VIJIMAMBOZ PROUD AFRICAN KASRI LA MWANAZUO BONGOCELEBRITY NKYA MAWAZO NA MAWAIDHA JIKOMBOE MIRUKO NDABULI SHAMIM ZEZE DAMIJA MATERU MLOYI CHEMI CHE MPONDA BAKANJA MTAFITI LUKWARO MSANGI MDOGO MARK MSAKI DIRA YANGU MWAIPOPO KONA YANGU FURAHIA MAISHA YAKO DAMIJA MICHUZI FATHER KIDEVU MWANDANI NGURUMO FATMA KARAMA ZAINAB OMEGA NGOLE YAHYA CHARAHANI JARIDA LA UGHAIBUNI NYEMBO BWAYA BHALEZEE JUNGU KUU WATOTO WETU BLG BROTHER SAA YA UKOMBOZI NURU AKILINI TAFAKARI ZA MAISHA ALBERT WILSON UCHUMI MIDRAJI IBRAHIM Lucassano CHESI HAKI NGOWI KISIWA CHA AMANI Innocent Kahwa SULTAN TAMBA SIMON KITURURU MAVIZO MUSA NGARANGO KIJIWENI(NED) WATANZANIA JADOUNG METTY MAGGID MJENGWA SAHARAN VIBE MWENYE MACHO ABDALLAH MRISHO MYAFRICA SHERIA NA MAVAZI
NEW VISION UGANDA MONITOR UGANDA KENYAN NATION MEDIA EASTANDARD FROM AFRICA BUSINESS WEEK ALL AFRICA
MAGAZETI YA IPP UHURU NA MZALENDO BUSINESS TIMES DAILY NEWS TANZANIA DAIMA MWANANCHI BUNGE LA TANZANIA SERIKALI YA TANZANIA IPS INTERNATIONAL
AFRIKA HURU NINI KILITOKEA PAMBAZUKA DUNIA YETU GADO CARTOONS
SEND ME AN E-MAIL
Sunday, May 27, 2007
KOMBE LA DUNIA U-20

Kuanzia tarehe 1 Julai mwaka huu mashindano ya kombe la dunia la soka kwa vijana walio na umri chini ya miaka 20 yatakuwa yanafanyika. Mwaka huu mashindano hayo yanafanyikia hapa Canada na Toronto ukiwa ndio mji utakaokuwa na mchezo wa kufungua mashindano na pia kufungia(fainali). Afrika inawakilishwa na timu nne ambazo ni Zambia, Congo, Gambia na Nigeria.Jumla ya timu zinazoshiriki ni 24.

Kwa vyovyote vile mashindano haya hayana ushabiki kama yale ya kombe la dunia la wakubwa yaliyofanyika Ujerumani mwaka jana. Lakini kwa washabiki wa soka hapa Canada hii ni nafasi muhimu na ya kipekee katika kujaribu kuukuza mchezo wa soka ambao hauna umaarufu sana hapa ingawa jumuia ya mataifa ya Ulaya na Amerika ya kusini, walio wanazi wa kutupwa wa soka yamejaa hapa. Kuna jumuia kubwa sana wa wareno,wabrazili,wanigeria,waghana,wamexico,waargentina na watu wa kila aina. Inasemekana ni kwa sababu hakuna anayeweka pesa zake kwenye soka.Tusubiri tuone itakuwaje baada ya mashindano haya na pia David Beckham kuhamia huku ambapo atacheza katika ligi ya Marekani (MLS) ambayo Toronto FC wanashiriki pia. Mchezo wake wa kwanza hapa Marekani ya kaskazini unatarajiwa kuwa hapa Canada timu yake mpya ya Los Angeles Galaxy itakapopambana na Toronto FC.

Bwana mdogo Freddy Adu,mzaliwa wa huko Tema nchini Ghana ambaye sasa ni raia wa Marekani ndio anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa cha mashindano hayo.Yeye ndio kapteni wa timu ya USA.

Pichani juu ni uwanja wa BMO Field uliopo Exhibition Place.Uwanja huu ndio utakaokuwa na mechi ya ufunguzi na fainali.Unauwezo wa kuwaweka vitini mashabiki 20,000.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 8:37 PM | Permalink | Maoni 4
Thursday, May 24, 2007
NIMEUPENDA UANDISHI HUU
Siku zote tunajua kwamba nchi yetu inatafunwa na wachache wanaojiita "wajanja".Wengi wetu hatuwezi kusema kwamba eti hatujui wakati kila dalili zipo wazi na wanaoitafuna hujitapa hata wakiwa baa, wakiwa kwenye simu za viganjani hata kwenye daladala.Wanaokula nao wanataka pia kuonekana na wao ni watu wa daraja fulani.Kwa hawa nao tambo ni zile zile...Chukua Chako Mapema.

Tunachokuwa hatukijui na ambacho vyombo vyetu vya habari vinakuwa "bubu" kutuambia ni jinsi gani nchi inaliwa na nani hasa anahusika,akitumia vipi madaraka yake. Hakuna jambo zuri kama kumjua adui yako,silaha alizonazo,mafunzo aliyonayo, mbinu anazozitumia nk.Hawa ndio wale wanaotaka tuamini kwamba "tupo pamoja" na kwamba umasikini wa nchi yetu ni "mipango ya mungu" na hakuna tunaloweza kulifanya. Mipango ya mungu haina makosa!

Mwandishi mmoja wa gazeti la ThisDay katika toleo lake la leo Alhamisi tarehe 24,2007 ameonyesha njia inayoweza kutumika katika 'kuwatambua". Pengine umeshamsoma kwani habari hii imetapakaa kote mtandaoni hivi leo.Nilichotaka kusema ni kwamba nimependa uandishi huu.Tuendelee,tutawajua.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 5:38 PM | Permalink | Maoni 3
Monday, May 21, 2007
UTALII UGHAIBUNI!

Pichani ni landrover niliyoikuta huko Busch Gardens-Africa,Tampa Bay,Florida mwezi wa nne mwaka huu. Ni mwendelezo wa nilichoandika kuhusu utalii na kwanini serikali zetu hazina budi kuvuja soksi.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:20 AM | Permalink | Maoni 4
Friday, May 18, 2007
UKIWAZA KUHUSU UGHAIBUNI UNAPATA TASWIRA GANI?

Nilipokuwa mtoto na hata mwanzoni mwa ujana wangu, nilipokuwa nikisikia kuhusu majiji maarufu duniani kama vile Toronto,New York,Paris,London nk taswira iliyokuwa inanijia kichwani ilikuwa ni majumba marefu yenye gorofa nyingi,bustani za maua zinazovutia sana, wasichana warembo,wavulana watanashati wenye tabasamu zisizoisha kwenye nyuso zao nk. Kwa ujumla nilikuwa nikipata picha ya paradiso ya duniani. Ni kivipi nisipate taswira za namna hiyo wakati maisha ya ughaibuni yalikuwa yakiletwa kwenye mboni za macho yangu na kisha kutuama kwenye ubongo wangu kupitia sinema za Hollywood na vyombo vya habari vya magharibi ambavyo vilikuwa vimeapa (sijui siku hizi) kwamba havitoonyesha kitu kibaya hata kimoja kutoka magharibi?

Kwa bahati nzuri au mbaya, mpaka leo hii, wapo watu wanaoiwazia dunia ya magharibi kwa taswira ile ile niliyokuwa nayo mimi enzi hizo. Siwezi kuwalaumu hata kidogo.Wa magharibi bado wanataka tuamini kwamba kwao mambo ni mswano tu. Kwa makusudi au bahati mbaya wanaficha kila lao lenye doa hata chembe tu.Wanasema Image Is Everything. Lakini kweli???Picha unazoziona ni kutoka mojawapo ya mitaa maarufu hapa jiji Toronto. Ni karibu kabisa na soko maarufu la Kesington. Najua ningesema tuotee hapo ni wapi majibu ambayo ningeyapata yangeweza nikatisha tamaa. Je hii ndio picha ya unayoipata ukijaribu kupiga picha za jiji la Toronto kichwani kwako? Enzi hizo je?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 6:25 PM | Permalink | Maoni 6
Thursday, May 17, 2007
UKISAFIRI UJIANDAE!

Pichani ni basi lijulikanalo kama Executive linalofanya safari zake kati ya majiji ya Dar-es-salaam na Mwanza. Hapo lilikuwa limeharibika.Ndio maana unashauriwa kwamba ukitaka kusafiri ni lazima ujiandae huku ukikumbuka kwamba msafiri kafiri. Picha na Ebby Mkandara, mkazi mwenyeji wa Toronto, aliyekuwa mmojawapo wa abiria walioonja joto ya jiwe na raha za aina zake za Bongo hivi karibuni.Hapo ilikuwa ni Singida. Nasikia ukitaka kufika kaskazini mwa Tanzania vizuri ni vyema ukachukua njia ya kupitia Kenya. Hivi ni kwanini?Kodi zinafanya kazi gani?Suti na safari?
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 5:46 PM | Permalink | Maoni 2
Wednesday, May 16, 2007
UMEWAHI KUSIKIA KUHUSU KITU NETIZENS?

Raia wa nchi fulani kwa kiingereza anaitwa citizen. Jambo ambalo pengine hujalisikia bado ni “uraia wa kwenye mtandao” au netizen kama ambavyo tunajulikana. Netizen ni uraia wa aina yake kwa sababu ni wa kimataifa, hauna mipaka.

Hati au mkataba maalumu wa netizenship unawataka raia wake kufanya yafuatayo:

1)Kwa kujitolea, kuiendeleza dunia ya mtandaoni kwa iendelee kuwa sehemu ya wazi na yenye mantiki kwa kila mmoja kujivunia na kufurahia.

2)Kuheshimu na kuzilinda haki za binadamu na faragha ya watu wengine na kuziheshimu kama vile ni za kwako binafsi.

3)Kuheshimu kazi za wengine na hivyo kutovuruga uhuru kamili wa habari.

4)Kuzilinda habari binafsi za watu wengine kama unavyolinda za kwako.

5)Kutotumia lugha chafu na zisizopendeza.

6)Kutokutengeneza au kusambaza habari zisizo sahihi.

7)Kutojihusisha na biashara haramu za mitandaoni.

8) Kutotumia majina ya uongo.

Hayo ni baadhi tu ya majukumu ya uraia mwema wa mtandaoni. Nadhani jumuia yetu ya wanablogu wa Tanzania ambao hivi sasa kampeni ya kutafuta viongozi wake zimeshaanza, inaweza ikazitumia baadhi ya kanuni hizo za uraia mwema wa mtandaoni katika kuandika katiba ya kutuongoza.

Chanzo cha mikataba ya kibinadamu kama hii imesukumwa zaidi na ukweli kwamba mtandao unachangia sana kuharibu maisha ya watoto.Wapo watu wazima chungu mbovu ambao kazi yao ni kutafuta watoto wadogo mitandaoni,kuwarubuni,kuwafanya kitu mbaya na hata kuwaua.Inawezekana kirahisi kwani mtandaoni mtu anaweza kujiandikisha kwa kudanganya kila kitu.Babu wa miaka 90 anaweza kujiandikisha kama mtoto wa miaka 10 nk. Nchi zinazoendelea kama Tanzania yetu ni lazima nazo ziamke mapema inavyowezekana katika kuwalinda watoto wa nchi. Tembelea tovuti ya cybertipline uone jinsi wenzetu wanavyojitahidi.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 5:45 PM | Permalink | Maoni 1
Saturday, May 12, 2007
MAWE YA MWANZA!

Ukiambiwa uzitaje nchi ambazo zimejaliwa kuwa na mandhari nyingi tofauti na za aina yake usisite kuitaja nchi yetu ya Tanzania. Kama kuna mtu anabisha anyoshe kidole. Pichani ni mawe yaliyoko pembezoni mwa Ziwa Victoria jijini Mwanza. Hivi tukilisukuma lile jiwe pale juu litaanguka? Picha kwa hisani ya Ebby Mkandara, mkazi wa hapa Toronto aliyetembelea kanda hiyo ya ziwa hivi karibuni.
 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 5:37 PM | Permalink | Maoni 7
Friday, May 04, 2007
UNAHESHIMU UHURU WA HABARI?

Jana ilikuwa ni siku ya uhuru wa habari duniani. Kama tunavyojua, uhuru wa vyombo vya habari ni vita ambayo tunaweza kusema haina mwisho. Waandishi wa habari bado wanatishiwa, wanauawa, wanatiwa gerezani, wanapigwa, wanateswa wao wenyewe na wakati mwingine hata familia zao. Hivi sasa tunapoongelea “waandishi wa habari” hatuwezi kusahau dhana mpya ya uandishi wa umma (citizen journalism) ambamo wanablog nao wanakuwamo. Blog ni tishio jipya kwa wale wasiopenda au kuheshimu uhuru wa habari.


Tangu uandishi wa umma uanze kuchanua baadhi ya wanablog wameshatiwa ndani, wameshashtakiwa, wamenyanyaswa nk Mfano mzuri ni kesi hai ya wanablog wa huko Misri Kareem Amer na Abdul Moneim Mahmud kama ambavyo imeanishwa katika tovuti ya Maripota wasio na mipaka au kwa kizungu Reporters Without Borders ambao kazi yao kubwa ni kutetea haki za waandishi wa habari na pia kuibua hadharani madhambi wanayofanyiwa waandishi wa habari wakiwemo wanablog.

Je, wewe unaheshimu uhuru wa vyombo vya habari? Kama ndio basi tembelea tovuti ya Maripota wasio na mipaka kisha usaidie kwa kutia saini petition mbalimbali ili kusaidia kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari kitu ambacho ni muhimu sana katika kujenga jamii zinazoheshimu demokrasia, haki za binadamu na maendeleo.

Kwa kumalizia hebu soma habari hii ya jaji mmoja huko Washington anayedai jamaa wa Dry Cleaner wamlipe dola milioni 65 kwa sababu walimpotezea suruali yake! Huku Marekani ya kaskazini watu wanapenda kushitakiana si mchezo.

 
Muandishi: Jeff Msangi |Tarehe: 10:09 AM | Permalink | Maoni 1
   
 
Copyright 2006 © JEFF MSANGI. All Rights Reserved
 
Idadi ya watu Idadi ya watu Idadi ya watu
eXTReMe Tracker