoko ya silaha holela,madawa ya kulevya,madawa yasiyokuwa na viwango na mengineyo.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:36 PM | Permalink | Maoni 6
Friday, January 12, 2007
KITABU CHA BLOG NA TAJIRI MTOTO

Rafiki yangu mmoja amenipa zawadi ya kitabu kilichoko kwenye picha hapo juu.Kama kinavyoonekana kinaitwa The Rough Guide to Blogging mwandishi akiwa jamaa anayeitwa Jonathan Yang.Kitabu kipo kwenye mfululizo wa vitabu vya jamaa wa rough guides.

Kwa mtazamo wangu, kama unataka kuzidisha maarifa yako juu ya kublog basi sio wazo baya kama katika hema za vitabu vyako hiki nacho kitakuwa kimojawapo. Naendelea kukisoma na kujifunza mambo lukuki.Kitabu kinapatikana katika maduka mengi ya vitabu yakiwemo yale ya mtandaoni kama Amazon.

Wakati huo huo: Hivi ukizaliwa kwenye familia yenye hali duni kiuchumi inamaanisha na wewe utadumu kuwa duni na kisha kuiaga dunia ukiwa masikini? Yaani utaendeleza historia ya umasikini?Inawezekanaje basi kukata "mzizi wa fitina"? Hebu fuatilia maisha ya Dr.Farrah Gray,bwana mdogo ambaye aliukwaa umilionea akiwa na umri wa miaka 14 tu akiwa anatokea kwenye familia masikini huko kusini mwa jimbo la Illinois nchini Marekani. Fungua tovuti yake na kisha ukurasa wake wa wiki kisha usikate tamaa,inawezekana.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 7:47 PM | Permalink | Maoni 1
Friday, January 05, 2007
MATEMBEZI KATIKA JIJI LA KARNE!


Naomba nianze kwa kukutakia kheri ya mwaka mpya. Kwa takribani wiki tatu nilijaribu kukaa mbali na mtandao ili kupumzisha akili,kutafakari yaliyojiri mwaka tulioupa kisogo hivi majuzi na kupanga mikakati mipya ya 2007 kama ikibidi. Tofauti na miaka iliyopita, mwaka huu sijaweka malengo maalumu.Nataka uwe mwaka shaghalabaghala kama itawezekana.Wewe unasemaje? Lakini jambo moja ambalo nipende nisipende tayari lipo kwenye malengo
na ajenda za mwaka huu ni suala la
kuendelea kublog.


Wakati wa kufunga mwaka nilitembelea kwa Joji Kichaka kama ambavyo Ndesanjo hupenda kumuita. Katika pita pita zangu nilitembelea mojawapo ya ile "miji shoka" ambayo mingi imegeuka kuwa namna ilivyo baada ya kuhamwa na watu weupe. Historia ndio inayosema hivyo,sio mimi.Kuhamwa huko kulipewa jina "white flight" ikimaanisha wazungu kuhama na kuwaacha weusi waendelee kukaa wenyewe katika miji yao.Kilichochangia sana ni ubaguzi wa rangi ambao mpaka hivi leo ungali upo na pengine utaendelea kuwepo milele.Wachumi wanasema sababu za kiuchumi ndio zilizochangia "white flight".


Jiji la
Gary(mpaka hivi sasa sielewi nini kinasababisha sehemu moja kuitwa jiji na nyingine kuitwa mji au kijiji) lipo katika jimbo la Indiana mpakani kabisa na jimbo la Illinois lenye jiji maarufu la Chicago ambapo mwanamama Oprah Winfrey huendesha shughuli zake. Nia yangu ya kutembelea Gary,Indiana ilikuwa kuanzisha kasumba ya kutembelea kule wanakoishi "wenzetu" na kuachana na kasumba ya kutembelea majiji makubwa peke yake( yale ambayo wenyewe hupenda kuyaonyesha kwenye sinema zao na kurubuni wengi duniani kwamba Marekani ndivyo inavyomeremeta).Pia nilitaka kuona mahali mwanamuziki maarufu wa muziki wa pop Michael Jackson na ndugu zake kina Janet Jackson,Tito Jackson,LaToya Jackson, Marlon Jackson,Randy Jackson,Jackie Jackson na Rebbie Jackson walizaliwa na kuanzia maisha yao ya uanamuziki.

Pichani juu ni nyumba walimozaliwa nyota hao wa muziki ambapo baadaye kaka yao Michael Jackson alikuja kuwa na umaarufu wa aina yake wenye mchanganyiko wa mambo chungu tele. Tofauti na nyumba zingine zilizopo katika jiji la Gary nyumba walimozaliwa nyota hao wa muziki inaonekana kuwa safi,inayotunzwa na ina hata majani ya kupandikiza. Sababu ni kwamba familia ya wanamuziki hao imeamua kuitunza nyumba hiyo kwa ajili ya kumbukumbu (souvenir ) kama ilivyokuwa enzi hizo.Hivi sasa kuna mpangaji anayeishi humo.Nyumba hiyo iko katika kijimtaa kidogo ambacho kwa heshima ya familia ya Jacksons nacho kinaitwa Jackson Street. Mwaka uliopita(2006) jiji la Gary lilitimiza miaka 100 na hivyo kuchukua jina la jiji la karne!


Jambo ambalo litakushtua ukifika Gary,Indiana ni hali ya maisha,uchakavu wa majengo,vichaka,uchafu na kila aina ya takataka za dunia hii. Picha ya pili hapo juu ni mfano wa nyumba nyingi nilizoziona. Nyumba hiyo ni makazi ya mtu ndani ya Marekani.Ilikuwa vigumu kwangu kuamini kwamba hii ndio Marekani ambayo inatumia mabilioni ya dola kupigana vita inavyojua kabisa kwamba kamwe haitaweza kuvimaliza bila kurekebisha sera muhimu za ndani na nje.Hii ndio nchi ambayo viongozi wake wanajifanya hawaoni umasikini na uharamia unaojiri nyumbani na hivyo kuyafumbia kabisa macho masuala hayo.Nilichokiona mimi ni kama uwanja wa vita au jamii ambayo imehamwa baada ya mapigano ya muda mrefu. Hapana,nilikuwa nimekosea; hapo ni Gary,Indiana jiji lenye wakazi zaidi ya laki moja na nusu. Damu ilikuwa inasisimka huku vinyweleo vikisimama kila mara.Au ni uoga wangu tu?


Kama nilivyoeleza hapo juu,jiji la Gary ni mojawapo ya majiji mengi ya Marekani ambayo yalikumbwa na "white flight", mengine ni kama vile Philadelphia, Atlanta, Houston, Miami, Cleveland, Boston, Detroit, Memphis, St.Loius, Milwaukee, New Orleans(Katrina), Magharibi na Kusini mwa jiji la Chicago, maeneo kama Bronx, Oueens(Coming to America), Brooklyn na kwingineko. Kitakwimu (wakati mwingine sipendi kuziamini) miji kama hiyo niliyoitaja hapo juu inaongoza kwa kuwa na ghasia,mauaji na gharika chungu mbovu za kijamii. Kwanini ni swali gumu kujiuliza lakini muhimu. Hivi sisi weusi hatuwezi bila wazungu? Nini kilitokea katika historia ya binadamu,historia yetu? Kuna mkono wa mtu?


Mwishoni swali la kwamba kwanini Marekani haisaidii wananchi wake kama hawa wa Gary,Indiana jiji ambalo kila mara limo kwenye orodha ya miji hatari kupita yote nchini Marekani, inahangaika kuihadaa dunia kwamba inapeleka maendeleo na demokrasia duniani? Hivi ni kweli kwamba zipo Marekani mbili tofauti kabisa ndani ya Marekani tunayoijua sisi?Tuendelee kublog,2007 ndio hiyo.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 2:46 PM | Permalink | Maoni 15
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker